Waziri Ndumbaro awajibishwe kwa matokeo mabovu Law School

Sasa kama wanasoma vitu walivyo soma chuoni na bado wanafeli ina maana hata huko chuoni walikua wanakariri tu!!

Kwani mitihani yote hutolewa kwa nia njema? Kwani wewe umeishia grade gani mkuu?
 
Vijana uwakili siyo rahisi hivyo, unatoka chuo mwaka huu mwaka kesho kutwa uwe wakili, ndiyo maana mawakili wanadharaulika sasa kuliko zamani ilikuwa taaluma yenye heshima kubwa mno.
 
UKIHIYO WA WANAFUNZI WAZIRI AJIUZULU? KWELI WAJINGA WAPO WENGI NDIO MAANA MNATETEA WANAFUNZI
NAIPONGEZA LAW SCHOOL KWA KUSIMAMIA TAALUMA
 
Vijana uwakili siyo rahisi hivyo, unatoka chuo mwaka huu mwaka kesho kutwa uwe wakili, ndiyo maana mawakili wanadharaulika sasa kuliko zamani ilikuwa taaluma yenye heshima kubwa mno.

Kwamba uwakili ni rocket science siyo? Kumbe udaktari, uhandisi, na vya namma hiyo ni rahisi sana siyo ndugu?
 
Acha uongo wote tumepita LAW SCHOOL Matatizo ya LAW SCHOOL kubwa ni Wanafunzi
Lugha ni kikwazo kikubwa
Wanafunzi wanadhani ifaulu wa LAW SCHOOL unaamuliwa na Mwalimu mmoja kama Vyuoni
LAW SCHOOL hakuna RUSHWA ya Fedha wala ya NGONO
LAW SCHOOL wanasimamia TAALUMA.
 
UKIHIYO WA WANAFUNZI WAZIRI AJIUZULU? KWELI WAJINGA WAPO WENGI NDIO MAANA MNATETEA WANAFUNZI
NAIPONGEZA LAW SCHOOL KWA KUSIMAMIA TAALUMA

Mtanzania halisi wewe:

"Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza."

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Umetuwakilisha vyema kabisa!
 
Kwani wewe ni Malaika, Jini, Shetani au Mungu? Povu lote hilo kutokea kijiwe gani ndugu?
 
Kusoma msisome nyie kisha Yy abebe mzigo wenu? Hapana
 
Mtoa mada utakuwa ni mmoja au mnufaika wa waliofeli! Sasa waziri anahusika vipi na watu wazima kufeli kwasababu ya kutosoma?
 
Kwa usemavyo, Maana yake hapo kuna wasiosimamia taaluma mpaka tunapata wanafunzi vilaza wenye digrii za Sheria.

Bila shaka ni Wizara ya Elimu na TCU hao hawasimamii taaluma. Ni kama unasema kuwa Badala ya Ndumbaro, inabidi Waziri wa Elimu Prof. Adolph Mkenda ndio awajibishwe.

Vyovyote vile, unachomaanisha ni kuwa lazima kiongozi awajibishwe.
 
Mtoa mada utakuwa ni mmoja au mnufaika wa waliofeli! Sasa waziri anahusika vipi na watu wazima kufeli kwasababu ya kutosoma?

Mtoa mada ni mnufaika kwa maana hii:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Nikijipambanua wazi wazi kutoka kwa watanzania wajinga kama wewe:

"Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza."

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Umetuwakilisha vyema kabisa!

Hivi hamuoni aibu kutokukemea maovu kwa vile tu hayawahusu?

Kwamba mko kama mbuzi tu?

Bure kabisa!
 
Sasa hao wanao faulu wao wanasoma vipi?

Ingekua hakuna hata mmoja anayefaulu hapo sawa! Otherwise someni msitafute huruma.
Kufaulu ni jambo la kawaida na linalotegemewa (expected). Watu wanasoma ili kuondoa ujinga na pia kufaulu mitihani, hatuwezi kushangaa kwa nini watu wanafaulu wakati tunajua ndio lengo mojawapo la kusoma, tunashangaa na kuhoji pale watu wanapofeli.

Waziri hawezi kusifiwa kwa kuongoza chuo chenye ufanisi mdogo, tunamhoji kuwa kwa nini asiwajibishwe kwa kutumia fedha nyingi kuendesha chuo bila manufaa!!
 
Cha ajabu ni kuona wanashindwa kukariri wanayofundishwa Law School

Sidhani kama ipo namna sahihi ya kumtafsiri mtanzania mjinga zaidi ya hapa:

"Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza."

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Hawako wachache. Hao ndiyo unaowaona humu sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…