Waziri Ndumbaro: Wamasai waishio Ngorongoro siyo wenyeji halisi wa Ngorongoro

Waziri Ndumbaro: Wamasai waishio Ngorongoro siyo wenyeji halisi wa Ngorongoro

Bikis

Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
52
Reaction score
74
Wakati wa mahojiano na DW Waziri ndumbaro amekaririwa akisema Wamasai washio Ngorongoro siyo wenyeji halisi wa ngorongoro.

Imeibua mjadala mingi baada ya wananchi wasomi kutoka jamii ya kimasai kumwomba rais kutengua waziri wa mali ya asili kwa kauli yake kwamba Wamasai kwao ni sudan na siyo Ngorongoro.

Pia wananchi walitaka kujua kama hiyo ni kauli chama na serikali au ni kauli ya ndumbaro kama ndumbaro!!

Ni sahihi waasisi wetu, NYERERE, SOKOINE et.all walituachia taifa la Tanzania likiwa na makabila 120 na lugha yetu pendwa ya kiswahili ili kuweza kuwaleta watanzania wote bila kujali itikadi yao, dini yao, wala makabila yao na wote tunajitambulisha ni watanzania na siyo waamasi au Wachagga

Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa jamii ya kimasai kwamba wanaonewa serikali ya CCM kwasababu wao wanachukuliwa kama Wamasai na siyo watanzania!!

Baadhi ya wananchi wamemwomba mkuu wa nchi kumchukulia hatua mhusika huyo kwa kuvunja umoja wa watanzania uliopiganiwa na waasi wa taifa hili!!

Malalamiko hayo na mgogoro mkubwa huo unatokana na hatua ya wizara kuendelea na mchakato wa kuwaondoa wenyeji hao ili kupisha shughuli za uhifadhi na utalii!

Na wenyeji wameapa kwa aina ya uongozi wa wizara ya maliasili na utalii na baadhi wataalam kamwe mgogoro wa wananchi na uhifadhi hautaishia!!
 
Kila mwanadamu huzaliwa na kusudi.
Mungu uweka kusudi ndani ya mtu ili aweze kulitimiza katika siku zake za uhai.

Mungu pia humpa kila mtu utashi wa uchaguzi wa kutimiza kusudi alilopewa au kutokulitekeleza.

Magufuli alililiwa sana kwa sababu matendo yake yaligusa maisha ya watanzania wengi.

Alituonesha njia sahihi nasi tunaifata daima.
 
Inashangaza sana kuona ama kusikia Kiongozi mkubwa vile serikalini anatoa lugha ya kibaguzi namna hiyo. Kiongozi wa wizara nyeti kama ile anajitokeza hadharani na kusema hawa wana asili ya nchi fulani.

Kidogo imenistua maana sasa suala la Ngorongoro ni kama kutunishiana misuli sasa. Wananchi wale wanaonekana kama siyo watu sasa, hivyo imefika hatua watu wakubwa wakiwemo viongozi kama Ndumbaro kudiriki kutumia ushawishi wa hali na mali kuwaondoa.

Kusema kweli Wamasai popote wawapo hapa Tanzania wamekuwa wakionewa sana. Shughuli zao za kifugaji zimekuwa ni kama kero kwa serikali na hata ikitokea mgongano wa maslahi na watu wengine wanaowazunguka kama wakulima huwa mara nyingi inakula kwa upande wa Wamasai tu. Sijui kuna kitu gani lakini wanaonewa sana.

Juzi tu maeneo ya Kia nyumba na maboma ya Kimasai yamepigwa alama ya X kupisha utanuzi wa ule uwanja wa KIA. Serikali bila kujali wamekuwepo kwa miaka mingapi, imewapa muda wa kuondoka la sivyo nguvu itatumika kuwaondoa.

Mimi nashauri jamii hii kushikamana. Hii siyo vita ya Wamasai wa Ngorongoro peke yao, ni ya jamii nzima.

Natamani siku moja kusikia na kuona jamii hii ikishikamana na kupigania haki zao ambazo zinadidimizwa kila leo. Kwanini wasikichafue pale Ngorongoro kwa kushika ama kuteka magari mawili au hata matatu ya watalii ili dunia ijue kwamba hizi hela za Watalii ndo zinafanya haki za wale wamasai kupotezewa na kuonekana watu kuja tu wakati ni watu halali kwenye ardhi yao? Kama vipi wote wakose. No Wamasai in Ngorongoro, No Tourism, No NCAA.

Sitoshangaa Rais kukalia hii kauli ya Ndumbaro kimya. Ukimya wa kupigania haki husababisha kizazi kijacho kulaumu uzembe wa kizazi kinachopita. Hii itakuwa laana kubwa sana.

Amkeni!!
 
