TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

Utawaweza wapambe na bosi wao Rostam Aziz, wamekataza kutaja jina la Zitto kwa habari yoyote nzuri.

si wamemsimamisha ,so hawawezi kumpa ujiko sababu itaonekana ni mtu wa kuwasaidia wananchi(mtazamo wa hawa walanguzi wa nchi yetu).Hivi rostam ana ubavu gani katika kutoa maamuzi?

mwanakiji naomba nakala sheria ya uraia ya mwaka 1995,Je RA ni Raia wa Tanzania?
 
[CENTER

am3gr2.jpg





Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog

Yaani ushabiki wa siasa mpaka MISIBANI?

watu wengine wana roho mbaya bwana duh!
 
mchawi alikuwapo pia,kazi kubwa
Mchawi nani tena?haya huyu kijana lawleance Masha?Mwizi wa RDC teh teh ..
sikujua..anahusika na kumroga nani?
Dr. Mbatia anonesha kushikwa na simanzai kubwa,mpaka inatia huruma..
Poleni sana wote waliopata ajali.mbona kuna viongozi kibao wa CCM huko Iringa kulikuwa na nini?
 
Thanks: Mtu wa Pwani, Mtoto wa mkulima, hume and all, tuendelee kuwahabarisha mamillioni ya Watanzania kwa habari zinapotokea na ushirikiano wa kila moja ni muhimu.

Special thanks to Mjengwa.
 
mchawi alikuwapo pia,kazi kubwa

hahahahaha enewei watani hata ktk misiba wappo na tumezoea mambo haya tanzania. Lakini huyo mlozi alifata nini huko maana inaleta shaka sasa

na sali la logic limeulizwa kuwa kwa muda mfupi huu hawa viongozi wengi wa juu wa ccm walifata nini huko?? iko namna
 
Unachosema ni moja ya sababu za kuongezeka kwa ajali nchini. Nina imani kuwa umeshasafiri sana kwenye nchi hii na unajua miundo mbinu yetu ilivyo. Barabara ni za hatari sana. Siamini pia kuwa wote wanaopata ajali kwenye barabara zetu hawana leseni za halali ama hawana ujuzi mkubwa wa matumizi ya barabara na vyombo wanavyotumia.

AmaniK,

Hamna mahali popote nilipoandika wanaopata ajali ni wenye leseni zisizo halali. Ajali huwa zinatokea shauri ya mambo mengi na pia
hata uwe dereva mzuri kiasi gani na makini kiasi gani bado kama kuna madereva wachache ambao ni bomu, ajali itawakumba hata hawa madereva wazuri.

Kwa safari zangu za TZ sioni kama barabara ndio tatizo. Hata ujenge barabara zenye lane 10 bado kama kuna madereva wasio faa, ajali zitatokea tu.

Mimi Tanzania huwa siendeshi gari kwasababu nitafuata kila sheria na matokeo yake ni kuishia kugongwa. Badala yake natafuta kijana wa kuniendesha. Inabidi kugombana naye sana mpaka akubali kufuata sheria.

Huku Ulaya naendesha sana na kazi yangu ina mizunguko mingi mpaka kila pembe ya nchi. Hata hapa UK kuna barabara nyingi tu ndogo kama hizo za kwetu na tena zina magari mengi kuliko ya TZ lakini hakuna ajali nyingi kama TZ.

Huku sasa kila sehemu yenye hatari utakuta kamera, sasa kama wewe mjanja basi kimbia, safari moja points zote 12 zimeisha na sahau tena kuendesha gari. Kwasisi ambao kazi zetu lazima uwe unaendesha basi hapo na kazi umeshapoteza.
 
hii thread isihusishwe na siasa jamani, kuweni na nidhamu hata pale mtakapoona ni vigumu kuwa nayo ! Jitahidini kadri mtakavyoweza maneno yenu ya siasa kuhusisha na hiki kifo jamani yaishie kwenye vinywa vyenu jamani !
 
