Waziri Ulega Akutana na Wakuu wa Taasisi Wizara ya Ujenzi

Waziri Ulega Akutana na Wakuu wa Taasisi Wizara ya Ujenzi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI ULEGA AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI WIZARA YA UJENZI.

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi katika Ofisi ndogo za Wakala ya Barabara (TANROADS), leo tarehe 11 Disemba, 2024 Dar es Salaam.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour, pamoja na Wakuu wa Taasisi kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS), Wakala wa Majengo (TBA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) na Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT).

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Ulega amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumteua kuhudumu katika Wizara ya Ujenzi.

Aidha, Waziri Ulega ameahidi kuwapa ushirikiano Wakuu wa Taasisi hizo na kuendeleza yale yote ambayo yapo katika utekelezaji yakiwemo majukumu makuu ya Wizara ya Ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege, ujenzi na usimamizi wa vivuko, ujenzi wa majengo na nyumba za watumishi na Viongozi wa Serikali.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour amemkaribisha Waziri Ulega na kumuahidi ushirikiano kutoka kwa Menejimenti na watumishi wa Wizara pamoja na Taasisi zake
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.47.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.47.jpeg
    390.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.47 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.47 (1).jpeg
    306.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.48.jpeg
    387.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.48 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.48 (1).jpeg
    312.7 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.48 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.48 (2).jpeg
    498.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.49.jpeg
    305 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.49 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.49 (1).jpeg
    414.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.49 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.49 (2).jpeg
    264.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.50.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-11 at 14.44.50.jpeg
    373.3 KB · Views: 5
Huyu baba hata u m/kiti wa kijiji hauwezi, afu anakabidhiwa wizara Lol
 
Back
Top Bottom