Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Nimekutana na ujumbe wa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliouchapisha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii nikaona niulete hapa kama taarifa.
Ameandika:
"Nikiwa safarini kuelekea Mombasa kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, nimelazimika kusimama na kusikiliza changamoto niliyokutana nayo mpakani Horohoro ambapo nimekuta foleni kubwa sana ya magari ya mizigo upande wa Tanzania nikadhani shida iko upande wetu.
Katika kuongea na incharge wa KRA na TRA, nikagundua sababu kubwa ni ucheleweshwaji wa huduma ya forodha kutoka Kenya kwa kuwa bado hawajaanza kutumia mfumo wa pamoja wa huduma ya forodha (Single Custom Territory).
Magari yanayotoka Kenya, hayapati foleni kwa kuwa tayari Tanzania tumetumia mfumo wa pamoja wa forodha hivyo mizigo inayoingia nchini huwa inakuwa cleared upande wa Kenya kabla ya kufika mpakani hivyo kurahisisha mizigo kupita.
Nachukua hatua za kuzungumza na Waziri wa Fedha wa Kenya waanze ku-impliment mfumo wa pamoja wa forodha kwa kuwaleta Maafisa wa KRA nchini ili ku-clear mizigo kabla ya kufika Mpakani ili wafanyabiashara wasicheleweshwe mpakani."
Mwisho wa kunukuu.
My take: Hii itakuwa ni habari njema sana kwa madereva wa malori wanaopataga usumbufu pale Horohoro. Mpaka Waziri ameamua kwenda front, tutarajie Kenya watareciprocate vizuri hata kama kuna rafu majirani zetu walikuwa wanazicheza kwa makusudi. Kwa hili, Mhe Waziri anastahili pongezi.