Waziri Ummy nashauri ukae na wataalamu wa afya kabla ya tamko la bei ya huduma za afya

Kada zote hizo zimeletwa na kada hiyo muhimu ,hiyo ni fact....daktari anayajua yote ya waliobakia ...hutaki soma
Hawa madaktari wetu wanaochungulia vitu kwenye google....
Ni hivi huyo daktari hawezi kukamilisha kazi yake bila kusaidiwa narudia kusaidiwa na hizo kada nyingine, zaidi ya hapo atababia kwenye google na kukubandika midawa ukafe mbele, na hiyo ndio sekta ya afya bongo sababu hata ukifa, suala zima linabadilishwa na kuwa la kiroho kuwa bwana amekutwaa, hakuna uwajibikaji....
 
Mtoa mada una grandiosity sanaaa
Et kada saidizi za daktar hahaha hakuna kitu ka hicho

Btw m naona consultation fee ni kitu ambacho kinatakiwa kiwepo ili kuzipa uhai hospital kimapato, Tukileta siasa hapa hospital nyingi zitafeli kimapato na ndo zitakuwa anguko la hizo sekta au kugeuka mzigo mkubwa kwa serikali badala ya kufanya issue za maendeleo itatumia pesa zote kutibu raia wake

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe unaposema kwamba kuna mianya kwenye sekta ya afya nchini lakini tatizo hilo halisababishwi na uwezo wa serikali kuhudumia wananchi bali ni uwezo wa vyombo vyetu vya afya kujiendesha vyenyewe. Katika haya yote, ni vyema kufahamu kwamba huwezi kutoa huduma za afya bure kwa wananchi. Na sio kwamba haya yanafanyika makusudi bali ni uwezo wa kuweza kumudu gharama hizi kila siku kwa watu zaidi ya milioni arobaini na tano. Kwa sasa, gharama ya kujiunga NHIF kwa mtu mzima ni shilingi 192,000 kwa mwezi. Ingawa huduma ni mbovu na upatikanaji wa dawa ni hadimu, huduma ya afya kwa watoto chini ya miaka mitano na wazee zaidi ya miaka sitini ni bure. Labda inawezekana kuwa na bima kwa kila mwananchi lakini hili linawezakanaje kama hospitali ya taifa ya Muhimbili inategemea mafungu kutoka serikalini kila mwaka ili kuwa wezesha kuwa hudumia wagonjwa wa NHIF. Sababu zipi zinafanya hospitali kushindwa kuendesha huduma za NHIF bila kutegemea fedha kutoka serikali?. Nakubaliana na hoja yako kwa kiasi fulani ila nina amini hospitali zinapoteza mapato kwa kushindwa kufuatilia fomu za wagonjwa na hushindwa kufuatilia vizuri uwepo wa madawa kwa wagonjwa wa NHIF. Labda form 2c kuondolewa itawa sukuma wasimamizi kufuatilia uwepo wa dawa hospitalini.
 
Unataka upate matibabu bora katika hospitali binafsi kwa bei ya dezo. Haki yako wewe ni kutibiwa hospitali za umma sio hospitali binafsi.

Afya ni biashara vilevile sio huduma inapokuwa katika sekta binafsi.

Wewe hangaika na hospitali za umma ndio zinaendeshwa kwa kodi yako.

Kama huna uwezo wa kulipa hospitali binafsi waache wenye uwezo na wanaotaka huduma bora waende huko.. unataka huduma katika hodpitali binafsi zishuke ili wote wapate huduma mbovu kisa wewe huwezi tibiwa hospitali binafsi.
 
Consultation fee ktk hospitali za umma ifutwe kwa sababu serikali inalipa mshahara na gharama zingine za uendeshaji, hakuna haja ya kulipa fedha ya kumwona daktari wakati ni sehemu ya majukumu yake.

Mh waziri yuko sahihi. Consultation fee ifutwe
 
All too shallow when not contradictory.

Sustainable healthcare financing ndio kusubiri ruzuku ya serikali ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…