MBWARI
Member
- Sep 8, 2021
- 27
- 782
SHUGHULI za Royal Tour zilizokuwa zikifanywa kwa mara ya kwanza nchini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya Utalii, Biashara na Uwekezaji nchini zimeanza kuzaa matunda kwa wawekezaji kuanza kujitokeza kuwekeza hoteli za kisasa ndani ya hifadhi za Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema mara baada ya mkutano wake maalum na Wawekezaji uliofanyika Dar es Salaam mapema leo. Wawekezaji hao wanatoka Bara la Ulaya katika nchi ya Bulgaria na watajenga hotel za Nyota tano mithili ya Kempinski kwenye hifadhi Nne za Taifa nchini.
Waziri Dk. Damas Ndumbaro amesema mpango mkakati wa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kuandaa kipindi cha Royal Tour umeweza kuzaa matunda hayo na wao kama Wizara wameupokea na sasa ni utekelezaji.
''Juhudi kubwa za kimkakati za Royal Tour zilizoendeshwa na Rais wetu zimeweza kuzaa matunda ambapo leo tumepokea wawekezaji mahiri kutoka Bara la Ulaya ambao watawekeza kwenye hoteli kwa kujenga hoteli tatu za nyota tano za 'brand' ya Kempinski kwa uwekezaji wa Dola za Kimarekani Milioni 72.
''Mkutano wetu huu hii leo umekwenda vizuri sana na Wawekezaji hawa kwa hiyo unaweza kuipata hoteli ya Kempinski baada ya ujenzi huo kukamilika. .. Kempinski Serengeti, Kempinski Manyara, Kempinski Tarangile na Kempinski Ngorongoro." Amesem Dk. Ndumbaro.