Waziri Ndejembi aagiza kuundwa kwa kamati ya Uchunguzi wa hitilafu ya Gridi ya Taifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
c82c85fb-36e6-4482-bbef-7fc713952a1f.jpeg

📌 Taarifa ya Kamati itaiwezesha Serikali kuchukua hatua ili tatizo hilo lisijitokeze tena.

Waziri wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi (Mb.), amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu kuunda kamati ya uchunguzi itakayobaini chanzo cha hitilafu iliyojitokeza katika Gridi ya Taifa jana, Juni 27, 2026, na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini, ili kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua za haraka na kuhakikisha tatizo hilo halijitokezi tena.

Waziri Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo, Juni 28, 2026, Ubungo jijini Dar es Salaam katika Kituo cha usimamizi wa Gridi ya Taifa, ambapo ameelekeza kamati hiyo ishirikishe wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwa na jukumu la kufanya uchunguzi wa kina na kupendekeza hatua za kudumu za kuzuia matukio kama hayo kujirudia.
c13fe09f-26a1-44b9-9355-2c4bab2e40b5.jpeg
544926d1-1c56-4201-b368-c43bda48811d.jpeg

Waziri Ndejembi amemtaka Mtendaji Mkuu wa TANESCO kuwasilisha taarifa ya awali ndani ya wiki moja ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua za haraka, wakati Kamati ikiendelea na uchunguzi wa kina.

Aidha, Waziri Ndejembi ameiagiza TANESCO kuimarisha mfumo wa Gridi ya Taifa kwa kuweka mifumo madhubuti ya ulinzi na udhibiti ili hitilafu zinazotokea katika eneo moja zisisababishe athari kwa mfumo mzima wa usambazaji wa umeme nchini.

“Kilichokatika jana ni gridi ya Taifa, sio usalishaji wa umeme. Uzalishaji hauna changamoto yoyote lakini baada ya gridi kukatika ilisababisha mitambo ya uzalishaji kuzima kwani ni mitambo ya kisasa” amesema Ndejembi

Waziri Ndejembi amesisitiza umuhimu wa kukamilisha kwa wakati miradi ya kimkakati ya njia za kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400, ikiwemo Chalinze – Kinyerezi na Chalinze – Dodoma, akieleza kuwa ukamilishaji wake utaongeza uthabiti na usalama wa mfumo wa Gridi ya Taifa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema Wizara itasimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri, ikiwemo kazi ya Kamati ya Uchunguzi na utekelezaji wa miradi ya kuimarisha Gridi ya Taifa.

“Tutaimarisha usimamizi wa utekelezaji wa maelekezo haya na kufuatilia kwa karibu miradi ya njia za kusafirisha umeme ili ikamilike kwa wakati, hatua itakayoongeza uthabiti na ufanisi wa Gridi ya Taifa,” amesema Mhandisi Mramba

View attachment 3617625
📌 Taarifa ya Kamati itaiwezesha Serikali kuchukua hatua ili tatizo hilo lisijitokeze tena.

Waziri wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi (Mb.), amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu kuunda kamati ya uchunguzi itakayobaini chanzo cha hitilafu iliyojitokeza katika Gridi ya Taifa jana, Juni 27, 2026, na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini, ili kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua za haraka na kuhakikisha tatizo hilo halijitokezi tena.

Waziri Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo, Juni 28, 2026, Ubungo jijini Dar es Salaam katika Kituo cha usimamizi wa Gridi ya Taifa, ambapo ameelekeza kamati hiyo ishirikishe wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwa na jukumu la kufanya uchunguzi wa kina na kupendekeza hatua za kudumu za kuzuia matukio kama hayo kujirudia.
View attachment 3617626View attachment 3617627
Waziri Ndejembi amemtaka Mtendaji Mkuu wa TANESCO kuwasilisha taarifa ya awali ndani ya wiki moja ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua za haraka, wakati Kamati ikiendelea na uchunguzi wa kina.

Aidha, Waziri Ndejembi ameiagiza TANESCO kuimarisha mfumo wa Gridi ya Taifa kwa kuweka mifumo madhubuti ya ulinzi na udhibiti ili hitilafu zinazotokea katika eneo moja zisisababishe athari kwa mfumo mzima wa usambazaji wa umeme nchini.

“Kilichokatika jana ni gridi ya Taifa, sio usalishaji wa umeme. Uzalishaji hauna changamoto yoyote lakini baada ya gridi kukatika ilisababisha mitambo ya uzalishaji kuzima kwani ni mitambo ya kisasa” amesema Ndejembi

Waziri Ndejembi amesisitiza umuhimu wa kukamilisha kwa wakati miradi ya kimkakati ya njia za kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400, ikiwemo Chalinze – Kinyerezi na Chalinze – Dodoma, akieleza kuwa ukamilishaji wake utaongeza uthabiti na usalama wa mfumo wa Gridi ya Taifa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema Wizara itasimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri, ikiwemo kazi ya Kamati ya Uchunguzi na utekelezaji wa miradi ya kuimarisha Gridi ya Taifa.

“Tutaimarisha usimamizi wa utekelezaji wa maelekezo haya na kufuatilia kwa karibu miradi ya njia za kusafirisha umeme ili ikamilike kwa wakati, hatua itakayoongeza uthabiti na ufanisi wa Gridi ya Taifa,” amesema Mhandisi Mramba.
well done waziri Ndenjembi 🐒
 
Does it mean it could be a cyber attack?
 
Ripoti ya uchunguzi ya waliomteka mzee Kibao iko wapi?

Ripoti ya uchuguzi kuanguka ghorofa Kariakoo iko wapi?

Ripoti ya uchunguzi kuungua soko Kariakoo iko wapi?

Ripoti ya uchunguzi ya waliompiga Tundu Lissu risasi iko wapi?

Wajinga waliisha, kimetafutwa kichaka cha watu kupiga pesa tena hakuna lolote litakalotokea hapo!
 
Education
He attended the University of Dodoma (graduated around 2012).
His early education journey began in 1988, including studies at Cannon Andrew Primary School and Kirugunyembe Secondary School
 
Kina yavuz karazuu au waturuki tuseme in general! Wameshikilia bwawa mpaka walipwe hela zao! Na waziri anajua hlo na sisi pia tunajua! Sasa hizi hela za kuunda kamati , mikutano ya kina g msuguliwa si mngepeleka kupunguza deni? Halafu hivi nzanziba napo ulikata?
 
Kwani msemaji si alishasema ayo ni mambo ya kawaida tu sasa kamati yanini tena?
Msemaji wa nini huyo?

Hapo lazima kuna vichwa vitaliwa.

Chadema wakataka Bunge la Ulaya na senet ya marekani iunde tume, majinga machadema haya.
 
Ina maana sababu ya umeme kukatika jana haijulikani?

Inataka uwe kichaa au chizi kuwasikiliza maneno yao

Msigwa msemaji wa serikali ameshasema ni tatizo la kawaida kutokea jambo hilo hata nchi zingine linaweza kutokea

siku hiyohiyo waziri anakuja kusema inatakiwa kamati sijui tume ifanye uchunguzi kwa wiki moja na kutoa majibu ya awali huku wakiendelea kutathimini kwa kina

je Tanesco haina wataalamu wenye kujua tatizo nini? Mbona kila kiongozi na majibu yake?

posho za hizo kamati ziwekwe wazi pamoja na taarifa ya uchunguzi wao
 
Back
Top Bottom