Waziri Mwambe: Mazungumzo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi

Waziri Mwambe: Mazungumzo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi

Who is Dr. Chamuriho....unaambiwa mkataba haukuwepo unaleta undezi hapa simama katika HOJA.
Kwani kinachofanyika sasa ni nini? Si kilekile ambacho kilifanyika awamu ya 5 kikapingwa? Tena wamesema hata kama awamu iliyopita ulikataliwa lakini wataanza tena kule na sipo walipoishia awamu ya 5 ila ilipoishia awamu ya nne. Unajua hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LNG na bandari ya Bagamoyo, huku bado kuna SGR, Nyerere dam, Kigongo Busisi yote miradi mikubwa ya gharama kubwa na bado haijamilika, hii haraka ya nini kama sio nao wanataka 10% zao?
Tutaongeza tozo mpya ili pesa ipatikane ya kufund hiyo miradi.
 
Kwani kinachofanyika sasa ni nini? Si kilekile ambacho kilifanyika awamu ya 5 kikapingwa? Tena wamesema atakama awamu iliyopita ulikataliwa lakini wataanza tena kule na sipo walipoishia awamu ya 5 ila ilipoishia awamu ya nne. Unajua ilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mwendazake yale maneno aliokuwa anadanganya Umma wa Watanzania aliyatoa wapi, kwa maelezo haya ya Mwambe naamini kwa asilimia mia 100 yule mzee hakuwa na nia ya dhati kutusaidia watanzania... Halafu anasema msema kweli mpenzi wa Mungu... Hakika tutaendelea kumshukuru Mungu.
 
Nafarijika sana naposikia maamuzi yenye tija kama haya yanafanyika. Bandari ya Bagamoyo ni mkombozi kwa ajira za vijana wetu wanaomaliza ngazi mbalimbali za elimu
Hapana.
Sio kweli na sio sahihi.
Toka mkoloni mpaka leo hii mikataba imekuwa pigo kwa kila mlalahoi, huu wa Bagamoyo utakuwa na maajabu gani?
Kuweka mambo sawa, hivi huu mkataba ulishawahi kuuona popote mpaka uushangilie?
 
Waziri wa uwekezaji Mr Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Source: ITV habari
Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Waziri wa uwekezaji Mr Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Source: ITV habari
Safi sana Mama
 
Sasa mwendazake yale maneno aliokuwa anadanya Umma wa Watanzania aliyatoa wapi , kwa maelezo haya ya Mwambe naamini kwa asilimia mia 100 yule mzee hakuwa na nia ya dhati kutusaidia watanzania... Halafu anasema msema kweli mpenzi wa mungu... hakika tutaendelea kumshukuru mungu.
Katika hili siwezi kumlaumu au kumpongeza Magufuli. Alichokifanya Kikwete ndio hicho hicho alichokifanya Magufuli na ndio hicho hicho anakifanya Samia kwenye hili la bandari ya Bagamoyo. Marais wote hao wanatulisha upepo wa sumu za matango pori, hakuna kati yao aliyetuletea kwanza huo mkataba tukausoma na kuuchambua ili kujua mbichi na mbivu.
 
Katika hili siwezi kumlaumu au kumpongeza Magufuli. Alichokifanya Kikwete ndio hicho hicho alichokifanya Magufuli na ndio hicho hicho anakifanya Samia kwenye hili la bandari ya Bagamoyo. Marais wote hao wanatulisha upepo wa sumu za matango pori, hakuna kati yao aliyetuletea kwanza huo mkataba tukausoma na kuuchambua ili kujua mbichi na mbivu.
 
Sasa bado najiuliza hivi ilikuwaje kwa Rais Kikwete tarehe 16/10/2015 pale bagamoyo aliweka jiwe la msingi la kuanza kujengwa bandari hiyo ya Bagamoyo ikiwa mkataba ulikuwa bado haujasainiwa?

Hawa jamaa wanatufanya sisi mazuzu.
 
Sasa bado najiuliza hivi ilikuwaje kwa Rais Kikwete tarehe 16/10/2015 pale bagamoyo aliweka jiwe la msingi la kuanza kujengwa bandari hiyo ya Bagamoyo ikiwa mkataba ulikuwa bado haujasainiwa?

Hawa jamaa wanatufanya sisi mazuzu.
Mkataba ulishawahi kuuona, Prof. Assad alishawahi kuomba Documents za Bagamoyo port hakupewa, kumbe hazipo....sasa naelewa kwanini hamkupenda Assad.
 
At last, dalili za mradi wa Bandari ha Bagamoyo sasa zimeanza kuonekana.

Taarifa ya Habari ITV, saa mbili ya jioni hii Waziri wa Biashara na Uwekezaji , Ndg Mwambe, ametamka kuwa maongezi karibu yataanza juu ya utekelezaji wa agizo la Rais Samia kupitia mambo yote yaliyoongelewa katika hatua za awali na kama kulikuwepo na mkataba.

Waziri Mwambe amesema HAKUNA mkataba wowote uliokuwepo kati ya serikali na wawekezaji toka China na mawasiliano yataendelea ili mradi huo ufikie hatua za utekelezaji.

MY TAKE
Tumerudi nyuma sana katika miaka hii sita iliyopita, tugange yajayo, yaani uchumi endelevu, yaliyipita si ndwele.
Kwa mswahili uliye Bagamoyo, tunza arhi yako kama mboni ya jicho,” Kurasini” ya pili yaja.
 
Huo mkataba utawekwa hadharani ili kuondoa wasiwasi uliogubika utekelezaji wa huo mradi?

Kusema tumerudi nyuma sana miaka sita iliyopita ni ulevi tu, kama ulivyo ulevi mwingine wowote, kwani ni awamu ipi hili taifa liliwahi kwenda mbele?

Ya Kikwete? una hakika ulienda mbele na wewe au wao peke yao, halafu wewe ukabaki msindikizaji huku unashangilia? mnajua sana kuimba mapambio ya kusifu na kuabudu halafu baadae mnakurupuka na kuanza kelele za tunapigwa.
 
Huu mradi masharti yake ya hovyo si yalisemwa hadharani mpaka viongozi waliokuwa kwenye huo mkutano wakaguna…sasa hivi unafufuliwa tena?!

Hivi jamani hii Tanzania ni yetu wote au ya watu wachache…tuwajue basi tuwaombee uhamisho wapate makazi mengine wale asali huko waendako km wanaitamani sana…watuachie Tanzania yetu tujikongoje taratibu…kuliko kuja kulishwa masumu na uwekezaji ambao hauna tija kwetu na ardhi yetu na dawa hospitalini hakuna…
 
Mama anakiuka wosia wa mwendazake - kwamba mwenye akili timamu hawezi kuendeleza au kuukubali huo mradi.
JPM alivuta kamba kuelekea Kanda ya Ziwa, sasa mama anavuta kuelekea baharini.
 
Huu mradi masharti yake ya hovyo si yalisemwa hadharani mpaka viongozi waliokuwa kwenye huo mkutano wakaguna…sasa hv unafufuliwa tena?!

Hv jamani hii Tanzania ni yetu wote au ya watu wachache…tuwajue basi tuwaombee uhamisho wapate makazi mengine wale asali huko waendako km wanaitamani sana…watuachie Tanzania yetu tujikongoje taratibu…kuliko kuja kulishwa masumu na uwekezaji ambao hauna tija kwetu na ardhi yetu na dawa hospitalini hakuna…
Hayo masharti ni yenu ninyi.
Kama yapo si yaweke hadharani kwa nini kuandikia mate.
 
Back
Top Bottom