Waziri Ndalichako better late than never; Mikopo ya elimu ya juu hailipiki sababu ya Value Retention fee ya 6%

Waziri Ndalichako better late than never; Mikopo ya elimu ya juu hailipiki sababu ya Value Retention fee ya 6%

Leverage

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
2,125
Reaction score
3,150
Mikopo ya elimu ya juu hailipiki na huu ndio ukweli sababu ya ujinga wa Value Retention fee ya 6%.

Mfano: Mnufaika asiye na ajira rasmi anatakiwa kulipa 100000 au 10% ya kipato anachokilipia kodi kwa mwaka. Mimi nilifungua stationery walipokuja kunikadiria kodi nilitakiwa kulipa 200,000/= kwa mwaka.

Kwahiyo 10% yangu ni 20,000/= ndio natakiwa nilipe bodi kila mwezi. Mkopo wangu ni milioni 10. Nikilipa kwa mwaka nitalipa laki 2.4. Deni litabaki milioni 9 na laki 7 na sitini elfu.

Mwaka unaofuata hili litaongezeka kwa 6% ambayo ni sawa na laki 5 na point hivyo deni langu litarudi milioni 10 laki 3. Kwa hali hii nani atajileta kwa hiari?

Bado kuna wale vijana waliosoma nje ya nchi ada zao kwa dola kisha wakija nchini mishahara laki 7, unafikiri deni watamaliza?

Peleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya HESLB ili tuone kama kweli elimu yako ya uprofesa ni genuine.

Muda bado upo.
 
Huyo unayemuomba mwenyewe muda huu amechanganyikiwa kuandaa vitabu vya somo la historia ya Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa chekechea mpaka chuo kikuu!

Sijui hata kama ana muda wa kuusoma huu ushauri wako! Maana ana upigania huo Uwaziri wake kwa namna yoyote ile baada tu ya kutishiwa kutumbuliwa kwa ulegevu wake na kusuasua kuanzisha hilo somo haraka, na Mzalendo namba 1 Nchini.
 
Lipa madeni ya serikali na wengine wakope ili wasome kama wewe ulivyo someshwa. Kwani kuomba mkopo ulilazimishwa? Kama ulijua huo mchanganuo, kwanini hukukataa kuchukua huo mkopo? Umeanza kuleta michanganuo ya deni na ukali wake baada ya kuhitimu shahada yako. Unafahamu kuwa wapo ambao wamesitisha masomo baada ya kukosa huo mkopoo? Dawa ya deni nikulipa.
 
Mimi namsihi sana mh waziri, akaze uzi huo huo, kwani hata watoto wake na wajukuu na pia vitukuu wake nao watalipa hivyo hivyo,,na pindi wakati wake wa kwenda mbinguni ukifika, Mungu atamshukuru kwa kusimamia mapato vizuri na hivyo kuwezesha maendeleo ya nchi na wizara kwa ujumla.

Makato ya 6%, yaendelee kama kawaida na waziri history itamkumbuka kwa kusimama kidete kutetea maslahi ya nchi.
 
Back
Top Bottom