Hivi huyo jamaa aliyevaa kofia ya SI-SI-EM hakufikiria mara mbili? Why would he wear this hat? I don't support CCM policies but as a Tanzanian nimehuzunishwa sana na kifo cha Mh. Mbatia.
In a tragedy like this, we are suppose to put aside our political differences and come together as one. Huu ukereketwa sasa is too much. Does this mean kwamba the CCM folks ndio wameumia zaidi na huu msiba than us non CCM's? Huyu mama alikuwa akifanya kazi kwa umma wa wa Tanzania na sio kwa wachache wa kijani na njano. Tujifunze, and lets hope we do better next time.
Mwisho napenda kutoa salam zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, na marafiki wa marehemu Mama Mbatia.
 
Thanks Guys kutuletea picha hapa. It helps hasa kwa tulio ughaibuni. Thanks
 
Mchawi ni serikali amabyo imetoa ahadi mlima za kuleta maendeleo lakini Mhhhh!! Pamoja na kuwa mie polisi wa barabara lakini chanzo cha ajali Tanzania 90% ni barabara zisizostahili. nyembamba na zina mashimo kila pahala.
 
lakini magazeti mengine si yametaja? tatizo liko wapi?


nilidhani watetezi wa fani ya uandishi wa habari mngekuwa na kiwango kile kile.. magazeti ya serikali yanapoamua kuminya habari haisaidii kitu.. hivi kweli unaamini kuwa "jina halikuthibitishwa"? Mnapotaka sisi wengine tuwe wa kweli na tusifanye makosa tumieni kipimo hicho hicho kwa vyombo vya magazeti ya serikali. Sasa kutotaja jina la Zitto kunawasaidia vipi serikali? Yaani, hadi kwenye misiba watu bado wanataka kumfungia Zitto, huo ni uhuni!!

Hata magazeti yote duniani yakitaja lakini inapotokea magazeti ya serikali yasipotaja inakuwa ni uhuni!! wamechemsha big time!!
 
hii thread isihusishwe na siasa jamani, kuweni na nidhamu hata pale mtakapoona ni vigumu kuwa nayo ! Jitahidini kadri mtakavyoweza maneno yenu ya siasa kuhusisha na hiki kifo jamani yaishie kwenye vinywa vyenu jamani !

isihusishwe na siasa vipi, wakati aliyekufa ni mwanasiasa na ambaye ameogopwa kutajwa ni mwana siasa, unataka tuiweke kwenye "udaku"?
 
AmaniK,

Hamna mahali popote nilipoandika wanaopata ajali ni wenye leseni zisizo halali. Ajali huwa zinatokea shauri ya mambo mengi na pia
hata uwe dereva mzuri kiasi gani na makini kiasi gani bado kama kuna madereva wachache ambao ni bomu, ajali itawakumba hata hawa madereva wazuri.

Kwa safari zangu za TZ sioni kama barabara ndio tatizo. Hata ujenge barabara zenye lane 10 bado kama kuna madereva wasio faa, ajali zitatokea tu.

Mimi Tanzania huwa siendeshi gari kwasababu nitafuata kila sheria na matokeo yake ni kuishia kugongwa. Badala yake natafuta kijana wa kuniendesha. Inabidi kugombana naye sana mpaka akubali kufuata sheria.

Huku Ulaya naendesha sana na kazi yangu ina mizunguko mingi mpaka kila pembe ya nchi. Hata hapa UK kuna barabara nyingi tu ndogo kama hizo za kwetu na tena zina magari mengi kuliko ya TZ lakini hakuna ajali nyingi kama TZ.

Huku sasa kila sehemu yenye hatari utakuta kamera, sasa kama wewe mjanja basi kimbia, safari moja points zote 12 zimeisha na sahau tena kuendesha gari. Kwasisi ambao kazi zetu lazima uwe unaendesha basi hapo na kazi umeshapoteza.

Mtanzania unachosema ni kweli ila pia kuna ukweli kwenye argument hiyo nyingine kuwa ubovu wa barabara sio tu unachangia kwenye ajali Tanzania bali pia unakwamisha shughuli nyingi sana za kuinua uchumi kitu ambacho kinapelekea watu kuwa masikini na wengine kufa kwa njaa au kufa kwa kukosa usafiri mzuri na wa haraka wa kuwapeleka hospitalini.
 
..hata mimi nadhani hayo magwanda ya CCM hayaleti picha nzuri ktk misiba.
 
AJALI YA MH.MBATIA SUMAYE,ZITTO CHUPUCHUPU

2007-10-25 16:23:06
Na Emmanuel Lengwa, Jijini


Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa Fredric Sumaye, Mbunge Machachari wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. David Mathayo ni miongoni mwa watu walioponea chupuchupu kupatwa na ajali iliyotokea jana jioni na kusababisha kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Marehemu Salome Joseph Mbatia.

