Waziri Ummy: Michango ya kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali isizidi Tsh. 188,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amepiga marufuku wakuu wa shule zote za serikali kutoza michango ya kujiunga na kidato cha tano zaidi ya Sh. 188,000.

ummy.jpg

Amesema mkuu yeyote wa shule atakayebainika kukiuka agizo hilo, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Ummy alitangaza katazo hilo jana alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Bihawana mkoani Dodoma kukagua utayari wa shule za serikali kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2021.

Alisema kiasi hicho kinajumuisha ada ya Sh. 70,000.

Waziri Ummy alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa mwaka huu ni 87,663 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule 476 na kutoa wito kwa wazazi ambao wataamua kuwapeleka watoto wao kwenye shule za binafsi kutoa taarifa kupitia mfumo, ili kutoa fursa kwa wengine.

Aidha, aliwataka wakuu wa shule kuandaa mazingira mazuri ya kuwapokea wanafunzi na kuwapo na mahitaji yote muhimu.
Aliwataka wanafunzi wa bweni kuripoti Julai 3 na wa kutwa Julai 5.

Kadhalika, alisema katika ajira mpya za walimu hivi karibuni hakuna shule itakayokosa mwalimu wa Fizikia wala Hisabati.

Alifafanua kuwa walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 wakati shule ambazo hazikuwa na mwalimu ni 1,100 na walimu wa Hisabati walioajiriwa ni 459 wenye shahada na stashahada 140 wakati uhaba ulikuwa kwa shule 400.

Chanzo: NIPASHE
 
Kama kichwa kinavyoeleza, kwa sasa shule nyingi hasa zile za Serikali kwa wanafunzi wanaoenda kuanza kidato cha tano zinaenda kufunguliwa. Lakini nilichogundua mbali na ada kuainishwa kwenye fomu za kujiunga, michango ni mingi sana inayofika karibia mara tano ya ada.

Waziri ingilia kati kuwanusuru wazazi na huu utitiri wa michango ikiwa tayari ada ambazo wazazi wanaweza kujitahidi kuzilipa zimeshawekwa. Huu ni sawa na upigaji kwa wakuu wa shule.
 
Safi kabisa maana kuna shule tumeambiwa tupeleke viti na Meza!
 
Hii tanzania ina viongozi wa ovyo yahn waziri anajitutumua kuwa kila shule itakuwa na mwl mmoja wa phy na math wakati mashule yao ya elimu bure yanabeba sio chini ya wanafunz 1000
 
Kama kichwa kinavyoeleza, kwa sasa shule nyingi hasa zile za Serikali kwa wanafunzi wanaoenda kuanza kidato cha tano zinaenda kufunguliwa. Lakini nilichogundua mbali na ada kuainishwa kwenye fomu za kujiunga, michango ni mingi sana inayofika karibia mara tano ya ada.

Waziri ingilia kati kuwanusuru wazazi na huu utitiri wa michango ikiwa tayari ada ambazo wazazi wanaweza kujitahidi kuzilipa zimeshawekwa. Huu ni sawa na upigaji kwa wakuu wa shule.
Na wanafunzi wengine wamepangiwa shule ambazo nauli tu ya kufika huko ni changamoto!! bado hiyo michango!! wahusika saidieni katika hili!!!twafaa awamu hii
 
Kuna Shule Moja michango tu imefikia jumla ya Tshs 145,000= nje ya Ada kwa mwanafunzi wa Kidato cha 5...
Uniform na mazagazaga mengine nayo imefikia 430,000=
Ni shida aisee.....na wanashupaza misuli ya shingo wanakwambia elimu bure.....hovyo sana hawa watu.
 
A'level hakuna elimu bure...michango ipo kama yote

Hata hivo sikubaliani na utaratibu unaotumika na baadhi ya shule kwenye kulipa michango hiyo...

Mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano, yamegeuka biashara kwa mkuu wa shule na makamu wake...hili ni tatizo kubwa japo mamlaka hazilioni
 
Hapo ndo upigaji unapotamalaki, tulitegemea ada iwe ime cover gharama za mwanafunzi......mzazi abaki na mahitaji kama uniform, stationeries na mahitaji mengine binafsi ya mwanafunzi, kweli watu wanatumia fursa.....
 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amepiga marufuku wakuu wa shule zote za serikali kutoza michango ya kujiunga na kidato cha tano zaidi ya Sh. 188,000.

ummy.jpg

Amesema mkuu yeyote wa shule atakayebainika kukiuka agizo hilo, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Ummy alitangaza katazo hilo jana alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Bihawana mkoani Dodoma kukagua utayari wa shule za serikali kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2021.

Alisema kiasi hicho kinajumuisha ada ya Sh. 70,000.

Waziri Ummy alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa mwaka huu ni 87,663 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule 476 na kutoa wito kwa wazazi ambao wataamua kuwapeleka watoto wao kwenye shule za binafsi kutoa taarifa kupitia mfumo, ili kutoa fursa kwa wengine.

Aidha, aliwataka wakuu wa shule kuandaa mazingira mazuri ya kuwapokea wanafunzi na kuwapo na mahitaji yote muhimu.
Aliwataka wanafunzi wa bweni kuripoti Julai 3 na wa kutwa Julai 5.

Kadhalika, alisema katika ajira mpya za walimu hivi karibuni hakuna shule itakayokosa mwalimu wa Fizikia wala Hisabati.

Alifafanua kuwa walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 wakati shule ambazo hazikuwa na mwalimu ni 1,100 na walimu wa Hisabati walioajiriwa ni 459 wenye shahada na stashahada 140 wakati uhaba ulikuwa kwa shule 400.

Chanzo: NIPASHE
sasa mwalimu mmoja wa hesabu kwa shule yenye minimum madarasa manne, anafudishaje kwa ufanisi!! jamani muwe serious japo kidogo!!
 
Back
Top Bottom