jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Nampongeza Waziri wa Afya kwa kupata updates mbalimbali za sekta unayoisimamia kwa wakati na hivyo kuwa responsive.
Nikijikita katika mada,
Mimi ni muumini wa sustainable health system financing yaani sekta ya afya inahitaji njia endelevu ya rasilimali fedha ili iweze kuleta tija. Mfumo wa afya nchini kama ilivyo nchi nyingi maskini bado inategemea uhisani wa marekani na mataifa mengine, hii ni hatari kwa usalama na ustawi wa Taifa. Yaani siku tukimchukiza Marekani, Uingereza au Japan tunarudi miaka 50 nyuma, hili ni jambo hatari.
Bado bajeti ya sekta ya afya ni changa mno yaani haijafikia 15% ya GDP Kama ilivyowahi kuazimiwa huko Abuja. Hivyo sekta ya afya inaidai serikali deni la kufulfill hiyo asilimia ili angalau kutoa huduma.
Bado Serikali haitoi ruzuku stahiki sawia na hitajika kwenye huduma za afya ukilinganisha na sekta nyingine mfano Elimu. Ukihitaji mifano fanya mapitio ya uwekezaji katika huduma za afya vs huduma nyingine (fanya rejea kwenye bajeti ya huduma za jamii bungeni kwa miaka 10).
Sekta ya afya imejitahidi kuja na bunifu mbalimbali ili kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha ili iinuke,
hapo utaona in recent 7 years or so kumekuwa na mabadiliko chanya.
Nikiri kuwepo kundi la wahuni na wafanyabiashara walioanza kujitokeza kwenye sekta ya afya wenye nia ya kubadili sekta hii kutoka katika utoaji huduma na kuwa bisashara (hii ni kwenye sekta binafsi na mashirika ya dini sio public). Kamwe sikubaliani na dhana hii ya wahuni kwani imeprove failure hata Marekani.
HIVYO NI LAZIMA WADHIBITIWE!
Lipo jambo la kisera ambalo Wizara ya Afya inalikwepa kwepa na kuishia kuja na matamko ya taharuki.
Jambo hili niliwahi kulisemea humu humu jamvini, na niliwahi kuliulizia katika moja ya midahalo ya wagombea urais miaka kadhaa imepita. Jambo hilo sio lingine bali ni bima ya afya kwa wote. Mh. Rais Samia Suluhu Hassan wakati anaingia madarakani na alipokuwa anawaapisha mawaziri wake awamu ya awali kabisa aliwaagiza Wizara ya Afya kuja na Sera ya Bima ya Afya kwa wote. Alisisitiza swala hilo lichakatwe na kufikia mwisho lakini hadi sasa hakuna draft yoyote iliyowasilishwa bungeni badala yake tunaona purukushani za majukwaani. HII SIO SAWA.
Consultation fee ni sehemu muhimu ya ada za kumuona ,kumsikia na kupata ushauri wa daktari (sio kumuona daktari tu). Unapoingia chumba cha daktari yapo mengi yanayofanyika kabla ya kwenda kwenye vipimo n.k.
MAONI
Sekta ya afya imevamiwa na ngwini wengi sana, na ngwini hawa waemkuwa wasemaji sana huku uwezo wao ukiwa mdogo.
Kuna tatizo la wasaidizi wa madaktari, yaani ukianzia wauguzi, wafamasia, wateknolojia wa maabara nk, ambao baada ya kupewa fursa wameanza kupeleka umbea kwa viongozi badala ya kutoa ushauri kuntu.
Pia naamini madhila mengi ambayo umeyatolea ufafanuzi yanatokana na sekta binafsi na mashirika ya dini. Basi ni muhimu kurusha jiwe katika eneo husika na sio kwa public sector. Rationing ya bei ianzie sekta binafsi.
Mhe. Waziri tumia vyanzo sahihi kupata genuine challanges na solutions katika sekta ya afya. Nashauri ukipata fursa au ukiamua kutengeneza fursa hebu waite waganga wafawidhi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali (ngazi ya msingi) upate maoni yao ili kuja na Sera bora.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!