Waziri Ulega akipiga mkwara na Kingereza cha ugoko

Binafsi naona kaongea vizuri, labda na mimi ndio walewale.

Tutofautishe grammatical errors na accent, grammar yake haikuwa mbaya, tena yupo vizuri kuliko wengi wetu. Accent yake ni ya kiafrika, au tunataka aongee kama muingereza?
 
Nimemsikiliza kwa makini waziri akiongea sijaona grammatical errors au mmemaanisha lafudhi yake sio nzuri mlitaka arembe kama wanavyoongea wagombea umiss Tanzania?
Au kwa vile alikuwa anaongea kwa slow speed ndio mnasema hajui ilhali yeye ameongea polepole ili wachina wamuelewe kwa urahisi maana wachina pia kiingereza sio lugha yao.
Halafu ni kwa nini mnahusianisha kuongea kiingereza na uwezo wa akili ina maana mnataka kusema huko ilikotoka hii lugha watu wote wana akili?hakuna vilaza,hakuna vichaa?
 
Ulega ametiza wajibu wake na English yake sio mbaya kabisa. It's normal sisi waswahili kaongea kwa utulivu na lugha rahisi kwa wachina
 
Nilichogundua kinge changu kimemzidi ulega kidoogo
Lakini ulega yuko perfect hii ni Swahili republic
Kushindwa kuongea lugha za watu kwa ufasaha si ushamba wala kujua si ujanja
Hii ipo Tanzania tu
 
Ahhahaja kingereza cha watanzania wengi above 40yrs leo ndio hicho hicho....amini usiamini ...labda kizazi kileeee hapo sawa kwa sasa wote sawa tuuu
 
Mbona anaeleweka,kikubwa wamemuelewa.Shule zenyewe tunafundishwa na walimu ambao nao hawajui kiingereza, utawezaje kuongea kingereza kilichonyooka,hata hivyo mwamba kajitahidi,maana naona hapo mpaka kijasho chembamba kinamtoka...
 
Wengi wetu tunaotea kiingereza cha kuandika.
 
Hapo sio chuo kikuu katika kitengo cha lugha hapo ni kazini na huyo mchina amemuelewa vizuri sana.

Narudia tena tunao ushamba wa kudhani kujua kingereza ndio kila kitu na unatuchelewesha.

Kule mbugani Arusha kuna wamasai wazee wanaongea kingereza cha Malkia mwenyewe lakini wanaishi kwenye nyumba za majani makavu.
 
Tukienda kupatana kuhusu mikataba, tunatumia kiswahili na kuwa na mkalimani!!?
Tukienda kuomba China, pamoja na muwakilishi wa China kutumia kichina, sisi huwa tunatumia kiswahili na kuwa na mkalimani wa kuwatafasiria Wachina!!??
Magufuli na Samia kingereza chao ni cha kawaida sana lakini wameweza kuitoa Tanzania kutoka katika uchumi wa chini na kuupeleka katika uchumi wa kati na kazi anayoifanya Samia kabla ya 2030 ataiacha nchi mahali pazuri sana.

Kingereza ni lugha tu, kuijua au kutoijua haimpunguzii mtu chochote.
 
Hapa hatuzungumzii utajiri, topic iliyopo kwenye huu uzi ni Kiingereza. Tusiende nje ya mada, it doesn't take a neuroscientist to know that.
China hawaongei kabisa hiki kingereza, kiuchumi tunawafikia?.

Wajerumani na Wafaransa kingereza ni lugha ya pili kwao, vipi tunawafikia kiuchumi kwa namna yoyote ile?.
 

Halafu anaongea kwa CONF kwelikweli.
 
China hawaongei kabisa hiki kingereza, kiuchumi tunawafikia?.

Wajerumani na Wafaransa kingereza ni lugha ya pili kwao, vipi tunawafikia kiuchumi kwa namna yoyote ile?.
Endeleeni tu kulishana ujinga. Ndo mana mnashindwa ku compete kwenye kazi na shughuli za kimstaifa. Wachina kibiashara wanakitumia kiingereza kuliko waingereza wenyewe.
 
Endeleeni tu kulishana ujinga. Ndo mana mnashindwa ku compete kwenye kazi na shughuli za kimstaifa. Wachina kibiashara wanakitumia kiingereza kuliko waingereza wenyewe.
Kingereza ni lugha tu mkuu denning. Wapo mabilionea hawakijui na wameajiri wafanyakazi wengi wenye umahiri wa kukiongea.
 
Duh! Let me search for it.
Ndalichako yule sijui alipata je udakitari PhD, wote na mwendazake kiingereza kinawasumbua na Zelensky wa Ukurain anawaxidi wakati hakusoma kiingereza
Hata kule NEC sijui alipenyapenya vipi? It baffles me!
 
Sina matatizo na kiingereza chake, iyo tumeizoea sasa, hata majirani zetu wanajua kiingereza ni taabu kwetu. Maana ukienda Zambia na Malawi hata muuza nyanya sokoni anaongea kiingereza kizuri kuliko Waziri wa Tanzania.

Nimefurahi pale alipomuuliza mchina fedha zetu tumekupa unajua? Mchina akakubali. Lakini Wachina kwenye Habari zao wanasema hizo pesa wametoa wao, sasa nimeelewa.
 
Binafsi naona kaongea vizuri, labda na mimi ndio walewale.

Tutofautishe grammatical errors na accent, grammar yake haikuwa mbaya, tena yupo vizuri kuliko wengi wetu. Accent yake ni ya kiafrika, au tunataka aongee kama muingereza?
Humu wengi wanaomsema huyo waziri ukiwaambia waandike au kuongea hicho hicho kingereza basi utaishia kusikitika tu ni wachache sana humu wanaoweza kunyoosha kingereza kama cha kina Kiranga, Nyani Ngabu au Prof Griff
 
Naomba mwenye CV ya Ulega. Maana si kwa English mbovu !! Na wachina unaongea vile je wangekuwa Wazungu na lugha yao.

Huyu na Ndalichako na Waziri Jenista hawachekani
Huyu jamaa ni PhD holder open university ametunukiwa last year kule Kigoma.
 
Tatizo ni kuwa uchawa ndiyo kigezo kikubwa siku hizi
Ccm na meritocracy ni Sawa na mafuta na maji!! Wanafikiri wakiwa na watu waliowazidi akili watawachanganya na kuzuia uharamia wao kwa nchi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…