mdudu
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 7,013
- 10,000
Safi sana serikali ,Lisu na Zito Kabwe watanyooka tu
Walifikili hapa JF ni mahali pa kudangiaWatoto wa kiume kilasiku wanazidi kupungua hapa jamiiforum wamejaa makaka poa kila kukicha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Safi sana serikali ,Lisu na Zito Kabwe watanyooka tu
Walifikili hapa JF ni mahali pa kudangiaWatoto wa kiume kilasiku wanazidi kupungua hapa jamiiforum wamejaa makaka poa kila kukicha
Mjamzito alienda kujifungulia Amana hospital awe na 81,000/=. Ummy Mwalimu ni miongoni mwa mawaziri wabovu wanaongoza kwa kutoa matamko ya ovyo na ovyo kabisa!. Kama anataka watanzania watibiwe bure ni vema apeleke msaada huo wa matibabu ya bure bungeni ujadiliwe hatimaye upelekwe kwa Rais kuwa sheria vinginevyo aache progapanda hizi za majitaka.Hizi ni siasa tu ili waonekane kama wanajali watu kumbe ni bure kabisa.Mwanzo walitangaza wajawazito na watoto chini ya miaka mitano ni bure lakini ukienda unadaiwa pesa.Mawaziri mpunguze siasa mnakera sana
Rekodi nyingine ya awamu ya 6 hii..WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu, ameagiza matibabu ya malaria kutolewa bure kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali.Pia amewataka watoa huduma kuacha kutoza fedha kwa wananchi wanaofika kufanya vipimo vya malaria na kifua kikuu.
Pia amewataka watoa huduma kuacha kutoza fedha kwa wananchi wanaofika kufanya vipimo vya malaria na kifua kikuu.
Waziri Ummy alitoa maelekezo hayo jana mjini hapo wakati akizungumza na wananchi katika Zahanati ya Disunyara Halmashauri ya Kibaha alipokuwa katika ziara ya siku moja akiambatana na Mkurugenzi wa Mfuko wa kimataifa wa kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya (HIV), kifua kikuu (TB) na malaria (Global Fund) Peter Sand, aliyefika kujionea huduma.
"Kipimo cha malaria cha haraka ni (MRDT), dawa za malaria Alu na sindano ya malaria kali ni bure na kipimo cha kifua kikuu ni bure kwasababu ya Global Fund wanatusaidia tuweze kutokomeza magonjwa haya matatu," alisisitiza.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), malaria ni miongoni mwa magonjwa sita yanayochangia vifo vingi nchini sambamba na magonjwa ya mfumo wa hewa, kisukari na Ukimwi.
Katika hatua nyingine aliwataka wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kutoacha kutumia dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo (ARV) na pia kusitisha ngono zembe kutokana na kasi ya maambukizi iliyoko kwa sasa.
Kwa mujibu wa Ummy kumekuwapo na kusuasua kwa matumizi ya dawa za ARV kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi jambo ambalo ni la hatari.
"Kati ya watu 100 Tanzania wanaoishi na virusi vya ukimwi 95 wanatumia dawa tumeona kusuasua kwa matumizi ya ARV kwasababu watu hawaoni kwa hiyo wanaacha kutumia dawa," alisema Ummy.
"Wakati tunakaribia kuushinda Ukimwi, tunaanza kurudi nyuma hata kama huumwi unaona vimepungua tusiache kutumia dawa," alisisitiza.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, alisema Global Fund ndiyo wanaosaidia, na kwamba wanasaidiana na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya.
Kunenge alisema kuwa kiongozi Global amefika kujionea shughuli zinazofanywa na Mfuko huo kwa Tanzania amefika kutembelea baadhi ya vituo vya afya vya mkoa huo.
Mkurugenzi wa Global Fund, Peter Sand, alisema Mfuko huo umeridhishwa na huduma zinazotolewa hususani kukabiliana na magonjwa Ukimwi, malaria, kifua kikuu na huduma za mama na mtoto.
Sand aliwahikikishia kuwa Mfuko huo utaendelea kushirikiana na Tanzania kuendeleza mapambano dhidi ya kifua kikuu, Ukimwi, maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na malaria.
Chanzo: Nipashe