Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Mwanasiasa wa CCM ni muongo muongo, ila kwenye hii awamu ya tano mwanasiasa wa CCM ni "LIONGO"
 
So kilichotuponya watanzania ni maombi na sala? Sasa tufunge basi na kusali kwa ajili ya dunia. Tuwaombee na wao basi

Ndiyo kinachoendelea kufanyika.Ila dhihaka zao zinaweza zikawacost.
 
Watu wenye Corona hawaendi hospital maana wananyanyapaliwa. Wengi wako nyumbani wanatumia asili.

Ninavyoandika hapa amezikwa shemeji huko Moshi alikufa Corona huko kanda ya ziwa. Jumatano wiki hii anazikwa mwingine huko Marangu na mwili utapelekwa na watu wa afya kutoka Arusha. Mwingine atazikwa Rombo Ijumaa hii mwili utatolewa Moshi.

Je serikali inayo taarifa kamili za hali ya ugonjwa nchini? Watanzania tuchukue tahadhari Korona ipo na inaenda kasi sana.

Vaa barakoa , kula virurubisho, piga nyungu, epuka mikusantiko. Cha kusikitishaha toka ile tarehe 24 May walipotangaza hali si mbaya wagonjwa wamebaki 9 basi 99% ya watanzania wameyarudia maisha ya kawaida.

Life ni kama kawaida vijiweni mpaka daladala hakuna barakoa tena. Soko la Temeke Stereo nilipata hata yale mtanki ya maji ya kunawa hayana maji muda mrefu sana. Nihatari sana hii.
 
...Kudos kwa watumishi wote wa sekta ya afya kama ni kweli wamebakia wagonjwa wanne TUU...quote of the day ni i fear the government more than i fear terrorism...
Yaani baki kuelimisha familia yako tu. Hivi watu wanavyokufa na tunazika kila leo ni kwa faida ya nani? Huu uchumi ukikua watafaidi marehemu au?
 
Hili naweza kuliamini. Shughuli zinaendelea Tanzania nzima kama kawaida ila hata jirani au rafiki hajashikwa na huu ugonjwa. Ingekuwa ni kusambaa, kwa lifestyle iliyoko huku mtaani tunhekuwa tushazika wengi
 
Nadhan anamaanisha "wagonjwa" si "waathirika" wa covid-19, kama ni hivyo anaweza kuwa sahihi au hapana, yote kwa yote tuzidishe maombi na tahadhari.
 
Hongera sana, ni muda muafaka wa kutoa utaalamu kwa Nchi jirani.
 
... waliopungua ni waganjwa waliolazwa (4) ila Corona ipo; tusipochukua tahadhari tutarudi pale pale! Nadhani ndicho alichomaanisha.
Kama huenda alimaanisha hivi basi tusiache kuchukua tahadhari.
 
Hospitali hazipokei wagojwa na wengi wanajiuguza nyumbani bila data ku report.

Mimi najua watu wawili ambao hawajaripoti chochote lakini wamepambana wenyewe wiki kama nne. Hospital zimarudisha watu an hawana msaada.

Hakuna anayejua kuna wagojwa wangapi. Hal ni waliobaki kabla ya sera mpya ya kurudisha. Halafu waliokufa wamepiga marufuku kuwatangaza. Hakuna anayetuamini majirani bad wanapata na hakuna sayansi wala ushahidi wowote.

Lindeni wazazi wen achaneni na propaganda mpaka chanjo ipatikane
 
Back
Top Bottom