Waziri Ndumbaro awajibishwe kwa matokeo mabovu Law School

Mnaopiga mayowe wengi humu itakua mna supp au mmekuwa discontinued, LST ni habari nyingine ngumu lakini lazima profession iwe na njia yakugovern na kupunguza flow ya professionals mtaaani . Waendelee na utaratibu huo huo cz wakiachia mawakili wajae mtaani tayari itakuwa ni pigo kwa taaluma ndio maana hata sikuhizi unaskia kuna wakili au mtumishi wa mahakama anafanya double dealing. Waendelee kubana hata watoe watu kumi kwa mwaka ndio itakua poa ili na sisi tuiheshimu taaluma na tuheshimiane. Hapo uwaze umetoka kati ya hao wachache halafu mtu aje akuambie nifanyie notirization kwa alf tatu uone utakavyo mtimua, lakini wakiachiwa wakawa lukuki mtaani inakua ni changamoto tayari. Waziri asiwajibishwe bali aendelee na utendaji kazi wachuje mpaka tupate the best lawyers sio tu mauza uza wakili anafika mahakamani hawezi hata kujenga hoja.
 

Mawazo mufilisi kabisa. Wengine haki yako tu inatuhusu hata kama hatuna maslahi nayo ya moja kwa moja:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Lau post #2 au 3 uliziona?

Ila kwa utambulisho wako umejieleza vizuri sana ndugu. Wewe utakuwa mtanzania halisi:

"Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza."

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Umetuwakilisha vyema kabisa!
 
Waziri haimhusu hiyo anayetakiwa kuwajibishwa ni wahadhiri chuoni walikotokea hao wanafunzi. Wanasiasa mnashindana kupeleka watoto wenu kwenda kusomea sheria kama kitega uchumi cha kujipatia pesa kwa njia za kitapeli wakati hawana uwezo kiakili kuchambua mambo kisheria. Shule ya sheria ina darasa la kimahakama na kitengo cha uchunguzi makosa; ukiwasikiliza waendesha mashitaka, mahakimu na mawakili wanafunzi kwenye zoezi zima utasikitika sana kwamba kwanza walifikaje kudahiliwa kuingia kenye shule ya sheria wakati kwanza lugha ya kigeni ni mbovu na hawana uwezo wa kujenga hoja zenye mashiko.

Kwa muktadha huo ni ndoto kufaulu hata nusu ya darasa sembuse hao 23. Si kila mtu anayesomea sheria lazima awe wakili washauriwe wajiingize kwenye fani zingine wanazozimudu vizuri sio kukikimbilia kwamba nataka niwe kama Lissu, Kibatala, Jebra, Chenge au Mkono. Practice ya sheria ni 'serious and aggressive commitment which is not politically motivated with vengeance ambition's hapo utakwama tu kama ilivyotokea hata wakipewa nafasi zaidi ya mara tatu hawatoboi maana msingi wa elimu yao ni dhaifu kwa matumizi ya akili pevu.
 
Kumbe lengo lao ni kupunguza flow ya professionals mtaani.
Unafikiri wapo sahihi??
 

Hivi uliwahi iongelea lugha ya kigeni ya jiwe - PhD holder? Au yule waziri wa elimu - Prof? Au tuseme ndiyo umefika duniani leo?

Umeelewa waziri aliunda tume kutafuta ufumbuzi na akatumia pesa zetu?

Vipi tija ya tume hiyo ya waziri? Hivi hata ilichukua maoni ya wadau kweli au ilikuwa na yake tu? Post #2 na #3 ziliwasilishwa kwenye tume kama maoni. Kumbe tume ilizingatia maoni kutoka wapi? Au ilichukua maoni toka kwenu tu?

Waziri aliwataka wadau kuwa na subira kuwa anakuja na suluhu. Akawaomba majaji kuondoa tume yao iliyokuwa imepanga kufanya uchunguzi huru.

Bado wewe huoni kwa nini waziri anapaswa kuwajibishwa?

Kwa akili yako hudhani hata CAG labda angeachana tu na hizi audits zake kwani anaowaletea ni heri mbuzi?
 
Sasa huyu wakili mjinga akiingia mtaani si soko lenyewe tu litamtema mzee!! Atapata kesi siku ya kwanza, atashindwa kwa uzembe basi wateja watamhama na kuchagua mawakili bora

Ukisoma kanuni za LST zihusuzo mitihani na rufaa, na ukaulizia utekelezaji wa hizo kanuni hapo chuoni, huenda utabadili mtazamo wako na kuona kuwa wanafunzi hawana shida.
 
Mkubwa umeandika vizuri sana. Ambaye atashindwa kukuelewa ana lake jambo. Wahusika kama wapo serious wanapakuanzia kufanya reform just kwa ushauri wako huu. Ubarikiwe sana.
 
Naona umeandika vitu vingi visivyo na maana!

Hoja hapa ni moja, wanafunzi kufeli. Nikasema shida ya kufeli haipo kwa walimu au law school iko kwa wanafunzi wenyewe. Ningesema law school wana shida ikiwa hakuna mwanafunzi hata mmoja amefaulu.

Kama kuna wanao fauli ina maana mfumo wa law school unaeleweka na hauna shida.
 
Huku secondary ndo balaa! Mtoto wa kidato Cha pili anafundishwa 'functions of electral committee'!! Semeni wenyewe kama mtoto wa kidato cha pili anapaswa kufundishwa mambo haya.. kama mnashangaa ya TLS basi shangaeni na hili.
 
Mkubwa umeandika vizuri sana. Ambaye atashindwa kukuelewa ana lake jambo. Wahusika kama wapo serious wanapakuanzia kufanya reform just kwa ushauri wako huu. Ubarikiwe sana.

Kama ilivyo kwenye mada, hayo yote yaliwasilishwa tume ya Mwakyembe wakaona ni upuuzi mtupu.

Hawana nia njema bali ule ule uswahili wetu na akina Upepo wa Pesa tuliouzowea.
 
Tufanye umeongea jambo la maana. Umeongelea mfumo, sasa hebu soma kanuni za Rufaa uone huo mfumo ulivyo sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…