Nyinyi viongozi mna faida gani kwetu ikiwa kila jambo linalotaka leadership mnafeli?Mna maana gani kwetu?Hopeless!Rasilimali za ardhi ya Africa zimejaa utajiri,lakini hamuutumii kufanya nchi mnazoongoza ziwe tajiri.Mungu kawapeni mtu bora kabisa,mweusi mwenye nguvu na uvumilivu.Immunity ya mwafrika inawapeni muda wa kutosha kupambana na huu ugonjwa lakini bado hamtumii hizi priviledge za Africa.Hatukuwa na ulazima wa kufikia emergence kama ya wazungu sababu ya slow spreading ambayo kila mtu dunia nzima walishangaa na hakuna namna ya kuelezea sababu zaidi ya strong immunity aliyonayo mwafrika na idadi kubwa ya waafrika kutosafiri sana nje ya nchi,lakini nyinyi viongozi mna laana gani sijui mmeshindwa kutumia hii divine priviledge
Mkuu 'kerubi afunikae', umeandika mengi ya msingi sana, hasa kuhusu kiburi walichoonyesha hawa viongozi wetu hapo mwanzo wa ugonjwa huu.
Njia zao ni zile zile, za kujiona wao ni tofauti na wengine na kufanya yao bila hata ya kuwa na ushahidi wowote kuwa njia zao ni bora kuliko zinazotumiwa na wengine kote dunia nzima.
Kwa kufanya hivyo, wanategeshea tu wapewe sifa endapo Mungu atapitishia mbali hili janga, watu wetu wasidhurike zaidi. Hapo ndipo utakapowasikia wakijipiga vifua kwa kujisifu, kana kwamba walifuata mwongozo wowote uliokwishaonyesha ubora wa njia hizo kuliko zinazofuatwa na wengine wote.
Katika andiko lako, kidogo ni kama unajichanganya, ndio nikaona niku'quote' na kuandika juu ya haya uliyoandika hapa.
Ninakubaliana nawe moja kwa moja kwamba, mwafrika, kama atapona kwa kiasi kikubwa na huu ugonjwa, ili maambukizi na 'fatality' zisiweze kufikia zile za wenzetu huko nje, kuepuka kwetu huko kutahusiana kwa kiasi kikibwa na kinga ya aina fulani, kimwili au kimazingira.
Kwa hapa tulipofikia sasa, ninayo matumaini makubwa kwamba Afrika tutatoboa. Hatutafika kule kwa hali ya ulaya na Marekani.
Pale ninapoona kama umejichanganya ni ..., kama kinga itakayotulinda inatokana na miili yetu kuwa nauwezo wake, basi, pengine hata bila kujali waliyofanya hawa viongozi wasiokuwa makini ni sehemu mhimu inayopelekea miili yetu ijilinde na haya magonjwa ya milipuko kila mara inapojitokeza.
Inawezekana nikawa sikuunganisha vizuri kukuonyesha mkanganyiko unaoonekana katika hoja zako; kwa sababu nimetiririka tu baada ya kukusoma na sikurudi nyuma kuhakiki.
Ikinibidi, italazimu nikuchambue taratibu kuonyesha ni wapi nilipoona mkanganyiko huo.
Lakini kwa yote, naungana nawe kulaumu 'cavalier attitude' waliyoionyesha viongozi wetu mbele ya ugonjwa hatari kama huu.
Hili linawaondolea sifa ya kuwa viongozi wanaojali maisha ya wananchi wao.
Walichoweka mbele ni kulinda uchumi zaidi ya kulinda maisha ya wananchi.
Tungekuwa na wananchi wanaojitambua vyema, hili jambo lingewapa wakati mgumu sana hawa viongozi. Lakini, ndio hivyo, basi. Tutaishia kusifu hatua zilizochukuliwa kutulinda, kumbe ni bahati au kudra za Mwenyezi Mungu ndizo zilizo tuepushia janga.