VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine, ni mkuu wa nchi na mkuu wa Serikali. Kuongoza nchi na Serikali ni kuongoza watanzania wote: furaha na karaha zao huelekezwa kwa Rais. Mazuri yao na mabaya kwao wananchi husemwa kuwa yametokana na uongozi wa Rais aliye madarakani. Kwasasa, Rais wetu mpendwa ni Mama Samia Suluhu Hassan. Yeye ndiye dira yetu, nguzo yetu, tegemeo letu na nembo yetu.
Katika kutekeleza majukumu yake, Rais huwa na wasaidizi wake. Wapo wanaochaguliwa; wanaoteuliwa na hata anaowakuta anapoingia madarakani. Mawaziri ni kati ya wasaidizi wa Rais. Wao hubeba na kuzitekeleza ajenda/sera za Rais katika Wizara zao na kuzisimamia. Mawaziri ni mikono ya Rais. Mikono hiyo inapofurahisha, wananchi humfurahia Rais. Inapoumiza, wananchi humlalamikia na 'kumchukia' Rais.
Waziri wa Fedha, Daktari wa Falsafa Mwigulu Nchemba amekuwa gumzo lenye mzozo na kodi zake za miamala ya fedha kimtandao na hata kupanda kwa tozo kwenye mafuta na bidhaa nyinginezo. Amekosolewa na anaendelea kukosolewa kwa sauti kuu ya wananchi pamoja na kuziita kodi hizo kuwa ni kodi za kizalendo. Ajue kuwa uzalendo huwa haulazimishwi. Uzalendo ni uhiyari na utayari. Kulazimisha kodi si kulazimisha uzalendo. Ni kuubomoa.
Waziri Nchemba ameteleza. Amekosea pakubwa kwenye kodi husika. Amekaribisha madhara makubwa ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha na hasara yenye hasira kwa wahusika wa huduma za kifedha. Wananchi wanaweza kuwa na 'mgomo' kwenye matumizi ya huduma hizo. Huduma zitaathirika na hata kufa. Uwekezaji utaathirika. Hasira na chuki kwa Rais. Uchonganishi. Bidhaa na huduma zitapanda bei. Maisha yatakuwa magumu. Hasira kwa Rais. Uchonganishi.
Nani hasa amekutuma huku akihema Waziri Nchemba umchonganishe Rais na wananchi wake? Kwa lengo lipi? Kwa faida ya nani? Ili iweje? Waziri Nchemba, amini nakwambia, hautafanikiwa. Rais Samia hatakubali kuchonganishwa na wananchi wake kupitia kodi na tozo. Atachukua hatua. Atajilinda. Atajitetea. Ataibuka mshindi. Lengo lako limeshajianika, halitafanikiwa.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)