Waziri Selemani Jafo ashauri kuanzishwa kwa wiki ya nyungu katika kupambana na Corona

Waziri Selemani Jafo ashauri kuanzishwa kwa wiki ya nyungu katika kupambana na Corona


Katika harakati za kupambana na janga la virusi vya corona, Waziri Selemani Jafo amependekeza kuanzishwa kwa wiki ya nyungu kitaifa. Wiki hiyo itatimiza upigaji wa nyungu asubuhi, mchana ma usiku. Amewaasa Watanzania kutokebehi upigaji wa nyungu kwa kuuita kama uganga wa kienyeji na kusisitiza ulaji wa vyakula asili kama mapapi, ubuyu na kisamvu ambavyo vinaweza kuimarisha kinga ya mwili.

Fahamu zaidi kuhusu nyungu na faida zake
Majani ya Mvuje kiboko ya wachawi na majini, mfunge mwanao - JamiiForums
 
Katika harakati za kupambana na janga la virusi vya corona, Waziri Selemani Jafo amependekeza kuanzishwa kwa wiki ya nyungu kitaifa. Wiki hiyo itatimiza upigaji wa nyungu asubuhi, mchana ma usiku. Amewaasa watanzania kuto kebehi upigaji wa nyungu kwa kuuita kama uganga wa kienyeji na kusisitiza ulaji wa vyakula asili kama mapapi,ubuyu na kisamvu ambavyo vinaweza kuimarisha kinga ya mwili.

Tangia nipate kuambiwa na Mtu kuwa Mhusika ni Mshirikina aliyeshindikana wala sijashtushwa na Ujuha wake alioushauri hapa.
 
Hivi hawa ndio walitaka madereva wao, wawe na vyeti kidato cha nne ili hali wao kiuwezo wa akili, hawawafikii hao madereva wa darasa la Saba!!.
Haya yalikuwa matumizi Malaya sana ya akili.

Kigezo ni kujua kusoma na kuandika.
 
Yupo sahii. Kma kuna mtu anabisha atoe njia zake lakini sio za kuiga kwa wenzake! Usitoe ushauri kwa jambo lisilowezekana! Asante jafo
 
Waziri anawaza na kupromote vyungu wakati wenzetu wapo busy kutafuta mbinu za kisayansi za kupunguza maambukizi: limit mizunguko/spreading, test as much as possible and isolate/treat those who tested positive. Mawaziri wetu hawana clue jinsi ya kudeal na hii kitu. Hatari kubwa sana
 
Nasema na nassisitiza kauli yangu nchi kama nchi imeshakwama...
Kama hawa(akili hizi) ndizo tunazotegemea zituvushe kwenye janga hili.
Tumekwisha
 
Mwisho watasema tuchome moto miji yote ili tuanze upya
Lakini ukishangaa ya kwetu angalia ya Spain ambapo wameamua kumwaga bleach kwenye fukwe za bahari na imeleta taharuki na hasira kwa wananchi
Mpaka Corona inaisha tutasikia mengi
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom