Waziri Ndumbaro: Wamasai waishio Ngorongoro siyo wenyeji halisi wa Ngorongoro

Mkuu Pascal wewe ni mmoja wa wachangiaji ninaowaheshimu sana hapa JF.
Soma Bantu Expansion utakuta kwamba bantus asili yao ni South Cameroon. Na walitoka huko .
Tembelea Bujora kuna maandishi kwamba wasukuma walipitia Ethiopia kwenye hiyo migration.
 
Makabila ya asili kabisa Tanzania ni chache kwa mujibu wa historia, kauli kama za Ndumbaro na zingine zenye mrengo wa ukabila za kukemewa kwa nguvu zote, siyo njema kabisa kwa ustawi wa Taifa Letu pendwa.
 
Makabila yote ya TANZANIA hayana asili ya Moja kwa moja na nchi hii.
Ukisoma Historia unakuta wote walihamia kutoka kusini au kaskazini mwa nchi za kiafrika.
Kuna wajaluo wapo Sirari-Rorya nao sio wabantu je sio wenyeji wa eneo la Sirari.
Hapa tunazungumzia baada ya mkutano wa Berlin Conference kugawa mipaka na watu wake.
Wamasai kutokea Serengeti kwenda NGORONGORO haimaanishi sio wenyeji wa NGORONGORO au ndani ya nchi hii.
Ikumbukwe kuwa wakati wale wamasai elfu 8 wanahamishwa kule Serengeti kwenda NGORONGORO kuna baadhi waliokutwa wakiishi NGORONGORO.

Wamasai ni watanzania, kabila lao linawatambulisha hivo wao pia ni wabaguzi sababu wa ukabila sababu hawaruhusu mswahili kuoa bint wa kimasai . .ukiona mswahili kaoa mmasai ujue ni mmasai wa kiarusha sio yule ambaye anaishi NGORONGORO ndani.

Hata naunga mkono kuhamishwa
 
Thanks for this.
Wamasai kutokea Serengeti kwenda NGORONGORO haimaanishi sio wenyeji wa NGORONGORO au ndani ya nchi hii.
Ikumbukwe kuwa wakati wale wamasai elfu 8 wanahamishwa kule Serengeti kwenda NGORONGORO kuna baadhi waliokutwa wakiishi NGORONGORO.
Hili pia nimelisema, the essence ya kauli ni kuwaandaa kisaikolojia Wamasai kuhamishwa Ngorongoro, kwa hoja kuwa, wale Wamasai 8,000 waliohanishwa kutoka Serengeti na kuhamishwa Ngorongoro, hapo Ngorongoro sio kwao, hivyo ikitokea need ya wao kuhamishwa, na need hiyo ikiwa justified, then, watahamishwa!. Kama mwanzo walikuwa Serengeti, ikatokea need wakahamishiwa Ngorongoro, na wakahamishika, na sasa imetokea tena need, then, watahamishwa pengine popote na watahamishika!.
Wamasai ni watanzania, kabila lao linawatambulisha hivo wao pia ni wabaguzi sababu wa ukabila sababu hawaruhusu mswahili kuoa bint wa kimasai . .ukiona mswahili kaoa mmasai ujue ni mmasai wa kiarusha sio yule ambaye anaishi NGORONGORO ndani.
Kumbe ni Wabaguzi, sikuwahi kulijua hili, then Sawa ya kuukomesha ubaguzi huu ni kuwahamishia maeneo ya Usukumani kwenye wale Wasukuma wa asili, huwa hawa approach, wanatwaa tuu, kesho yake wanapeleka ng'ombe kufidia, hivyo watawaoa mabinti zao, watake, wasitake, na huo ubaguzi wao utakoma. Kitu ambacho I'm not sure ni kama Wasukuma wataweza kuenjoy kufuatia mabinti wa Kimasai kufanyiwa Ile kitu!.
Hata naunga mkono kuhamishwa
Pamoja Sana!.
p
 
Wangoni, wamasai, wachaga, waha, wahaya, wanyakyusa, wawanji, wamakonde na wamakua, wajaluo, wahangaza, na kadhalika hao ni watu wakuja Tanzania sio asili yao waangalie hata mfumo wa maisha yao
 
Yeye Ndumbaro kwao Africa Kusini na wala siyo Songea. Arudi kwao
 
crap
 
Basi warudishwe Serengeti kama Ngorongoro siyo kwao. Jamii hii ya wafugaji ndiyo ambao wametusaidia hadi leo tina hizo hifadhi za wanyama sasa kama zawadi yao ni mateso basi semeni. All we enjoy mpaka sasa ni kwasababu yao, get your facts right!
 
