Thanks for this.
Hili pia nimelisema, the essence ya kauli ni kuwaandaa kisaikolojia Wamasai kuhamishwa Ngorongoro, kwa hoja kuwa, wale Wamasai 8,000 waliohanishwa kutoka Serengeti na kuhamishwa Ngorongoro, hapo Ngorongoro sio kwao, hivyo ikitokea need ya wao kuhamishwa, na need hiyo ikiwa justified, then, watahamishwa!. Kama mwanzo walikuwa Serengeti, ikatokea need wakahamishiwa Ngorongoro, na wakahamishika, na sasa imetokea tena need, then, watahamishwa pengine popote na watahamishika!.
Kumbe ni Wabaguzi, sikuwahi kulijua hili, then Sawa ya kuukomesha ubaguzi huu ni kuwahamishia maeneo ya Usukumani kwenye wale Wasukuma wa asili, huwa hawa approach, wanatwaa tuu, kesho yake wanapeleka ng'ombe kufidia, hivyo watawaoa mabinti zao, watake, wasitake, na huo ubaguzi wao utakoma. Kitu ambacho I'm not sure ni kama Wasukuma wataweza kuenjoy kufuatia mabinti wa Kimasai kufanyiwa Ile kitu!.
Pamoja Sana!.
p
Kitu ambacho hawataki wao kuona ni kwamba.
1.Wakihamishiwa maeneo mengine utamaduni wao utapotea.
2.Wanataka maeneo ya malisho ya mifugo (no restriction araea) wawe guru kulisha mifugo kokote popote sio wagombane na wakulima na hawataki maeneo yenye ukame.
Sasa kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi NGORONGORO imeharibika.
Kuhusu zile KAYA zenye idadi ya watu elfu 8 kutoka Serengeti hakuna rekodi kamili kwamba kwa sasa wamezaliana kiasi gani ,ila serikali inataka iwapeleke sehemu ambazo wao watachangamana na jamii nyingine za kitanzania,Mfano Meatu,Maswa,Karatu, Kilimanjaro, Handeni wataishi na watakua na maisha mazuri.
Kwa machache ndugu Pasko.
Idadi ya mifugo imeongezeka NGORONGORO leo mifugo ni 883,216
Uwezo wa kukaa mifugo ni 156,000.
Idadi ya watu 123,021
Uwezo wa kukaa watu ni 28,000.
Kwa wastan KAYA moja NGORONGORO inatakiwa iwe na ng'ombe wa maziwa 5 na Maksai 3 jumla 8 na kondoo 50 tu bila kuwa mbuzi.
Vichaka vilikua kwa ajili ya wanyama kama swala kukaa kivulini vilikuwa 300,000
Sa hizi vimebaki 48,000 ,means watu wamekata miti sana.
Ongezeko la makazi ya watu na malisho litaongezeka kwa 13% ifikapo 2030 kwa sababu idadi pia ya watu itaongezeka sana na yale maeneo ya malisho yamepungua.
Serikali pia iache ujenzi holela wa mahoteli kwa kigezo cha kupata mapato.
Makazi ya huduma za kijamii kama shule,zahanati na ofisi za umma zingekua kwa zones.