Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewataka wataalamu wa sekta ya ujenzi kubuni mbinu za kupunguza foleni mijini na kuongeza mapato ya Serikali kupitia barabara za mwendokasi huku akipendekeza zitumiwe na magari binafsi kwa kulipia.
Akizungumza leo Alhamisi Februari 13, 2025 mkoani kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo mkoani Singida, Ulega alipendekeza mfumo wa kulipia kwa magari binafsi ili kutumia njia za Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) wakati wa msongamano mkubwa.
"Kwa nini barabara moja ibaki tupu kwa muda mrefu wakati magari mengine yamekwama kwenye foleni? Nchi nyingine zinatumia mfumo wa kulipia ili kuepuka foleni, tunaweza kufanya hivyo hapa pia," amesema Ulega.
Aidha, Ulega amesisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia thamani ya fedha katika usimamizi wa miradi ya barabara, madaraja, na viwanja vya ndege, huku akiagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kusimamia miradi ya dharura yenye thamani ya Sh868.56 bilioni.
Mkutano huo pia umejadili bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2025/26 kabla ya kuwasilishwa bungeni
Huyo ni mwendawazimu kweli kweli, hivi anajua malengo ya mwendokasi ni yapi? Kwahiyo mabasi yapambane tena na foleni? Hiyo itakuwa ni mwendokasi sasa?
Mabasi ya mwendokasi yanaitwa mwendokasi sio sababu yanaenda speed kubwa, la hasha, bali yanaitwa hivyo sababu yanapita njia isiyo na foleni, hivyo yanafika haraka.., na lengo ni watu waache magari binafsi nyumbani yanayokaa foleni na badala yake watumie usafiri wa umma usio na foleni. Sasa ukiruhusu gari binafsi zipite kwa kulipia , mwisho wa siku mwendokasi nayo itakuwa na foleni kama barabara ya kawaida, na kuharibu malengo yote ya mradi. sasa utaahira kama huu kweli mtu anapendekeza kabisa bila aibu.., jamani, hizi taka taka za namna hii zinapataje uwaziri.., how?!!!
Watatue tatizo la msingi wasianze kupoteza lengo la BRT.Walete hayo mabasi ya mwendokasi ili watu tuyatunie na tupaki magari magari binafsi.Wakitaka hivyo walete mradi mwingine wa expressway wa kulipia.
Kwa kukurupuka na miradi hawajambo
Na sasa wanataka kuwapa sijui kina nani tenda ya cable cars tuanze kupita juu kwa juu kwa kutumia nyaya
Kweli kuna mradi umefanikiwa tangu uhuru
My Take
Binafsi naona ni pendekezo zuri ambalo kitakuwa chanzo Cha Mapato na pia kusaidia kurudisha hela za Mkopo maana malengo ya BRT na uendeshaji wake umeshashindikana Bongo.