Waziri Ndumbaro awajibishwe kwa matokeo mabovu Law School

Waziri Ndumbaro awajibishwe kwa matokeo mabovu Law School

Sasa kama wanasoma vitu walivyo soma chuoni na bado wanafeli ina maana hata huko chuoni walikua wanakariri tu!!

Kwani mitihani yote hutolewa kwa nia njema? Kwani wewe umeishia grade gani mkuu?
 
Waziri Ndumbaro aliunda tume ya Mwakyembe mwaka jana kutafuta suluhu ya matokeo mabovu Law School.

Ikumbukwe (kipindi hicho) wadau mbali mbali walilivalia njuga vilivyo suala la matokeo mabovu shuleni hapo.

Majaji waliunda tume yao ambayo waziri Ndumbaro aliwahakikishia suluhu, na kuwa hawakuwa na haja ya kuendelea jitihada zao.

Tume ya Mwakyembe ilikusanya maoni na kuja na yake. Post #2 na #3 ni moja ya maoni yaliyowasilishwa kwa Mwakyembe kama yalivyo.

Kwamba matokeo ya leo ni mabovu kuliko ya yaliyopelekea tume ya Mwakyembe kuundwa:

1. Tume hiyo kumbe ilikuwa ya kazi gani?
2. Pesa za mlipa kodi zilizotumika kwenye tume hiyo kumbe zilitupwa bure?
3. Kwa nini waziri angali ofisini?

Bila aibu waziri alikuwa bungeni kuwasilisha ya kwake kana kwamba hakujatokea kitu. Huku ni kuwakejeli wananchi.

Shit hole countries hazina utamaduni wa kuwajibika. Bila kuwachukulia hatua hawawezi kufahamu wapo kuwajibika na si kumcheza mtu shere.

Waziri huyu awajibishwe kwa kushindwa majukumu yake.

Ieleweke hakuna shule wanayokwenda kusomea kufeli.
Vijana uwakili siyo rahisi hivyo, unatoka chuo mwaka huu mwaka kesho kutwa uwe wakili, ndiyo maana mawakili wanadharaulika sasa kuliko zamani ilikuwa taaluma yenye heshima kubwa mno.
 
UKIHIYO WA WANAFUNZI WAZIRI AJIUZULU? KWELI WAJINGA WAPO WENGI NDIO MAANA MNATETEA WANAFUNZI
NAIPONGEZA LAW SCHOOL KWA KUSIMAMIA TAALUMA
 
Vijana uwakili siyo rahisi hivyo, unatoka chuo mwaka huu mwaka kesho kutwa uwe wakili, ndiyo maana mawakili wanadharaulika sasa kuliko zamani ilikuwa taaluma yenye heshima kubwa mno.

Kwamba uwakili ni rocket science siyo? Kumbe udaktari, uhandisi, na vya namma hiyo ni rahisi sana siyo ndugu?
 
Kwa hisani ya mdau aikambe:

Anaandika mdau:

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
Acha uongo wote tumepita LAW SCHOOL Matatizo ya LAW SCHOOL kubwa ni Wanafunzi
Lugha ni kikwazo kikubwa
Wanafunzi wanadhani ifaulu wa LAW SCHOOL unaamuliwa na Mwalimu mmoja kama Vyuoni
LAW SCHOOL hakuna RUSHWA ya Fedha wala ya NGONO
LAW SCHOOL wanasimamia TAALUMA.
 
UKIHIYO WA WANAFUNZI WAZIRI AJIUZULU? KWELI WAJINGA WAPO WENGI NDIO MAANA MNATETEA WANAFUNZI
NAIPONGEZA LAW SCHOOL KWA KUSIMAMIA TAALUMA

Mtanzania halisi wewe:

"Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza."

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Umetuwakilisha vyema kabisa!
 
Acha uongo wote tumepita LAW SCHOOL Matatizo ya LAW SCHOOL kubwa ni Wanafunzi
Lugha ni kikwazo kikubwa
Wanafunzi wanadhani ifaulu wa LAW SCHOOL unaamuliwa na Mwalimu mmoja kama Vyuoni
LAW SCHOOL hakuna RUSHWA ya Fedha wala ya NGONO
LAW SCHOOL wanasimamia TAALUMA.

Kwani wewe ni Malaika, Jini, Shetani au Mungu? Povu lote hilo kutokea kijiwe gani ndugu?
 
Kusoma msisome nyie kisha Yy abebe mzigo wenu? Hapana
 
Mtoa mada utakuwa ni mmoja au mnufaika wa waliofeli! Sasa waziri anahusika vipi na watu wazima kufeli kwasababu ya kutosoma?
 
Acha uongo wote tumepita LAW SCHOOL Matatizo ya LAW SCHOOL kubwa ni Wanafunzi
Lugha ni kikwazo kikubwa
Wanafunzi wanadhani ifaulu wa LAW SCHOOL unaamuliwa na Mwalimu mmoja kama Vyuoni
LAW SCHOOL hakuna RUSHWA ya Fedha wala ya NGONO
LAW SCHOOL wanasimamia TAALUMA.

Kwa usemavyo, Maana yake hapo kuna wasiosimamia taaluma mpaka tunapata wanafunzi vilaza wenye digrii za Sheria.

Bila shaka ni Wizara ya Elimu na TCU hao hawasimamii taaluma. Ni kama unasema kuwa Badala ya Ndumbaro, inabidi Waziri wa Elimu Prof. Adolph Mkenda ndio awajibishwe.

Vyovyote vile, unachomaanisha ni kuwa lazima kiongozi awajibishwe.
 
Mtoa mada utakuwa ni mmoja au mnufaika wa waliofeli! Sasa waziri anahusika vipi na watu wazima kufeli kwasababu ya kutosoma?

Mtoa mada ni mnufaika kwa maana hii:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Nikijipambanua wazi wazi kutoka kwa watanzania wajinga kama wewe:

"Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza."

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Umetuwakilisha vyema kabisa!

Hivi hamuoni aibu kutokukemea maovu kwa vile tu hayawahusu?

Kwamba mko kama mbuzi tu?

Bure kabisa!
 
Sasa hao wanao faulu wao wanasoma vipi?

Ingekua hakuna hata mmoja anayefaulu hapo sawa! Otherwise someni msitafute huruma.
Kufaulu ni jambo la kawaida na linalotegemewa (expected). Watu wanasoma ili kuondoa ujinga na pia kufaulu mitihani, hatuwezi kushangaa kwa nini watu wanafaulu wakati tunajua ndio lengo mojawapo la kusoma, tunashangaa na kuhoji pale watu wanapofeli.

Waziri hawezi kusifiwa kwa kuongoza chuo chenye ufanisi mdogo, tunamhoji kuwa kwa nini asiwajibishwe kwa kutumia fedha nyingi kuendesha chuo bila manufaa!!
 
Cha ajabu ni kuona wanashindwa kukariri wanayofundishwa Law School

Sidhani kama ipo namna sahihi ya kumtafsiri mtanzania mjinga zaidi ya hapa:

"Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza."

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Hawako wachache. Hao ndiyo unaowaona humu sasa.
 
Cha ajabu ni kuona wanashindwa kukariri wanayofundishwa Law School

Screenshot_20230428-091154.jpg
 
Back
Top Bottom