Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Viongozi wenyewe mapopoma.mawazo kama hayo wataya toa wapi.
 
Huu ujinga ndio mnaoutegemea kuwalaza akili watu.

Hebu eleza kama Tanzania nzima wakifa watu mia mbili kwa siku, kutokana na sababu yoyote ile, kama utajua hapo ulipo kuwa hao watu wamefariki siku hiyo?

Hata serikali yenyewe haina takwimu hizo!

Na huo ndio usingizi wa pono unaokulaza wewe.
Sasa wewe umejuaje kuwa waliokufa ni wengine kama huna takwimu? Usilete unyumbu hapa! Pumbavu!
 
Mkuu 'kerubi afunikae', umeandika mengi ya msingi sana, hasa kuhusu kiburi walichoonyesha hawa viongozi wetu hapo mwanzo wa ugonjwa huu.

Njia zao ni zile zile, za kujiona wao ni tofauti na wengine na kufanya yao bila hata ya kuwa na ushahidi wowote kuwa njia zao ni bora kuliko zinazotumiwa na wengine kote dunia nzima.

Kwa kufanya hivyo, wanategeshea tu wapewe sifa endapo Mungu atapitishia mbali hili janga, watu wetu wasidhurike zaidi. Hapo ndipo utakapowasikia wakijipiga vifua kwa kujisifu, kana kwamba walifuata mwongozo wowote uliokwishaonyesha ubora wa njia hizo kuliko zinazofuatwa na wengine wote.

Katika andiko lako, kidogo ni kama unajichanganya, ndio nikaona niku'quote' na kuandika juu ya haya uliyoandika hapa.

Ninakubaliana nawe moja kwa moja kwamba, mwafrika, kama atapona kwa kiasi kikubwa na huu ugonjwa, ili maambukizi na 'fatality' zisiweze kufikia zile za wenzetu huko nje, kuepuka kwetu huko kutahusiana kwa kiasi kikibwa na kinga ya aina fulani, kimwili au kimazingira.

Kwa hapa tulipofikia sasa, ninayo matumaini makubwa kwamba Afrika tutatoboa. Hatutafika kule kwa hali ya ulaya na Marekani.

Pale ninapoona kama umejichanganya ni ..., kama kinga itakayotulinda inatokana na miili yetu kuwa nauwezo wake, basi, pengine hata bila kujali waliyofanya hawa viongozi wasiokuwa makini ni sehemu mhimu inayopelekea miili yetu ijilinde na haya magonjwa ya milipuko kila mara inapojitokeza.

Inawezekana nikawa sikuunganisha vizuri kukuonyesha mkanganyiko unaoonekana katika hoja zako; kwa sababu nimetiririka tu baada ya kukusoma na sikurudi nyuma kuhakiki.

Ikinibidi, italazimu nikuchambue taratibu kuonyesha ni wapi nilipoona mkanganyiko huo.

Lakini kwa yote, naungana nawe kulaumu 'cavalier attitude' waliyoionyesha viongozi wetu mbele ya ugonjwa hatari kama huu.
Hili linawaondolea sifa ya kuwa viongozi wanaojali maisha ya wananchi wao.

Walichoweka mbele ni kulinda uchumi zaidi ya kulinda maisha ya wananchi.

Tungekuwa na wananchi wanaojitambua vyema, hili jambo lingewapa wakati mgumu sana hawa viongozi. Lakini, ndio hivyo, basi. Tutaishia kusifu hatua zilizochukuliwa kutulinda, kumbe ni bahati au kudra za Mwenyezi Mungu ndizo zilizo tuepushia janga.
Kuna nzige wapya huko wanataka kuvamia East Africa,wana nguvu zaidi ya hawa wa sasa na wako wengi mno,miezi 9 wakiwa wanbreed tu huko wanakotokea.Umelipata hilo mkuu?Na tabia za aina hii za viongozi wetu katika emergence sijui tunafikaje aisee.Lazima tubadili fikra na utendaji wetu kuendana na mabadiliko ya kidunia yaliyopo.Tuamke na kujua tuna bahati mbaya ya kuishi wakati wa great changes za dunia na vilivyomo.
Baada ya hii corona kuna economic crisis kubwa,je tunajiandaa na hayo?!Au tunasubiri kama tulivyoisubiri corona?!
 