Basi warudishwe Serengeti kama Ngorongoro siyo kwao. Jamii hii ya wafugaji ndiyo ambao wametusaidia hadi leo tina hizo hifadhi za wanyama sasa kama zawadi yao ni mateso basi semeni. All we enjoy mpaka sasa ni kwasababu yao, get your facts right!
Hii ndiyo CCM halisi haina upendo na wananchi
 
Wakamatwe tu hawa watu
 
Kitu ambacho hawataki wao kuona ni kwamba.
1.Wakihamishiwa maeneo mengine utamaduni wao utapotea.
2.Wanataka maeneo ya malisho ya mifugo (no restriction araea) wawe guru kulisha mifugo kokote popote sio wagombane na wakulima na hawataki maeneo yenye ukame.
Sasa kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi NGORONGORO imeharibika.

Kuhusu zile KAYA zenye idadi ya watu elfu 8 kutoka Serengeti hakuna rekodi kamili kwamba kwa sasa wamezaliana kiasi gani ,ila serikali inataka iwapeleke sehemu ambazo wao watachangamana na jamii nyingine za kitanzania,Mfano Meatu,Maswa,Karatu, Kilimanjaro, Handeni wataishi na watakua na maisha mazuri.
Kwa machache ndugu Pasko.
Idadi ya mifugo imeongezeka NGORONGORO leo mifugo ni 883,216
Uwezo wa kukaa mifugo ni 156,000.

Idadi ya watu 123,021
Uwezo wa kukaa watu ni 28,000.

Kwa wastan KAYA moja NGORONGORO inatakiwa iwe na ng'ombe wa maziwa 5 na Maksai 3 jumla 8 na kondoo 50 tu bila kuwa mbuzi.

Vichaka vilikua kwa ajili ya wanyama kama swala kukaa kivulini vilikuwa 300,000
Sa hizi vimebaki 48,000 ,means watu wamekata miti sana.
Ongezeko la makazi ya watu na malisho litaongezeka kwa 13% ifikapo 2030 kwa sababu idadi pia ya watu itaongezeka sana na yale maeneo ya malisho yamepungua.
Serikali pia iache ujenzi holela wa mahoteli kwa kigezo cha kupata mapato.
Makazi ya huduma za kijamii kama shule,zahanati na ofisi za umma zingekua kwa zones.
 
Naafiki na wewe mkuu.
CCM ikiendelea na msimamo huu, wakuondoa wamasai na nguvu, basi isitoke hata kura moja ya kwao kwa hawa wadudumizi wa Jamii ya Muafrika/mmasai. Ni aibu katila karne kuendelea na ukoloni mamboleo.
Aluta Continua.
 
Ngorongoro ni yetu Wakurya ilimegwa toka kwetu Serengeti
 
Nilimsikia kwenye mahojiano kwa kweli sikutegemea kiongozi kujibu kijinga kiasi hicho...anasema ardhi ni mali ya rais!!!Wakati rais ni custodian na amepewa nguvu ya kuitunza na kusimamia in good cause..ardhi ni mali ya nchi na nchi ni watu...ndiyo maana kuna compensation.
 

 
Sikusikia mahojiano hayo, ila kama ni ya kweli, basi huyu mtu hafai kabisa kuwa kiongozi wa watanzania, anatakiwa afutwe kazi mara moja. Yaani yeye anatuona kwa ngozi ya makabila yetu badala ya kutona sote ni watanzania. Yeye Ndumbalo naye huenda suyo mtanzania kwani Wangoni nao asili yao siyo Songea bali ni kutoka wa kutoka Afrika ya Kusini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…