Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Ulega ameyasema hayo tarehe, 1 Oktoba, 2026 Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuwasili na kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo Mhe. Dkt. Juma Homera kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 27 Septemba, 2026.
“Mimi niko tayari kujifunza mambo mbalimbali kuhusu wizara hii na sekta ya Sheria kwa ujumla lakini pia kushirikiana na watumishi na viongozi ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa weledi na ubora na hatimaye kufikia malengo yaliyowekwa” alisema Ulega.
Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 1 Oktoba, 2026 katika ofisi za wizara Mtumba Jijini Dodoma, na kushuhudiwa na viongozi wengine wa wizara akiwemo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba, Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Baraka Luvanda pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo vya wizara.