Waziri Ummy: Toto Afya Kadi haijafutwa ila sasa Watasajiliwa Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh 50,400

Sasa watoto wanasajiliwa vipi katika hiyo bima na kwa gharama gani?
 
Watoto under 5 wanatibiwa bure kwenye hospitali zote za serikali
 
Ili ku fast track kuondoa maradhi kwa watoto utaratibu wa toto bima ungebaki kama zamani, kwa sasa utaratibu haueleweki vizuri kwa kupitia shule zipi? na kwa vipi? kuna mkanganyiko mno
 
Watoto under 5 wanatibiwa bure kwenye hospitali zote za serikali
Embu jiongeze na ufikirie wewe.
Kama watoto under five ni kweli bure, sasa serikali inapoteza nini ikiwa watu watataka kuwakatia bima watoto wa under five?

Kwanini serikali ilikuja na bima ya toto afya wakati mpango wa matibabu bure kwa watoto under five ulikuwepo siku zote kabla hata NHIF haijaanzishwa

Logic ni kwamba, kama kweli watoto under five wanapata matibabu bure na bora, automatically Toto afya ingekosa watumiaji na wala serikali isingepoteza muda na nguvu kuifuta.
 
Mbwa Tanzania ndio pumzi imekata kila mtu anakula pesa uchaguzi 2025 ni kiama Kwa watanzania
 
Nakosa neno sahihii ya kuwashauri ila ki ukweli viongozi wetu wanaonekana kama wapumbavu flani hivi.
Sio tu wanaonekana bali ni wapumbavu haswa.

Kama wanashindwa kujali afya za watu wanaowaongoza watajali nini sasa?
 
Pamoja na changamoto ya bima,Pia njoo Kaliua District Hospital Kuna upigaji wa kutisha pale wakati hata viongozi wengine wakiwa wanatazama tuuu,(Ummy Mwalimu)

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa NHIF endeleeni kutoa elimu kwa watanzania kujua umuhimu wa BIMA tusiwe watu wa kulalamika kila wakati ,pili endeleeni kuhamasisha watu wengi zaidi kujiunga na Bima ya Afya na ndio namna ya kulinda mfuko wetu
 
Ili ku fast track kuondoa maradhi kwa watoto utaratibu wa toto bima ungebaki kama zamani, kwa sasa utaratibu haueleweki vizuri kwa kupitia shule zipi? na kwa vipi? kuna mkanganyiko mno
Watoto wanajiunga kuanzia chekechea ,primary ,shule za sekondari tena mpaka vyuoni ni 50400 na hata makundi maalum kama yatima nao wanaungwa kupitia vituo vyao rasmi kwa bei ileile ,lengo la NHIF kama mfuko wowote ule duniani ni kuboresha na kuimarisha mfuko
 
Tofauti ya usajili wa shuleni na huu wa sasa uliofutwa ni upi? Ndio hasara itapungua?

Hao ambao hawajaanza shule hawana haki ya matibabu?

Bla bla za waziri.
Swali zuri sana.
 
Ili ku fast track kuondoa maradhi kwa watoto utaratibu wa toto bima ungebaki kama zamani, kwa sasa utaratibu haueleweki vizuri kwa kupitia shule zipi? na kwa vipi? kuna mkanganyiko mno
Sema nn mkuu, ule utaratibu wa zamani ilikuwa no way mfuko ungetoboa, watu walikuwa wanasajili watoto wagonjwa tu,

Sio kwa ubaya ila ndo ukweli, hili ilibidi lije tu, kingine Waziri ajitahidi kupunguza upigaji wa hospital hasa za Pvt toka kwenye mfuko na serikali,
Mara nyingi mtu unaenda unatibiwa huduma moja ila kwenye bima wanaandika huduma 5
 
Tofauti ya usajili wa shuleni na huu wa sasa uliofutwa ni upi? Ndio hasara itapungua?

Hao ambao hawajaanza shule hawana haki ya matibabu?

Bla bla za waziri.
Kwa mujibu wa ummy ambao awajaanza shule means wapo 5 years ama chini ya hapo watakuwa kwenye msamaha wa huduma za afya. Japo uo msamaha ni kichekesho, mtoto anaweza asipate vipimo au akapata ila dawa ukaambiwa ununue. Kuishi Tanzania ni mateso makali sana 😭😭😭
 
Je, ni kweli kwamba watoto wote Tanzania wanasoma? Nafikiria watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri kabla ya kwenda shule. Lakini pia kuna watoto ambao hawaendi shule kwa sababu mbalimbali na wengine wameacha shule kwa sababu mbalimbali. Je, hawa wanasajiliwa shule zipi?
 
Ummy ni msanii sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…