Hii ni kweli kwa upande mmoja na sii kweli kwa upande mwingine.
Ni kweli kwa sababu wakati NCAA inaanzishwa Ile 1959, Wamasai waliondolewa maeneo yao ya asili ya Serengeti na wakapelekwa Ngorongoro, hivyo ni kweli, Ngorongoro kuna baadhi ya Wamasai ni watu wakuja.
Sii kweli kwasababu ndani ya Ngorongoro kuna baadhi ya Wamasai ni wa asili pale.
Na ukweli wa mwisho, Tanzania ni eneo la asili la Bantustans, watu wa asili kabisa wa Tanzania ni Wagogo, Wasukuma na makabila machache ya asili ya Kibantu, Masai sio Bantu, ni Semi Nilotic, asili yao ni North Africa wame descend from Nubi, Walihamia East Africa kutokea Northern Sudan during early migration baada ya kutimuliwa na Wakushi.
Hata Waziri mwenyewe ni Mngoni, nao asili yao sio Tanzania, ni jamii ya Wazulu waliokimbia Mfecane wars , wakiongozwa na Zongendamba ndio wakaingia Tanzania na ku settle Songea. Makabila mengi ya mipakani wakiwemo Wachagga, ni wahamiaji tu.
Lakini Ile siku tunapata Uhuru, kuanza saa 6:01 ya usiku wa December ,9, 1961, kila mtu aliyekuwepo kwenye ardhi ya Tanganyika, alipewa uTanzania bure. Hivyo sio busara kuwabagua watu based on early migration.
P