Wakati wa mahojiano na DW Waziri ndumbaro amekaririwa akisema Wamasai washio Ngorongoro siyo wenyeji halisi wa ngorongoro.
Hii ni kweli kwa upande mmoja na sii kweli kwa upande mwingine.

Ni kweli kwa sababu wakati NCAA inaanzishwa Ile 1959, Wamasai waliondolewa maeneo yao ya asili ya Serengeti na wakapelekwa Ngorongoro, hivyo ni kweli, Ngorongoro kuna baadhi ya Wamasai ni watu wakuja.

Sii kweli kwasababu ndani ya Ngorongoro kuna baadhi ya Wamasai ni wa asili pale.

Na ukweli wa mwisho, Tanzania ni eneo la asili la Bantustans, watu wa asili kabisa wa Tanzania ni Wagogo, Wasukuma na makabila machache ya asili ya Kibantu, Masai sio Bantu, ni Semi Nilotic, asili yao ni North Africa wame descend from Nubi, Walihamia East Africa kutokea Northern Sudan during early migration baada ya kutimuliwa na Wakushi.

Hata Waziri mwenyewe ni Mngoni, nao asili yao sio Tanzania, ni jamii ya Wazulu waliokimbia Mfecane wars , wakiongozwa na Zongendamba ndio wakaingia Tanzania na ku settle Songea. Makabila mengi ya mipakani wakiwemo Wachagga, ni wahamiaji tu.

Lakini Ile siku tunapata Uhuru, kuanza saa 6:01 ya usiku wa December ,9, 1961, kila mtu aliyekuwepo kwenye ardhi ya Tanganyika, alipewa uTanzania bure. Hivyo sio busara kuwabagua watu based on early migration.

P
 
Hii ni kweli kwa upande mmoja na sii kweli kwa upande mwingine.

Ni kweli kwa sababu wakati NCAA inaanzishwa Ila 1959, Wamasai waliondolewa Serengeti wakapelekwa Ngorongoro...
Wewe asili yako ni wapi ??

Maana you feel ok kujadili makabila ya wenzako.

Wafugaji wote sio wabantu.

Wasukuma pia.

Kwa hapa Tanzania natives pekee ni wagogo wengine wote ni wahamiaji.

Jiangalie mkuu.
 
Magufuli alililiwa sana kwa sababu matendo yake yaligusa maisha ya watanzania wengi.

Alituonesha njia sahihi nasi tunaifata daima.
Hali ya kumuabudu Magufuli kwa hawa wafuasi wake kama Nebuchadinezzer lazima tuukomeshe. Magufuli alivunja umoja wa kitaifa kwa vitendo vyake viovu. Alisema kabisa "siwezi kupeleka miradi ya maendeleo kwenye maeneo ambayo wananchi wamechagua upinzani"
 
Wamasai ndio wenyeji halisi wa Ngorongoro.
Kuna Mkataba unaodaiwa kusainiwa na waitwao Wazee wa Kimila na Mkoloni Mwingereza mwaka 1958 mbao umesemwa sana hapa JF uliowahamisha Wafugaji wa Kimasai kutoka Serengeti kuhamia Ngorongoro.

Kama huo Mkataba upo, basi ni dhahiri Wafugaji wa Kimasai siyo wenyeji wa Ngorongoro.

Ni Wahamiaji.
 
Na ukweli wa mwisho, Tanzania ni eneo la asili la Bantustans, Masai sio Bantu, ni Semi Nilotic, asili Yao ni North Africa, Walihamia East Africa during early migration.
P

tukianza kuchukua mtazamo huo hata huyo waziri mwenyewe asili yake ni Africa ya Kusini walikuja na kufika Tanzania kupitia mfecame .
Hata wewe mwenyewe utakuta kiasili sio mtanzania..
Hili suala la wamasai wa ngorongoro lichukuliwe kibusara sana na sio kimuhemko.
mimi kwa mtazamo wangu binadamu ni bora kulipo wanyama
utamlazimishaje binadamu aondoke eneo lake ili kumpisha mnyama just eti ili kuvutia utalii serikali itumie mbinu nyingine kupata hela
 
Wamasai ndio wenyeji halisi wa Ngorongoro.
Eneo la Ngorongoro kihistoria watu wa Kwanza kuishi hapo ni Wadatooga na Wairaqwi kwani ndio walikuwa wanafuatana na kuishi kindugu tokea Ethiopia... so walipokuja Wamasai kutokea huko Sudan kwa watu weusi nubian wakawafanyia fujo Wairawi na Wadatooga wakakimbia bila kupenda japo walionywa na Mtabiri wao waondoke wakabaki kupigana kama waukraine dhidi ya Urusi... so Masai waache ujinga kama wambulu walitoka hata wao watatoka tu
 
Back
Top Bottom