Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Lazima tuvunje rekodi ya Afrika Mashariki, kuna sehemu tumekosea, Hii kasi ni ya kipekee, na sioni kama kuna Tahadhari kubwa saana ya kuiepuka, hadi imefikia waumini wameanza kuamua wenyewe kwa wenyewe kuzuia wenzao wakae majumbani, hivyo basi kifuatacho kufikia Jumatano ijayo tutakuwa tunaongoza Afrika Mashariki...nategemea Juma tatu au Jumanne kuwepo kwa tamko gumu kuliko yote kutoka Serikali, hebu tujiulize, ni wapi tumekosea hadi kufikia huku tuelekeako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jumatano ni mbali sana

"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
Lazima tuvunje rekodi ya Afrika Mashariki, kuna sehemu tumekosea, Hii kasi ni ya kipekee, na sioni kama kuna Tahadhari kubwa saana ya kuiepuka, hadi imefikia waumini wameanza kuamua wenyewe kwa wenyewe kuzuia wenzao wakae majumbani, hivyo basi kifuatacho kufikia Jumatano ijayo tutakuwa tunaongoza Afrika Mashariki...nategemea Juma tatu au Jumanne kuwepo kwa tamko gumu kuliko yote kutoka Serikali, hebu tujiulize, ni wapi tumekosea hadi kufikia huku tuelekeako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Lile jitu la Equador
 
1587288833846.png
 
Tunashukuru muitikio mkubwa uliofanywa baada ya Mh. Rais kuwaomba Watanzania kwa dini zao na imani zao kuliombea Taifa dhidi ya janga la Corona. Muitikio ulikuwa mzuri na nyoyo zimeshiba imani ya Mungu si haba.

Sasa nadhani nguvu ielekezwe kuwahamasisha wananchi kuchukua hatua zaidi za kujikinga na Corona. Bado eneo hili halijatendewa haki kwa mtazamo wangu. Natarajia kusikia siku tatu za kuhamasisha uvaaji wa Barakoa, na kuhamasisha michango ya hiari kwa ajili ya wasiojiweza kupatiwa vifaa vya kinga.

Natarajia nione hamasa hiyo ya kuvaa barakoa na michango ianze kwa Rais wetu ili nchi nzima iingie hamasa.

Ni hayo tu.

Kishada
 
Mh. Ummy Mwalimu: Update on #COVID19Tanzania. Samples tested at the National laboratory between 18th - 20th April, 84 new cases in Tanzania mainland and Zanzibar. Total confirmed cases to-date 254. We regret to announce 3 new COVID-19 deaths in Dar es salaam. #CoronaInazuilika #JikingeWakingeWengine
 
Endeleeni kuficha ugonjwa. Wakiupata watu kadhaa hapo Lumumba mtatia akili.
Corona haina lumumba Wala ufipa ikipiga ina piga tu chukua tahadhari mwenyewe fuata mashariti na taratibu za kujikinga ukiona vp jifungie na familia yako ndani kulaumu hovyo hovyo sio kinga ya Corona hao hao unao watumikia wanachukua tahadhari na familia zao
 
Atakapoanza kuugua waziri ndio mtajua hii sio movie ya kibongo
Mmejawa na kiburi na uongo mwingi kwa sababu ya mtu mmoja hivi

Ummy sijui utawaambia nini WaTz tukianza kwanza tumeanza kuzikana
Covid-19 Tz ipo kila mahali

Mnaleta siasa kwenye uhai wa watu
Uzuri huyu virus hana uchaguzi ni wote kwa wote
Wakusanya watu akina bashite na wengineo muanze kujiandaa

Punguzeni viburi
Siasa ipi walio ileta hebu oredhesha hapa tujue hizo siasa walizo zileta
 
Hakuna kitu hapo usipoteze mda
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiongea na viongozi wa dini, amesema kuwa kwa sasa hali ya ugonjwa wa Korona nchini imebadirika kutoka kuletewa ugonjwa na watu kutoka nje imegeuka kuwa hali ya kuambukizana sisi wenyewe kwa wenyewe.

Wakati huo Waziri Ummy ameonya kuwa ndani ya muda mfupi ujao maambukizi yatageuka kuwa maambukizi ya jumuia(Community Transmission), akawataka watanzania wajiandae kwa hali hiyo.

MY TAKE:
Tuliwaambia mapema kabisa, Fungeni hii mipaka ya nchi mtatuletea janga, lakini tukaendelea kujivutavuta sasa tunakwenda kwenye hali ngumu sana

Tumeona juzi hapa mtu katoka Dubai tarehe 24 March kashuka Dar, kisha tukasikia kaenda mwanza tarehe 29 March alipopimwa na kukutwa na Korona, huyu mtu ilikuwaje hakuwekwa karantini?

Kwa hiyo ina maana Kwenye Karantini hatukuwa serious na pia kwenye kufunga borders hatukuwa serious, sasa matokeo yake huenda tukaingia kwenye hali ngumu

Kiufupi serikali haiwezi kukwepa lawama hali ikigeuka na kuwa mbaya nchini.

Saa hivi hao wachina tuliokuwa tukiwapokea kwa bashasha pale KIA kipindi wapo kwenye hali ngumu sasa hivi wamefuta residence permit na viza za foreigners walio nje ya mipaka ya nchi yao na wanawasumbuasumbua foreigners walio nchini mwao kwa sasa kwa kuwabagua na kuwafanyia kila aina ya ubaguzi kuwa eti ndo wanawapelekea New cases, Wanawanyima hoteli, kuingia kwenye supermarkets,Weusi wakipanda mabasi wachina wanashuka. Sasa najiuliza Je sisi wema wetu wa kufungua mipaka kipindi kile umetuletea nini zaidi ya kuhatarisha maisha ya watu wetu?

Msikilize Ummy Mwalimu hapa akiongea
View attachment 1413820

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom