Waziri Ndumbaro: Royal Tour ya Rais Samia yaanza kuzaa matunda kwa kuleta wawekezaji

Mtasema yote awamu hii,

Huu mwendo ni mpaka 2030 kwa maajaliwa ya Mwenyezi Mungu,

Mtateseka sana kama hamtakubali nguvu za Mungu zilizomzunguka Rais Samia,
Musiba wa awamu hii ya Samia

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
#MSIKILIZE WAZIRI WETU DK NDUMBARO
Viongozi wanatudharau sana WaTz. Wanatuona wajinga sana.

Filamu bado inaeditiwa, haijazinduliwa, haijaoneshwa kokote halafu eti imeleta mafanikio makubwa.
 
Wasemaji wa Serikali Kuna Jambo huwa hawasemi vizuri. Kuna kitu kinaitwa working in progress. Sasa unakuta maandalizi na mipango inaanzia regime moja na utekelezaji rasmi kufanywa wakati wa regime ingine Kisha credit anapewa aliyemalizia na sio aliyeandaa mpango wote.

Mfano mmoja Terminal three ya uwanja wa ndege uliasisiwa na JK lakini ukakamilika wakati wa Magufuli lakini credit anapewa Magufuli. Mifano ni mingi.

Hizo hotel feasibility study ilifanyika lini, athari za mazingira zimefanyika lini and Business proposal yao imefanyika lini ili kusema mama alipanga akashawishi na Sasa wanatekeleza.

Hivyo kila mtu apewe credit kwa alilofanya na sio cheap propaganda
 
Rais ameongeza thamani kwenye hii industry kwa kweli, lakini je, hao wawekezaji wamesema kuja kwao ni matokeo ya tour au walikua na mipango tayari?

Nauliza hivyo sababu ya muda uliopo tangu tour ifanyike na maamuzi ya hotels hizo kubwa kujengwa
 
Uwe unatumia na akili kudanganya

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Sio mtego.hotel ndani ya mbuga zilishakatazwa kipindi kirefu cha nyuma.labda kila zama na zake.wafanyakazi tu ngorongoro,manyara,tarangire wanaishi nje ya Park leo hii mwajenga Hotel ndani ya Park. Waziri aangalie fali za nyuma.wengi waliomba kujenga ndani ya Park walinyimwa ,leo policy zimebadilika.?.
 
Jamaa kadondosha radi bila kusikika ngurumo mitaani. Imebidi nicheke.

Hivi yule aliyezuia ndege alishalipwa????????
 
Umewahi kuona wapi uzinduzi ukazuia matumizi ya kitu?

Wewe unaumri wa miaka mingapi?

Matumizi ya Royal Tour Film ya Rais Samia hayazuiliwi na uzinduzi,

Uzinduzi unaweza ukafanyika katikati ya matumizi, It's OK also
 
Mkuu umeniwahi na hata mimi nashangaa, hivi hiyo filamu imetayarishwa muda gani na imerushwa hewani lini hadi ikaleta matokeo chanya, hata filamu za za akina Uwoya (takataka) zinachukua muda sembuse hizi za makala, ama semeni tu kuwa hizi filamu ni kama kutakatisha tu uhalali wa kujengwa hizo hoteli, na je mipango ya kujengwa hoteliza kitaliii imekuwa sawa na kujenga hivi vi lounge vyetu? ambavyo mtuunaweza kuamuka tuna kusema najenga ka lounge kangu mahala fulani, naona huu ni mpango wa kutakatisha yaliyopitishwa tayari kwa kutumia mgongo wa Royal Tour kama hizi habari ni za kweli
 
Ndugu zangu .

Royal Tour ni kipindi cha huko majuu na kina utaratibu wa kufanya tour katika mataifa mbalimbali mwaka 2018 walifanya Rwanda kwa Kagame .

Hapa kwetu tumefanya makala ambayo itarushwa katika kipindi cha Royal Tour Mwanzoni mwa Mwaka 2022 hivyo bado kipindi hakijarushwa mahali popote pale .

Sasa tija ya Royal Tour imekujaje ?
 
Vijana wa UVCCM muwe mnashirikisha akili zenu kabla ya kuanza mapambio yenu. Ili mtu apate kibali cha ujenzi wa hoteli kuna taratibumbalimbali huwa zinatakiwa kufuatwa hadi kupata kibali ikiwemo uchunguzi wa adhari za mazingira (Environmenta Impact Assessment) na mambo kibao. hata kama hayo mambo yatapelekwa kwa spidi ya kifisadi ya 5G hayawezi chukua muda mfupi hivyo kama unavotaka kuwaaminisha watu. Kwa taarifa yako hao wawekezaji walishaomba vibali toka enzi za kikwete lakini mwendazake alisababisha wawekezaji wengi kusita kuendelea na uwekezaji.
 
Umewahi kuona wapi uzinduzi ukazuia matumizi ya kitu?

Wewe unaumri wa miaka mingapi?

Matumizi ya Royal Tour Film ya Rais Samia hayazuiliwi na uzinduzi,

Uzinduzi unaweza ukafanyika katikati ya matumizi, It's OK also
Ukiondoa pazia la ushabiki utaelwa nini nasema, documentary hii imemalizika kufanyiwa shooting hata wiki tatu hazijaisha, sasa hivi ipo kwenye hatua ya uhariri...na kumbuka kuwa alikuwa akifanya documentary na kampuni kubwa ya kimataifa ambayo ndio hurusha hicho kipindi cha royal tour.. kama bado hawajazindua basi haijaanza kuruka hewani so bado haijaaza kuonekana hewani....Ni jambo zuri kuwa na uwekezaji huu lakini nakataa haujatokana na hii documentary ya Royal tour, Tuendelee kunywa mchuzi wa riyal tour nyama tutazikuta chini....kuhusu umri wangu ni kuwa kama nisingekuwa nimekorofishana na MAMA yako leo hii Ungekuwa unaniita BABA na ungekuwa unatumia Ubin wangu!
 
kwa kwel mm binafsi vitu vya kujegwa na wageni ndan ya haridhi yetu Tanzania naona uchungu sana. ndo maana hayati alikuwa ananifurahisha hapo jako kasoro zilikuwepo.
 
Kwanza mmemsikia jana alivyomwaga ile ngeli pale UN Gen Assembly ,

Huyu mama ni Mpango wa Mungu mwenyewe tuacheni amalize kazi ya Mungu aliyompa,

Sasa bilioni 158 haraka tu khaaa,

Yale makofi pale UN yalikuwa na maana kubwa sana,

Hongera Waziri
Hongera Rais
 
Mkuu tatizo mleta uzi ameuleta kishabiki mno bila hata kufanya tafakuri jadidi....anamuamini sana waziri ambaye ki ukweli amesema hayo kulinda tu tumbo lake na ugali wa familia yake....
 
Mkuu tatizo mleta uzi ameuleta kishabiki mno bila hata kufanya tafakuri jadidi....anamuamini sana waziri ambaye ki ukweli amesema hayo kulinda tu tumbo lake na ugali wa familia yake....
 
Umewahi kufika Mugumu Serengeti?

Hotel ziko nyingi tu pembeni ya hifadhi,

Hawajengi ndani ya hifadhi elewa,

Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu,
kwa kwel mm binafsi vitu vya kujegwa na wageni ndan ya haridhi yetu Tanzania naona uchungu sana. ndo maana hayati alikuwa ananifurahisha hapo jako kasoro zilikuwepo.
 
Mkuu tatizo mleta uzi ameuleta kishabiki mno bila hata kufanya tafakuri jadidi....anamuamini sana waziri ambaye ki ukweli amesema hayo kulinda tu tumbo lake na ugali wa familia yake....
Nchi hii wakubwa wanatuona wajinga wao ndio wanajiona pekee wenye akili. Hii ni aibu sana si kwa uongo huu.
 



NAO
NAONA MOD WAMEAMUA KUKATISHA HUU UZI WA KUMBRAND RAIS SAMIA,

JAMII FORUM ACHENI KUMUHUJUMU RAIS,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…