Kuna shida mahali tena shida kubwa sana. Kabla waziri hajatoa hilo tamko lake alitakiwa afanye utafiti yeye au wasaidizi wake kwa angalau hata wiki aone balaa lake. Sijui hao mawaziri huwa hawapigagi stori wenyewe kwa wenyewe. Maana lazima angejua Bashungwa na Chalamila walitoa agizo kama hilo japo haikuwa kulipia lakini balaa lake mwendokasi zikashindwa kutembea kabisa.
Suluhisho la mwendokasi ni serikali kuongeza mabasi tu. Na kwanini kupitia PPP anayohubiri Kafulila kila siku wasigawe njia kwa wawekezaji wa ndani kama Bakharesa, Abood, BM, Shabiby, n.k. na serikali ikabaki inakusanya kodi na mrahaba tu kama kwenye madini?
Hakuna mradi rahisi kuendesha kama mwendokasi sijui wasomi wanaopewa kuongoza huo mradi wanashindwa vipi kuuendesha kwa faida. Nina hakika hata leo ukiwapa mtaji wa mabasi hamsini tu umoja wa makondakta na madereva wa daladala japo sio wasomi sana hakuna abiria atakayekaa kituoni zaidi ya dakika 15 na ikifika mwezi wa sita watakuwa wameongeza gari nyingine hamsini na kuwa jumla mia.
Ni mtizamo tu