Mi nashauri serikali kwakuwa ni ngumu kufanya total lock down tufanye inter regional lockdown mikoa yote ifungwe.JWTZ wasimamie hili , kama upo Moro stay hapohapo ,kama dar the same ili kama mlipulo ukitokea at least tuokoe mikoa mingine isiguswe tukomae nalo kwenye infected zones.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo habari ya nzige ukiiwaza ni kama fursa mpya tusiyojua jinsi ya kuitumia mkuu 'kerubi afunikae'.
Hiyo ni 'protein' inayoelea tu bila ya matumizi sahihi.

Utadhani natania, lakini seriously, hatuwezi kupata njia nzuri ya kuivuna 'protein' hiyo amabayo inazalishwa bila ya gharama zozote, gharama pekee ni huko kuvuna na kutengeneza iwe katika hali bora ya matumizi?

Kama hatutaki kuwala, hata kuwalisha kuku wetu haiwezekani?

Anyway, tatizo letu ni hilo hilo, hatujifunzi chochote tokana na majanga haya na kujiandaa kujikinga pale yanapotokea tena.

Huo mstari wako wa mwisho, hapo ndipo penyewe akili zetu zinapotakiwa kuelekezwa. Lakini wapi, tutatoka hivi hivi.
 
Mi nashauri serikali kwakuwa ni ngumu kufanya total lock down tufanye inter regional lockdown mikoa yote ifungwe.JWTZ wasimamie hili , kama upo Moro stay hapohapo ,kama dar the same ili kama mlipulo ukitokea at least tuokoe mikoa mingine isiguswe tukomae nalo kwenye infected zones.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa na Wuhan, au sio?
 
Kwa taarifa hii ya leo iliyotolewa na waziri wa afya na maelezo yake kwamba sasa tunaambukizana sisi kwa sisi, na pia kwa kuona Dar ndo ina wagonjwa wengi, naomba kutoa maoni kwamba, safari za mabasi kutoka Dar na kuingia Dar zisimamishwe.

Kwa wastani kuna mabasi 200 yanayotoka Dar na kuingia Dar kwa siku. Ni mabasi yenye safari za zaidi ya masaa siyo chini ya 3 na mengine huchukuwa masaa zaidi ya 16. Kwa tabia ya ugonjwa wa Corona na maabukizi yake, ni rahisi mgonjwa mmoja kuambukiza zaidi ya nusu ya abiria ndani ya basi moja. Vituo vya mabasi havina ukaguzi wa wagonjwa na mazingira ya ndani ya mabasi huwa ni magumu sana.

Tupeane maoni na tusikilizane kwamba pamoja na shughuli zetu kuendelea, serikali tusidieni kwa kuzuia safari za mabasi ya mikoni ili kuinusuru nchi.
 
Nimesoma kimeti wewe!!!!
Imani + utaalamu.
Huwezi jua. Labda watu wameshapiga ramli kwa hiyo wanajua kila kitu.
Ninaacha komenti yangu namna hiyo ikiwa tungo tata. Mengenya upate maana mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa taarifa hii ya leo iliyotolewa na waziri wa afya na maelezo yake kwamba sasa tunaambukizana sisi kwa sisi, na pia kwa kuona Dar ndo ina wagonjwa wengi, naomba kutoa maoni kwamba, safari za mabasi kutoka Dar na kuingia Dar zisimamishwe.

Kwa wastani kuna mabasi 200 yanayotoka Dar na kuingia Dar kwa siku. Ni mabasi yenye safari za zaidi ya masaa siyo chini ya 3 na mengine huchukuwa masaa zaidi ya 16. Kwa tabia ya ugonjwa wa Corona na maabukizi yake, ni rahisi mgonjwa mmoja kuambukiza zaidi ya nusu ya abiria ndani ya basi moja. Vituo vya mabasi havina ukaguzi wa wagonjwa na mazingira ya ndani ya mabasi huwa ni magumu sana.

Tupeane maoni na tusikilizane kwamba pamoja na shughuli zetu kuendelea, serikali tusidieni kwa kuzuia safari za mabasi ya mikoni ili kuinusuru nchi.
Dar kwa sasa inastahili kabisa lockdown

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom