Waziri Nape: Hatujaibania starlink kutoa huduma ya intaneti, Elon Musk bado hajakidhi vigezo tulivyomuwekea

Waziri Nape: Hatujaibania starlink kutoa huduma ya intaneti, Elon Musk bado hajakidhi vigezo tulivyomuwekea

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nnauye amesema serikali ya Tanzania iliitaka kampuni ya Starlink inayomilikiwa na Elon Musk kuweka ofisi zake hapa nchini ili waweze kulinda data za watumiaji na kuwajibika kwa watanzania.

Source:

Huyu jamaa anatumiwa na makampuni ya simu yanayotukamua pesa nyingi kwa mb chach, sasa hii ni outright hujuma ya kutaka kulinda ulaji wao kwenye Mb. Hiyo sababu aliyotoa ni ya kitaahira kabisa.., unalinda vipi sasa kwa kuzuia kampuni ya huduma ya mawasiliano? Au hao wanatofauti gani na hizi kampuni zilizopo? Mfano Instagram ofisi zao zipo wapi hapa nchini?
 
Serikali ni mnafaika namba moja wa mitandao ya simu kupitia tozo za kimagumashi na bando zilizojaa dhulmat na uonevu usioelezeka.Hivyo sio ajabu kumpiga Pini mwamba ili asiharibu maslahi yake.Ila khabari njema ni kwamba teknolojia haizuiliki Bali utajichelewesha baadae utahitaji wewe mwenyewe.

Enzi Skype inaingia Tanziania waliigomea Kwa kuogopa itaharibu soko la TTCl kwamba wateja wao watahawama.Njia sahihi wakaona ni kuweka vikwazo vya kutosha lakini baadae wanajua ilikuja ikawaje.Serikali inayojali raia wake ilitakiwa iwe imeshweka mazingira sawa Kwa huyu mwekezaji na kuangalia namna nzuri ya wao kupata faida kutokana na huo uwekezaji.

Hapo wameshaona mwamba ataenda kukata mirija Yao mingi ya hela za wadanganyika.Uzuri ni kwamba Elon musk akitua nchi yoyote Africa mashariki access ya nchi yoyote kufungiwa internet inakuwepo.Jiandaeni na watu wenu wa makampuni muda wowote mtaanza kulia na kusaga meno coz mtetezi wa technologia hayupo mbali na sisi wanyonge
 
Mimi ni mwanaCCM kindaki ndaki siyo shabiki
Nauliza tu mbona analipia $8 twitter wakati HQ ipo US huyu mjamaa sijawahi kubali IQ yake bora hata FA angepewa hii wizara
Sasa kulipia huduma unayopata utalinganisha na kampuni inayotaka kuja kutoa huduma kwako?Hapo lazima vigezo masharti vifuatwe,mlivyoweka kama vipimnavibadirisha tu.
 
Nape wacha siasa, Elon Musk ofisi ya nini hapa Tanzania? Si anaweka mawakala tu kama wanavyofanya konnect.

Sema mpaka awe na God Father wa uhakika. Mpeni Rostam tu, hakuna zaidi, yupo kwenye sector hiyo na anajuwa kula na vipofu.
 
Nape na serikali yake wanataka ofisi ili wasiojulikana waweze kuwafikia ofisini mwao ikihitajika, hilo tu hakuna jingine.
Ofisi ina faida gani. Mtandao ndio shughuli zao, ukiwataka wanaptikana kila saa. Ofisi moja kwa dunia nzima. Hawa tatizo wanataka mambo ya kuzima data, na pia hawa wengine ie. Vod., airte., na wengine hawataki ushindani hapo.
 
Ni huduma ya nini ile? Mimi napiga Instagram video call kila siku, whatsapp ofisi zao zipo wapi? Au mawasiliano ni nini?
Mkuu jaribu kuelewa ni vitu vidogo hivyo!!tofautisha njia za mawasiliano na huduma !!basi kama Instagram ni huduma ya mawasiliano kama unavyodai,usiweke bundle kwenye line yako ,then jaribu kuwasiliana!

Kwani hata Tv/Radio si zipo za nje lakini si zinasikika hapa nchini,kupitia njia mbalimbali,lakini kuna zile zinazorusha vipindi vyao kutokea studio zao zilizopo nchini na ni za kimataifa?!kuna sheria yake ambayo ni tofauti na zile unazozipata kupitia internet.
 
Mkuu jaribu kuelewa ni vitu vidogo hivyo!!tofautisha njia za mawasiliano na huduma !!basi kama Instagram ni huduma ya mawasiliano kama unavyodai,usiweke bundle kwenye line yako ,then jaribu kuwasiliana!!
Kwani hata Tv/Radio si zipo za nje lakini si zinasikika hapa nchini,kupitia njia mbalimbali,lakini kuna zile zinazorusha vipindi vyao kutokea studio zao zilizopo nchini na ni za kimataifa?!kuna sheria yake ambayo ni tofauti na zile unazozipata kupitia internet.
Njia za mawasiliano ni barua, simu, barua pepe, fax, simu za Internet, radio calls nk. Unapotumia njia hizi za mawasiliano toka kwa mtoa huduma wako ndio tunaita huduma za mawasialiano.

Watoa huduma ni kama Shirika la Posta Tanzania (barua), TTCL (simu), Google (barua pepe za gmail) , Whatsapp (simu za internet).

Haya, futa ukichoandika au pinga nilichoandika, chagua moja.

Inwhich case uniambie, ofisi za whatsapp nchini zipo wapi
 
Njia za mawasiliano ni barua, simu, barua pepe, fax, simu za Internet, radio calls nk. Unapotumia njia hizi za mawasiliano toka kwa mtoa huduma wako ndio tunaita huduma za mawasialiano...
Umekuja vizuri sasa hiyo huduma ya Instagram utaipataje bila kuwa na mtoa hudumu wa internet?ambaye kwa sasa ni kampuni za simu zilizopo nchini!bila huyu hiyo huduma huwezi kuipata.kuipata hiyo WhatsApp unatumia miundombinu iliyopo wapi unapokuwa Tanzania?

Mambo ya kisheria sio mepesi hivyo kama mnavyotaka iwe!!
 
Umekuja vizuri sasa hiyo huduma ya Instagram utaipataje bila kuwa na mtoa hudumu wa internet?ambaye kwa sasa ni kampuni za simu zilizopo nchini!bila huyu hiyo huduma huwezi kuipata.kuipata hiyo WhatsApp unatumia miundombinu iliyopo wapi unapokuwa TZ?!!
Mambo ya kisheria sio mepesi hivyo kama mnavyotaka iwe!!
sasa hapo nami si nitakuuliza tutapataje hiyo internet bila Iphone, Samsung nk?, haya niambie ofisi zao zipo wapi hapa nchini?
 
Back
Top Bottom