Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Wacha tufe! Binadamu tumekuwa wengi sana kwenye uso wa Dunia! Hivi sasa tunakaribia watu Bilioni nane huku binadamu ambao wamesha kufa mpaka sasa tangu kuumbwa kwa Ulimwengu wakikadiriwa kuwa Bilioni 50! (Hii ni zaidi ya miaka 5000 BC na miaka mingine 2000 AD wamekufwa watu bilioni 50)!

Kwa maana hiyo Annual rate of death has been somewhere around watu milioni 7. (50,000,000,000/7000).
Korona haijaweza kuua hata watu laki tano kati ya watu milioni saba 'wanaotakiwa kuwa wamekufa' kwa mwaka Duniani!
kweli mkuu inatakiwa watu wafe ili tubalance nature

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wenzangu anzeni kuweka akiba ya chakula, inasubiriwa pasaka ipite nchi nzima tuingie kwenye karantini.
 
Duh, ina maana huyu waziri hakugundua hilo mapema? afukuzwe kazi imemshinda

Yaani wakitaka kuokoa maisha ya Watanzania mikusanyiko ya makanisani au misikitini inabidi isitishwe. Naona kama kuna aibu aibu kwa viongozi lakini watakuja kujuta pale tutakapo lazimika kufunga kila kitu kama NY.
 
Bwana mungu ni mwema ataturinda.bwana anasema "sitakuacha uangamie,nitakuacha upite katika changamoto"
 
Hawa kuna kitu wanatuficha hasa kwenye takwimu za walioambukizwa huu ugonjwa nchini. Ngoja ngoma isambae watafichua wenyewe.
Kwenu kuna wagonjwa wangapi ambao hawajatangazwa? Hebu tuanzie hapo ili tuone kama tunavichwa ama la!
 
Yaani wakitaka kuokoa maisha ya Watanzania mikusanyiko ya makanisani au misikitini inabidi isitishwe. Naona kama kuna aibu aibu kwa viongozi lakini watakuja kujuta pale tutakapo lazimika kufunga kila kitu kama NY.
Kwani huko makanisani na miskitini kwa sasa wanaenda wengi kiasi gani??
 
Yaani wakitaka kuokoa maisha ya Watanzania mikusanyiko ya makanisani au misikitini inabidi isitishwe. Naona kama kuna aibu aibu kwa viongozi lakini watakuja kujuta pale tutakapo lazimika kufunga kila kitu kama NY.
Rais wa nchi anamvunja nguvu Waziri Ummy ndiyo maana anasita kutoa tangazo la kusitisha mikusanyiko ya nyumba za ibada.
 
Hapo wanaanza kutengeneza mazingira ya kutangaza idadi yenyewe na siyo zile ngonjera

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧

Ni kweli, na itaitwa 'community transmission' kutoka 'local transmission!
 
Tulionya tangu mwanzo, lakini wapi aisee!

Tuliomba mipaka ifungwe and restricted entry kwa watu wanaotoka nje ya nchi especially high risk countries.

Tukasema pia strict and mandatory quarantine kwa wageni ni muhimu sana.

Nchi kama Rwanda, Ghana, Botswana zilionyesha njia, mipaka ilifungwa,ndege zote mpaka za shirika lao (Rwandair) zikawa grounded, partial lockdown,curfew,etc

Wakati nchi nyingi duniani zina-take decisive measures, sisi kila kitu wazi.
Sio tu kila kitu kiliendelea kuwa wazi lakini pia watu waliombwa waendelea kurundikana kwenye nyumba za ibada kwa sababu Corona ni shetani na hawezi kufika huko.

Yaani Mecca na Vatican na sehemu nyingi kote duniani wamesimamisha ibada za pamoja kukwepa maambukizi, sisi huku tumegundua kuwa tunafahamu dini kushinda wengine.
You don't fight a pandemic by gambling.
Eti ugonjwa unaweza usije! Au hata ukija wataambukizwa watu wachache halafu ugonjwa utaisha!

Oooh, hatuwezi kufunga mipaka tutakosa watalii! Tukasema humu, huo uamuzi ni counterproductive kwa sababu pandemic imeshika kasi huko wanapotoka watalii, itafika muda hawatakuja kabisa. Yametimia, watalii hawaji, hoteli nyingi zimefungwa na tourism industry ina suffer haswa.

Kwa wale vichwa ngumu, tukumbushane tu kuwa sote tuko hatarini.
Our healthcare system is too weak to handle this contagion. Nina uhakika nchi nzima haina hata ventilators zinazozidi 100, supply ya PPE ni ndogo na mengine ya muhimu kama hospital beds per capita ni hovyo kabisa.

Read between the lines,takwimu wanazotoa hawa watu zinatia mashaka sana.
 
Back
Top Bottom