mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Kweli kabisaJukumu la kwanza la usalama ni wewe Abiria unatakiwa kulichukua .
Kuna wakati nilisafiri kutoka dodoma kuja Dar abiria mwema akapiga simu polisi chalinze kuwa dereva anaendesha Mwendo kasi pasipo tahadhari polisi wakasimamisha basi likaenda kituoni , abiria wote walimtetea dreva yule abiria akaonekana hana hoja basi likaruhusiwa.
Mimi mwenye nilimuamuru dereva aendeshe basi kwa tahadhari tukitokea Mwanza kuja Dar nikidai haki yangu ya kuendeshwa kwa kufuata sheria za barabarani baada ya dereva kutaka kutuangusha Ilibidi basi lisimame abiria wakamtetea dereva.
Na hilo kila siku wanaambiwa,abiria ukiona dereva ana kimbiza mwendo wa kasi mseme
Ova