Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

BREAKING NEWS : Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuongezeka kwa watu 53 wenye maambukizi ya Virusi vya Corona, ambapo imepelekea jumla ya visa vya Corona kuwa 147.

38 - DSM
10 - Zanzibar,
1 - Kilimanjaro,
1 - Mwanza,
1 - Lindi
1 - Kagera
1 - Pwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaandika hapa kuharibu biashara ya mtu yoyote wala sijaishauri serikali naitii kulingana na Tito 3:1

Kulinganaa na mfumuko wa Covid-19 katika jiji la Dar es Salaam napata mashaka sana na mlipuko wa huu ugonjwa mikoa jirani

mfano;

Kuna mtu mmoja anagari labda kama 10 zinazoingia Dodoma kila siku kutoka Dsm, kiwango cha chini ni abiria 40 kwa basi moja, kwa siku unakuta yeye tu anaingiza abiria 400

Kuzuia watu kusafiri hakuepukiki kabisaa

sidhani kama hawa wafanyabiashara wetu wana ujuzi mkubwa wa kupambana na hii kitu
Goodnight
 
Tuzidi kuchukua tahadhari zote za kitaalamu na kisayansi, short of that tutakufa. Mungu asione hayo mataifa mengine wanaokufa kila siku kwa nini?
 
Ningekuwa mimi ni Rais ningefunga mipaka na viwanja vyote vya ndege hasa vya kimataifa
  • Ningepiga marufuku usafiri wa mabasi na dala dala nchi nzima
  • Ningepiga marufuku ibada zote
  • Ningepiga marufuku masoko makubwa isipokuwa zile soko mjinga za mitaani
  • Ningepiga marufuku kumbi zote za starehe zikiwemo bar na maeneo ya vilevi
  • Majeshi yote yangepewa majukumu mapya ya kuhakikisha kuwa marufuku hizi zinatekelezwa
  • Balozi zetu zinapewa majukumu ya kuwatambua watanzania waliokwama ughaibuni na kuwapa huduma maalumu ya Quarantine mpaka hali itulie
  • Serikali ingesimamisha matumizi ya pesa kwenye miradi mikubwa Kwani huko mbeleni, lolote linaweza kutokea
 
Lazima tuvunje rekodi ya Afrika Mashariki, kuna sehemu tumekosea, Hii kasi ni ya kipekee, na sioni kama kuna Tahadhari kubwa saana ya kuiepuka, hadi imefikia waumini wameanza kuamua wenyewe kwa wenyewe kuzuia wenzao wakae majumbani, hivyo basi kifuatacho kufikia Jumatano ijayo tutakuwa tunaongoza Afrika Mashariki...nategemea Juma tatu au Jumanne kuwepo kwa tamko gumu kuliko yote kutoka Serikali, hebu tujiulize, ni wapi tumekosea hadi kufikia huku tuelekeako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom