Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 433
Serikali imetangaza mpango wa kuanzisha Youth Special Economic Zones (YSEZ) utakaotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa lengo la kuwawezesha vijana kuingia kwenye uchumi wa uzalishaji na utengenezaji badala ya uchumi wa usambazaji na uuzaji pekee.
Akizungumza kuhusu mpango huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema Serikali inalenga kujenga kundi kubwa la vijana wazalishaji na watengenezaji ili kuharakisha ukuaji wa uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa vijana wenzao.
Soma pia: Waziri Nanauka: Vijana hawana taarifa za fursa za serikali
Amesema kupitia Youth Investment Program, Serikali inalenga kuwezesha kuanzishwa kwa kampuni za vijana takribani 100,000 kote nchini ndani ya miaka mitano ijayo. Kati ya kampuni hizo, 20,000 zitapewa nafasi maalum ndani ya Youth Special Economic Zones, ambapo vijana watawezeshwa kwa mazingira rafiki ya uwekezaji.
“Hatua hii inalenga kututoa kwenye distributive economy na kuelekea kwenye manufacturing and productive economy. Tunataka vijana wasiwe wasambazaji na wachuuzi pekee, bali wawe wazalishaji na watengenezaji wenye uwezo wa kuajiri wengine,” amesema Waziri Nanauka.
Ameeleza kuwa Serikali itaweka mkakati maalum wa ufadhili na mikopo nafuu kwa vijana, hususan katika ununuzi wa mitambo na mashine za uzalishaji. Mitambo hiyo itawekwa moja kwa moja ndani ya Youth Special Economic Zones, ambako kutakuwepo miundombinu yote muhimu ikiwemo maji, umeme na huduma nyingine za msingi.
Aidha, maeneo hayo yatakuwa na one stop center kwa ajili ya huduma zote za kiserikali na udhibiti, ikiwemo BRELA, SIDO na OSHA, ili kupunguza urasimu na kuwasaidia vijana kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa urahisi.
Kwa vijana wanaolenga masoko ya nje, Serikali imesema itatoa msaada maalum wa kiufundi na kisheria ili kuwawezesha kuzalisha kwa viwango vinavyokubalika kimataifa na kushiriki kikamilifu katika biashara ya kimataifa.
Waziri Nanauka ameongeza kuwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TSEZA), lengo ni kila kampuni ya vijana iweze kuajiri angalau vijana 50. Kupitia mpango huo, Serikali inatarajia kuzalisha ajira takribani milioni moja kwa vijana nchini.