Waziri wa habari, Nape Nnauye ametangaza kurejeshwa kwa 'Free local channels' kwenye king'amuzi cha DSTV alipofika ofisi za Multichoice Tanzania akiyataja kama maagizo ya Rais Samia kurekebisha kanuni na Sheria.
Agosti 12, 2018 DSTV ililazimika kuondoa chaneli za FTA baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini kuipiga mkwara wa uwezekano wa kuifutia leseni endapo itaendelea kwani ilikuwa hairuhusiwi kulipia chaneli hizo zinazopaswa kuwa bure.
Uamuzi huu pia iliwadhuru wote waliokuwa wanaendesha ving'amuzi kwa mfumo wa 'DHT' ambao iliwajumuisha pia Azam na Zuku ambao wenyewe waliamua kufata masharti na baadae kuruhusiwa.
Waziri wa mawasiliano wa wakati huo, Dkt. Mwakyembe akitoa sababu za kuzuia, alisema leseni ya kampuni hizo tatu ilikuwa na maudhui ya kulipia(Pay TV) hata kwa chaneli za FTA na pesa ikiisha zinazimwa kama luku. Pia alisema miundombinu yao ya urushaji matangazo haiko nchini.
Mwakyembe alisema waandaji wa maudhui(TV Stations) wana uhuru wa kuchagua TV zao ziwe za umma au kulipia na wakichagua za umma mapato yao yanatokana na matangazo ya biashara pekee bila kumtoza mteja kitu ambacho alisema DSTV walikiuka.
Pia, soma=>
Waziri Mwakyembe: Azam, Zuku na DSTV walirusha maudhui ya ndani kinyume na leseni zao! Lazima warejeshe fedha zote walizowatoza Wananchi
View attachment 2102845View attachment 2102846View attachment 2102847