Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Kama ilikuwa international transmission, then local transmission, then community transmission, itakayofuata ni nini? Halafu, kama modelling imefanyika, si watoe tu prediction.

Hivi ni lazima watu waende kwenye nyumba za ibada? Sasa vile vitabu vya dini tunavyo nyumbani vya nini?
 
707d942ba2ea64172d6020f25daf90dc

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

WATANZANIA wametakiwa kuongeza umakina katika kujilinda na virusi vya corona (COVID-19), kwa kuwa siku chache zijazo, nchi itaingia katika hatua ya kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Na kwamba, katika hatua hiyo, mtua anaweza kupata maambukizi na asijue amepata kutoka wapi.
Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya akifungua mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini kitaifa leo tarehe 9 Aprili 2020, amesema maambukizi kutoka nje (imported transmition) yamedhibitiwa.
“Tumetoka kwenye maambukizi yanayoletwa kutoka nje ya nchi (imported transmission), tuko kwenye local transmission (maambukizi ya ndani).

Hivi sasa, takwimu za kesi za jana na juzi, zinaonesha tumeanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe, hili lazima tuweke wazi. Hakuna maambukizi ya nje,” amesema Waziri Ummy na kuongeza:

“Tumeanza kwenye ‘local transmission’ na siku chache tutaingia kwenye ‘community transmission,’ maana yake tutapata mgonjwa hatutajua ameupata wapi huo ugonjwa, ndio maana tunafanya ufuatiliaji.

“Na ndani ya siku chache tutaingia katika hatua hiyo, lazima niwaambie ukweli viongozi wa dini, nisiwafiche kwamba soon tutaingia kwenye community transmission.”

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema Tanzania imevuka kihunzi cha Shirika la Afya la Kimataifa (WHO), cha kuwa na wagonjwa 1,000 wa COVID-19 ifikapo katikati ya mwezi Aprili mwaka huu.

“Tunamshukuru Mungu, hadi sasa anatutendea maajabu, tumevuka kihunzi WHO, walisema mwezi Aprili tutapata wagonjwa 1,000 na kati kati ya mwezi Mei tutapata wagonjwa 10,000 lakini kila mtu akichukua nafasi yake, tunaweza kuvuka hicho walichotutabiria,” amesema Waziri Ummy.
 
Hakuna kitu wanaogopa viongozi wa Tanzania kama kuwaambia viongozi wa dini wafunge misikiti na makanisa ili kuepuka maambukizi zaidi yaani wanajifanya watakatifu kuliko hata walioleta hizo dini wenyewe. Sasa ona mama anavyojibembeleza kwa viongozi wa dini badala ya kuwaambia wafunge majumba ya ibada kwa muda kama tulivyofunga shule na vyuo anajiuma uma tu. Kufunga makanisa na misikiti siyo kufunga maombi au sala. Hivyo tutavifanya tukiwa majumbani mwetu na Mungu atatusikia.
 
Hivi kuna quarantine Dar tu mbona sasa hivi kuna wimbi la wasafiri kutoka south Africa transist Kenya na kenya to south Africa sasa hivi hakuna ndege na wengine hawataki shughuli zao zisimame Wizara ya mambo ya Ndani immigration muko wapi kwenye hili mbona mmetelekeza wananchi, kama lila wanatoka nje apelekwe quarantine je ni wanao safiri kwa ndege tu,kuwe na barrier za imagination kukagua wanaingia law barabara
 
Back
Top Bottom