Jibu unalo mwenyewe.Nyerere pamoja na kuiongoza nchi yenye raia milion 9 tu tena akiwa ameachiwa na viwanda na wakoloni,bado raia waliishi kwa kuvaa magunia.Mwinyi alipochukua nchi kwa miaka 10 tu,tukapata kina Kishimba,kina Bhakharesa na wengine wengi tu.Raia wakaweza kujenga makazi,kufungua viwanda vidogovidoka kama mashine za kukoboa na kusaga,maduka n.k.
Mkapa akaja na kuudorolesha uchumi wa wananchi kwa namna alivyoweza mpaka mtaani pakawa pagumu tena.Na ni yeye Mkapa ndiye aliyeanzisha ufisadi serikalini.Yeye mwenyewe akijimilikisha mali za umma kikiwemo kiwanda cha sukari Mtibwa.
Sasa angalia utawala wa Kikwete ulivyofungua uchumi wa raia na angalia utawala Magu ulivyozorotesha uchumi wa raia mtaani.
Usifikiri waziri Ummy alikurupuka tu kuruhusu watoto waende shule hata na nguo za nyumbani ukafikiri ni amepagawa.