Bw. Sumaye, Zitto na Mathayo walikuwa kwenye magari tofauti wakiongozana katika barabara moja na gari la Mhe. Mbatia lililopata ajali, bila wao kufahamiana.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo wanasema lori aina ya Fuso liligongana uso kwa uso na gari la Mhe. Mbatia, ndilo lililopoteza mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.

Kwa vile magari yaliyokuwa yamewabeba waheshimiwa hao yalikuwa yakiongozana, basi kama lori hilo lisingegonga gari la Mheshimiwa Mbatia huwenda lingeyavaa magari ya waheshimiwa wengine.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya Simu leo asubuhi, Mheshiwa Zitto amesema gari lililokuwa limembeba marehemu Salome Mbatia lilikuwa mbele yake wakiongozana barabarani, lakini hakujua kuwa aliyekuwamo alikuwa ni Naibu Waziri Salome Mbatia.

`Gari hilo lilikuwa mbele yangu, nililiona lakini kwa vile marehemu alitumia gai binafsi, sikujua kuwa aliyekuwemo alikuwa ni Mhe. Mbatia,` akasema Zitto.

Akasema Mheshimiwa Zitto kuwa yeye alifika ndani ya muda wa dakika tano baada ya gari la Mheshimiwa Mbatia kupata ajali, lakini kwa jinsi gari hilo lilivyokuwa limepata ajali hakuwe .

Zitto amesema muda mfupi baadaye wakati wakiendelea kuwatoa majeruhi kwenye magari,likafika gari lingine alilokuwemo Bw. Mathayo, ambaye alimtambua moja kwa moja Naibu Waziri Salome Mbatia, kwa vile alikuwa na taarifa za safari yake hiyo na alilijua gari hilo lililopata ajali.

`Mheshimiwa Mathayo ndiye aliyemtambua Marehemu Mbatia,` akasema.

Kwa mujibu wa Bw. Zitto wakati wakiendelea kuiondoa miili ya marehemu kwenye magari, pia likafika gari lingine alilokuwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredrick Sumaye ambaye pia aliungana nao katika kusaidia kuitoa miili ya marehemu kwenye magari ambayo yalikuwa yamepondeka vibaya.

Bw. Zitto akasema baada ya kuona ajali hiyo akaamua kukatiza safari yake na gari lake likatumika kuwakimbiza majeruhi wengine hospitalini.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Advocate Nyombi amesema dereva wa gari aina ya Fuso liligongana na Gari la Naibu Waziri huyo na kusababisha kifo chake amenusurika.

Kamanda Nyombi ameiambia Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi kuwa aliyekufa papo hapo katika ajali hiyo ni Utingo wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Castory Kilagwa, 22, ambaye ni ndugu wa mmiliki wa Fuso hilo.

Amesema hata hivyo Dereva huyo inadaiwa kuwa alikimbia au aliondolewa haraka eneo la tukio, na hivyo hajulika alipo na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.

Kamanda Nyombi amesema Polisi imemkamata mmiliki wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Jackson Kilagwa ili awaaidie kumpata dereva wake.

`Tunaamini hawezi kumkabidhi mtu mali yake ya thamani kiasi kile bila kujua mahali anapoishi, ndio sababu tunamshikilia mmiliki wa gari hilo ili atusaidie kumpata dereva wake,` akasema Kamanda Nyombi.

Akizungumzia taratibu za usafirishaji wa mwili wa Marehemu Naibu Waziri Salome Mbatia, Kamanda Nyombi amesema anachosubiri ni maelekezo kutoka ngazi za juu.

Akasema taarifa aliyopewa awali ni kuwa ndege ya Serikali ingewasiri Njombe leo saa 3:00 asubuhi kuuchukua mwili huo, lakini mpaka wakati akiwasiliana na gazeti hili ilikuwa bado haijafika.

`Nimeambiwa ndege ingefika saa 300 asubuhi, lakini mpaka sasa sijaiona na hivyo nasubiri taarifa nyingine kutoka ngazi za juu,` akasema Kamanda Nyombi.

SOURCE: Alasiri
 
Back
Top Bottom