Waziri Ulega akipiga mkwara na Kingereza cha ugoko

Ndalichako yule sijui alipata je udakitari PhD, wote na mwendazake kiingereza kinawasumbua na Zelensky wa Ukurain anawaxidi wakati hakusoma kiingereza
Elimu ya bongo namna sana
 
Kwanini asiongee kiswahili fasaha, halafu mkalimani akafanya kazi yake?

Mbona wachina wanapenda kuongea na wageni kwa kutumia lugha yao?
Kwanini tunakinyanyapaa kukiongea kiswahili?

Siwezi kumlaumu ama kumcheka Waziri kutokana na mfumo mbovu wa ufundishaji wa lugha ya kingereza nchini Tz.
 
Tuwekee na clip ya kingereza walicho ongea wachina hapo
 
Kwahiyo unataka watu wateuliwe kwa kigezo cha lugha ya kingereza na sio uwezo wao kwenye utendaji?

Anyway, wawe wanatembea na wakalimani ili mambo yasiwe mengi.
 
Hata kumbe huna uelewa wa hoja ya mleta uzi.
Kwa watu kama mawaziri lazima tuwe na watu ambao wapo vizuri kichwani, ukijumlisha na lugha ya kiingereza kwani ndio wanaoingia mikataba kwa niaba ya wizara na nchi.

Kipimo cha mafanikio sio utajiri.
Kila mmoja ana kipimo chake cha mafanikio kulingana na mtazamo wake kuhusu mafanikio.
 
Kwani kiingereza ni intelligence ya mtu au ni lugha tu kama kiswahili, mbona wa Japan wengi hawajui kiingereza..........hizo ndo comment za watanzania walio shindwa kumudu lugha ya kiinaereza.
Kulinganisha japan na tanzania sio sahihi mkuu, sisi tanzania huko serikalini english ni lugha walioamua kuikumbatia katika sehemu mbalimbali. Hivo tukiwaona viongozi wanavochemka sisi tunafurahi
 
Wewe unaejua kingereza unamzidi 🥶uwezo wako kung'amua mambo ni mdogo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…