Waziri Nape aagiza wamiliki wa “Abroad Tv” wakamatwe kwa upotoshaji

04 November 2022

TANZANIA ITAFAIDIKA NA YAPI ?

Rais Samia Suluhu Hassan yuko ziarani nchini China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping huku akiweka historia.

Mbali ya hilo, wakuu wawili hao wameshuhudia kutiwa saini mikataba ya makubalino kwenye maeneo 15. Mchambuzi Godwin Gonde anatufahamisha

Source : Azam TV
 
Premier of the State Council Li Keqiang and Chairman of the Standing Committee of the National People’s Congress Li Zhanshu had separate meetings with President Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu wa China akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania​

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2022
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang akikutana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anayezuru China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Novemba 3, 2022. (Xinhua/Zhai Jianlan)​

BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anayezuru Beijing siku ya Alhamisi.

Akipongeza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tanzania, Li amesema Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefanya mipango mkakati kwa ajili ya maendeleo ya China katika kipindi kijacho, na China itaendelea kusukuma mbele kufungua mlango kwenye kiwango cha juu.

Li amesema China iko tayari kushirikiana na Tanzania ili kuongeza kushabihiana kwa mikakati ya maendeleo, kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile uchumi na biashara, nishati, afya, kilimo na uvuvi, na kuboresha mabadilishano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

“China iko tayari kupanua uagizaji wa bidhaa za Tanzania zinazokidhi kuingia sokoni na kuhimiza makampuni ya China kuongeza uwekezaji nchini Tanzania,” amesema Li, na kuongeza kuwa upande wa China unatumai kuwa Tanzania itatoa uungaji mkono unaohitajika.

Kuhusu uhusiano wa China na Afrika, Li amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika kwenye msingi wa ukweli na usawa, kuongeza mshikamano na kuaminiana, na kutafuta maendeleo jumuishi na endelevu.

Kwa upande wake, Rais Hassan ameishukuru China kwa uungaji mkono na msaada wake kwa Tanzania kwa miaka mingi, akisema Tanzania inashikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja na imejitolea kuendeleza urafiki wake wa jadi na China.

Amesema Tanzania itatekeleza matokeo ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kuhimiza ushirikiano katika masuala ya biashara, uwekezaji, kilimo, uvuvi, miundombinu na mabadilishano kati ya watu na watu.

“Tanzania inakaribisha uwekezaji kutoka kwa makampuni ya China,” Samia ameongeza.

Source : kwa hisani kubwa ya : Wahariri wa tovuti: Song Ge, Zhao Jian : www.swahili.people.cn
 
Nilidhani Nape ameguswa na kilio chetu na kuzungumzia ishu ya wizi wa bando...

Kumbe kuichafua serikali inakula loss kubwa🤣
Nape yuko sawa katika hili unapo report kitu cha uwongo juu ya serikali au hata mtu lazima uwajibike. Ikitokea chombo cha habari kumchafua mtu binafsi na ikawa habari zile sio za kweli una haki ya kuwashtaki sembuse serikali? ule ni mkutano wa nchi na nchi yale mazungumzo sio ya public serikali ikitoa ndio unawafakishia wananchi. Nape yuko sahihi hizo online TV hovyo sana nyingi
 
Waziri yupo sahihi, China wanatupa mihela bila masharti yoyote.

Hao Tv wakamatwe ingawa ndio naiskia leo hiyo TV.
 
Nape atakuwa aliomba rushwa na hiyo TV akanyimwa. Siyo kwa makasiriko haya.
 
Good, huyo aliyepotosha ruksa kukabwa mabumbu!
 
Anasema huo ni uongo wakati hasemi ukweli ni upi!!

Aseme kwanza ukweli ni upi ndipo aseme huo mwingine ni uongo!!

Yeah:
Kinachofanya watu wafoji na kuchafua ni kwa sababu hii misaada ya nasharti nafuuu kua hatuambiwi ukweli (mengi hufichwa).

Haya mambo ndio hufanya wananchi wachache waanze kujitungia habari zao ingawa ni kosa kisheria!
 
Haya mambo ndio hufanya wananchi wachache waanze kujitungia habari zao ingawa ni kosa kisheria!
Kwani wao si wanafanya kwa niaba ya watanzania wenzao. Siri ya nini sasa?

Hayo madeni yatalipwa na sisi sote.
 

Kama serikali ni ya waongo usishangae wananchi kuongea uongo kuhusu serikali hiyo. Nini mtu mjinga tu anaweza kuitetea serikali kwenye mikataba ambayo ni siri.
 
UTAFITI:CCM namba 3 Kwa Rushwa Duniani
1. NRM- Uganda 86%
2.ZANU–PF -Zimbabwe79%
3.CCM -Tanzania 76%
4.AZIMIO - KENYA 67%
5. CCC - Zimbabwe 63%
6. FCC - Congo 56%
7. SDF FSD- Cameroon 51%
8. GPPSB- Venezuela 50%
9. UPFA- Sri Lanka 49%
10.ANC - South Africa 46%
Source :AFGlobal..... Utafiti wao mwingine huu hapa
 
Kama serikali ni ya waongo usishangae wananchi kuongea uongo kuhusu serikali hiyo. Nini mtu mjinga tu anaweza kuitetea serikali kwenye mikataba ambayo ni siri.
Kuna mkataba gani sio siri? mkataba nipande mbili sio Tanzania tu ni mikataba ya kisheria sio karatasi zinaend public na hata mikataba binafsi inapitiwa na wahusika tu. Sasa sielewi ni nchi gani ulisikia au ofisi gani wakaweka mikataba hadharani, hata mwajiri na mwajiriwa ni siri. Halafu Tanzania hii nani wakusoma mikataba toka lini? wa Tz wanasoma umbea tu mambo ya msingi wanaruka hata ukileta gazeti ukiandika mambo ya maana watafungia vitumbua tu. Mkataba unweza kukuta una paper zaidi ya 50 lugha kizungu tuacheni kulaumu tu lugha ya kimikataba ni wanasheria tu wanaweza kupitia na wakaelewa na sisi tuna mwanasheria wa serikali.
 
Sijasema hayupo sawa
Ninaongelea vipaumbele.

Huwezi ukatoa maagizo bias tena publicly. Ninaposema bias namaanisha ameegemea kuilinda serikali lakini kabla haijachafuliwa kuna hoja zaidi ya alfu kuhusu uharamia wa mitandao na bando kuibiwa na cartel ya watoa huduma


Hii ni serikali ambayo wqtendaji wake wengi hawajali malalmiko ya wananchi.

Sheria za anayetoa taarifa za uongo ipo na siyo mpaka kujifaragua majukwaa i ili kuonesha unaisimamia kudefend mfumo ambao katu hakuna anayeweza kuuonea.

Wananchi hawana mtetezi, hawana pa kukimbilia kwa sababu serikali INAJILI DA dhidi yao
 
Tumesha jua ila yeye ataenda kujitetea kivyake kwa pilato
 
Kuichafua serikali?
Kwani serikali yenyewe ni safi na maji hayatoki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…