Waziri Mwigulu na wachumi wenzako mnalihujumu taifa, rudini mezani

Waziri Mwigulu na wachumi wenzako mnalihujumu taifa, rudini mezani

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Nafikiri Waziri wa Fedha, Dr. Mwigulu Lameck Nchemba na wataalamu wenzake wameshindwa kufanya utafiti makini kujua sababu kuu ya Benki kuanguka huku soko la miamala ya mtandaoni likiimarika kwa kiwango kizuri. Wao kwa uelewa wao wameaminishwa kwamba miamala ya kibenki imepungua kwakuwa tozo za benki zilikuwa kubwa, na njia sahihi wakaona ni bora kupunguza tozo hizo za benki.

Hatua ya pili wakaona soko la miamala ya kimtandao limeimarika ambapo uchumi wa Tanzania kwa sehemu kubwa umeshikiliwa kwenye (Mpesa, Tigopesa, Halopesa, Airtel Money nk) hivyo ili kurudisha uhai wa bank wakaona bora wapandishe tozo huku mara mbili ya tozo za awali. Wakiamini watu watarudi kwenye bank. Hili ni kosa kubwa wamelifanya, hawakutaka kuumiza vichwa vya kujiridhisha ni uchumi wa aina gani hasa uko kwenye hii miamala ya kimtandao. Utafiti usio rasmi ni kuwa miamala ya simu inatumiwa na kundi kubwa la masikini katika nchi ambao vipato vyao ni chini ya mstari wa umasikini unaotambuliwa na Umoja wa Mataifa under poverty line wanaoishi chini ya dola 5.50 kwa siku.

Utafiti usio rasmi unaonyesha kuwa kwa miaka mingi Mabenki ya Tanzania ni adui wa masikini na kwa Tanzania masikini ni 91.80% ndio wanaishi chini 5.50 na ndio wanamiliki uchumi na miamala ya simu. Leo Bibi yangu Mgulwa kule kijijini Maduma hawezi kwenda bank wala hana uwezi wa kumiliki account ya benki ili nimtumie 10,000 ya sukari badala yake nitalazimika kugonga kokoto huku Mbutu ili nipate 15,000 nimtumie Bibi yangu kwa Tigo Pesa.

Kwa miaka 15 hivi huduma hii ya miama ya kimtandao imekuwa mkombozi wa kundi hili la masikini. Leo unawafungia huduma hii ili waende bank ambazo nyingi zimefunga matawi yake kutokana na utawala dharimu uliopita na sasa Benki hizo ziko Dar tu na huduma za kibenki zenyewe ni mbovu kupita maelezo. Unataraji ukuze uchumi au uangushe zaidi uchumi? Njia bora ilitakiwa Mabenki hayo yaingie kwenye ushindani na mitandao ya simu kwakubuni njia anuwai za kimasoko na si kutegemea mkono wa serikali iwabebe, biashara ni ushindani, serikali itafute vyanzo vingine vya mapato katika madini, misitu, uvuvi, bandari nk... Badala ya kuendelea kumnyonya huyu masikini wa chini.

Screenshot_20210715-102501.png
IMG_20210715_104407_742.jpg
IMG_20210715_104407_697.jpg
IMG_20210715_104407_716.jpg
 
Sasahivi tuna serikali ya ujanja ujanja

Kodi zingekuwa zinatumika ipasavyo hakuna shida

Ila kwa matumizi haya ya Dar-Dodoma kila siku kujaza mafuta mawaziri kukimbizana tu hapana

Mimi pesa yangu yeyote kama unanidai kama hakuna account bank sikulipi pia na wewe usinilipe kama hauwezi kuniletea au kulipia bank!!
 
Unachekesha sana!

Swali la kujiuliza kwani hayo makato yanaenda mfukoni mwa Mwigulu au yanaenda kusaidia ndugu zako walioko kijijini na mjini?

Waswahili wanasema nguo ya kuazima haifichi makalio. Maendeleo ya Watanzania yalikuwa yanategemea zaidi misaaada kutoka ktk kodi za mataifa mengine, sasa leo hii watanzania wanazoweshwa kujitegemea kwa kuchangia maendeleo yao wenyewe ww unaleta ngojera?

Kwa hiyo unataka maendeleo ya Watanzania yachangiwe na watu wa nchi za Ulaya? Ahhh! kweli ulizoea kitonga, sasa ndio mjue kwa nn wazungu wakali na pesa zao wanapo zitoa kama mikopo kwa mataifa ya kiafrika, ni kwa sababu Raia wao wanjinyima kutoka ktk makato ya kodi.

Sasa leo hii kodi kidogo tu tunaanza kulia, mbona nchi ikiwa inakopa kulimbikiza madeni hampigi kelele kuwa nchi yetu inakopa sana?!
safari hii Watanzania tumeamua kuchangia maendeleo yetu sisi wenyewe, Chadema kama hawataki wahame nchi.
 
Wanamuhujumu mama kumbuka mwigulu na genge lake wanautaka uraisi 2025 hivyo wameanza mapema kumuharibia huyu mama achukiwe na wananchi kodi ya uzalendo
 
Wakuu tujaribu kutazama maoni ya wadau mbalimbali juu ya Gharama Mpya za miamala iliyiwekwa na serikali yetu tukufu chini ya madam president na waziri wa uchumi kijana kijana flani,

IMG_20210715_113719.jpg


IMG_20210715_115523.jpg


IMG_20210715_115250.jpg


IMG_20210715_115233.jpg


IMG_20210715_115210.jpg


IMG_20210715_123102.jpg
 
Back
Top Bottom