“Lipo jambo moja lilisemwa na Mpina, ni jambo nzito na ukilichukulia kwa wepesiwepesi unaona amezungumza kitu chepesi lakini mpina amezungumza kitu kizito” na ni lazima tukijibu kama Serikali.
Waziri Simbachawene ametaja tuhuma za Luhaga Mpina kama ifuatavyo
- Mpina anasema Ilani na Utekelezaji wa Serikali haviendani.
- Mpina anasema kuna uvunjaji mkubwa wa Sheria bila hatua kuchukuliwa, yaani utawala ambao hauna sheria, No enforcement.
- Mpina anasema Watanzania wanauawa.
- Kuna wizi wa kutisha.
- No Separation of Powers.
- Teuzi za ajira bila ushindani.
- Kuna ufisadi wa kutisha na akitolea mfano wa miradi ya SGR, JNHHP.
- Deni la taifa halieleweki.
- Viongozi hawaheshimia.
View attachment 2969225
Haiwezekani ukaacha kujibu kwasababi yeye ameshaipeleka kwenye Mitandao. ni nchi gani hiyo ambayo ina sifa kama hizi ikbaki stable kama ilivyo nchi yetu? nchi hiyo inaitwa Tanzania ambayo Demokrasia chini ya Uongozi wa Rais Samia iko kwenye viwango kuliko wakati mwingine wowote. Simbachawene ameongeza kuwa vyombo vya habari viko huru, vyama vya siasa viko huru vinafanya kikutano vinavyotaka na kuandamana vinavyotaka, halafu wewe unasema nchi hii imevurugugika.
Anachojaribu kusema Mpina hapa ni kuwa nchi hii kuna a failed State, anataka kusema kuna a weak state, sasa a weak state ina sifa zake. Sasa moja ya sifa ya a weak state ni kuwa mipaka yake haidhibitiki. Sasa katika ukanda huu kuna nchi ambayo mipaka yake inadhibitika kama Tanzania? Nchi haichezewi.
Tusijidharau kiasi hicho, ni dhambi kujidharau, na kama mtu una mambo yako ni vyema ukayazungumza kwa namna nyingine lakini si kwa mambo ya kitaalam kama haya.
Nchi yetu inaheshimika, Rais wetu anaheshimika na ndiyo maana kila anapokwena duniani wanampa shahada ya udaktari, ni heshima wanampa zawadi zote za kubeba wanaona hazifai ndiyo maana wanaamua kumpa za kichwani.
This global appreciation to a woman president haiwezekani ikadharauliwa na sisi wenyewe ndani ya nchi, ni lazima tujenge tabia ya kujiamini, kuheshimiana. Huwezi ukaizungumzia a failed state halafu ukasema unamheshimu Rais anayeiongoza hiyo nchi, hii ni insubordination.
Nchi yetu katika changamoto kubwa duniani, COVID -19 imepiga dunia nzima, nchi inatekeleza miradi mikubwa sana. Kule Meatu kwa Mbunge Luhaga Mpina Serikali imepeleka maendeleo lukuki halafu anasema this is a failed state, hapa nadhani kuna ajenda.
Pia soma