Waziri Simbachawene: Huenda Mpina ana ajenda. Uongozi wa Rais Samia uko kwenye viwango kuliko wakati mwingine wowote

Ccm washenzi Sana wenyewe ikikaribia Uchaguzi wanajifanya kugombana wanatupumbaza mwisho wa siku vyeo wanapeana hao hao wanateuana na Vizazi Vyao huku wakiendelea kuiba vya kutosha huko nyuma ya pazia,,kula Kuku na wakipeana chiazii na Whiskey za bei mbaya wakifurahia Kodi za Wanyonge
 
Waanze basi kufanya uchunguzi wa kifo cha mwendazake
Hakuna haja ya uchunguzi wa kifo cha jiwe. Jiwe alikufa kizembe kwa kutoheshimu masharti ya korona, badala ya kupiga chanjo yeye akawa anajifukiza. Matokeo yake korona ikamuua. Moyo ni kichaka tu cha kuficha aibu ya kifo cha kizembe.
 
Kbs
 
Kweli kabisa
 
Hawa waparuane wafukuzane... Kidumu cha hiyo cartel kipasuke ndo pona pona ya waTanzania ilipo!
 
huo udaktari kauokota wap ? hana fumbuz wala jambo kalifanya kiubora zaid ya watanguliz , zaid anashindwa kusimamia mali za nchi badala yake anazigawa kwa wageni kwa mikataba mibovu kbs
Ana PhD ya uzurulaji
 
Mtoa shutuma huwa anaitwa anakaa na vyombo vya usalama anatoa data za yale anayoyashutumu, kisha serikali inafanya analysis ya kila kilichosemwa na kukifanyia kazi, bila kujali ni kidogo kiasi gani.

Wao wanamjibu ki siasa, ki-team. Team Samia na Team Magufuli ziko vitani. Huyu Luhaga Mpina kesha itwa na kamati ya maadili ya ccm mkoa, kamati ya maadili ya bunge la ccm, na kote huko alipeleka ushahidi ya aliyoyasema na akaachwa huru. Inaonyesha huwa hakurupuki huwa ana data za kutosha kwa kila anachokisema.

Wayafanyie kazi waache blabla.
 
Mpina mimi namchukulia kuwa ni mtu mwenye roho ya kichawi.

Ni mtu ambae ameumizwa sana kuukosa uwaziri.
 
CCM inaelekea kwenye shimo la umauti.......kiwango chao ushenzi, ubaya, ufirauni, na uovu dhidi ya watanzania kimefikia hatua mbaya mpaka wameanza kuparuana wenyewe kwa wenyewe.........

Naweza kusema Mungu ameamua kusimama na wanyonge........ngoja vita vilipuke kuanzia ndani ili tuone milipuko mikubwa zaidi......
 
Kinachonisikitisha ni kuwa Mpina hana maisha marefu ya kisiasa na pengine hata ya kimwili na roho........

Huu ukimya wa CCM na namna wanavyojibu tuhuma zake ni wazi kuwa Wana buy time dhidi yake..... lakini mioyoni mwao wamedhamiria ubaya..........

Sote tunawajua CCM linapokuja suala la madaraka na utawala roho zao zinakuwaje.......

Mungu aepushe mbali
 
Mpina mimi namchukulia kuwa ni mtu mwenye roho ya kichawi.

Ni mtu ambae ameumizwa sana kuukosa uwaziri.
Unataka kusema angekuwa waziri asingesema anayosema? Je anayosema ni ya uongo?Uwaziri ni miwani ya mbao au ni ear-plug?

Kesha itwa na kamati za maadili kuhojiwa na kuombwa ushahidi wa anayoyasema na alipeleka ushahidi na akaachwa huru, sio mgeni kwao, wanamfahamu kwamba sio mropokaji, ana kusanya data za yote anayoyasema kisha naongea, anafahamu ccm ni nini na watafanya nini hivyo uwa anajiandaa.

Sioni kwanini mtu kuusema ukweli aonekane ni mchawi, au ndio kusema "Sisi ukweli kwetu mwiko".
 
Waziri amejibu kwa porojo namna hiyo? Au hizo porojo ni zako wewe mleta mada?
Ameanza vizuri mno ila ghafla amediverge kuelekea kwenye pambizo 😁😁😁! Hii nchi inahitaji nuclear missile kwenye mihimili miwili ambayo sitaitaja sababu mwanasheria wangu hajamaliza mitihani ya school of law. Tukianza upya kama taifa huenda tukaenda vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…