Waziri Simbachawene amwagiza IGP kuwapangia kazi nyingine matrafiki wenye vitambi. Je, ni kosa askari kuwa na kitambi?

Waziri Simbachawene amwagiza IGP kuwapangia kazi nyingine matrafiki wenye vitambi. Je, ni kosa askari kuwa na kitambi?

Sipati picha huko aliko kama presha haijapanda

IMG-20200523-WA0015.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awaache tu maana hata walinzi wa mzee baba siku hizi wana vitambi vya hatari kwa hio ni mabadiliko tu,ukishashika pesa mwili una umuka wenyewe tu.
 
Kuna watu maisha yanabadilika kwa kuingiza hela kwa njia tofauti kwa hiyo hata matumizi yake yanakuwa ya hovyo

Mtu alizoea kula ugali halafu anaanza kupata za kubrashi hapo chips kuku ni kila siku na bia kwa sana lazima utumbo uzidi kutanuka.

Na hao atakaowapeleka wasio na vitambi baada ya miezi kadhaa nao watakuwa hivyo hivyo
Sasa itakuwa kubadili kila wakati?


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Amri ya ajabu! Sijui ujinga huu wanautoa wapi?
Huwa nakuelewa sana "Retired". Ila nimeshangaa kuona unapinga hili. Kuna watumishi wakiwa na vitambi hatuwezi kuhoji wala kushangaa. Lakini kwa Askari kuwa na Kitambi haipendezi hata kidogo na ni ishara ya mtu mvivu na Mzembe. Askari anatakiwa kuwa Mwepesi.
 
kitambi ni utapiamlo
napendekeza wapewe elimu ya ulaji wa chakula
 
Hilo ni agizo ,linalohitaji kutafsiriwa kwa matendo katika kulitimiza.

Wapo kweli Askari wa aina hiyo katika kila ofisi wakiwa na vitambi huku utendaji wao ukiwa duni kutokana na tumbo kubwa.

Japo wapo wengine wanakitambi lkn wapo vzr kikazi. Hivyo baada ya agizo kinachofuata ni kutambua tambi zembe na tambi ngangari.

Vinginevyo agizo hili likichukuliwa jinsi lilivyo bila kutafakari kwa kina , litakuwa na uonevu maana wengine ni miili ya ugali toka kwa mama zao.

Sijui hao wa GAIRO.
Kuna ukweli fulani hapa!!
 
Kitambi Ni dalili ya uzembe na kutojiweka katika hali ya "utimamu wa mwili" ikiwa askari ana kitambi basi huyo Ni mzembe na haijalishi Ni mwepesi au vipi, mazoezi mhimu.

Kwa kawaida askari (kwa JWTz) uzito mzuri ni kuanzia kilo 65- 75 ikiwa Ni mrefu zaidi. Hawa wanaofuga mavitambi ya kijinga ni wazembe na walafi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom