Waziri Ummy: Toto Afya Kadi haijafutwa ila sasa Watasajiliwa Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh 50,400

Waziri Ummy: Toto Afya Kadi haijafutwa ila sasa Watasajiliwa Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh 50,400

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema mpango wa bima ya afya kwa watoto wanaojiunga kwa hiari (Toto Afya Kadi) haujafutwa, bali kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili watoto.

Akikanusha uvumi huo kwenye mtandao wake wa X (zamani Twitter), Waziri Ummy ameeleza kuwa utaratibu wa sasa ni kwa watoto kusajiliwa shuleni kwa gharama ya shilingi 50,400 ili waingie wengi wasio wagonjwa na hivyo kuweza kuchangia wachache watakaougua.

"Bima ni sayansi. Huwezi kuwa na bima inayokusanya shilingi bilioni 5; fedha inayolipwa kwa watoa huduma, yaani matumizi, ni bilioni 40. Natamani hizo nguvu za kupotosha zingetumika kuleta ushauri ni vipi NHIF itaweza kuvutia watoto wengi zaidi ambao hawana changamoto za kiafya ili kuweza kulipia wachache watakaopata changamoto za kiafya," amesenma.

“Kwa sasa Toto Afya Kadi wamesajiliwa watoto laki 2 tu, tuhimizane wazazi/walezi kuwakatia bima ya afya watoto wetu. Naamini wakisajiliwa watoto japo asilimia 10 tu (milioni 3) kwa utaratibu huu basi tunaweza kuhakikisha ustahamilivu na uendelevu wa fao hili." Amesema

Aidha, Waziri amesema sera ya watoto wa umri chini ya miaka 5 au watu wasio na uwezo kupata msamaha bado haijafutwa, na kwamba hospitali zote za umma zinaendelea kuhudumia watoto wa umri chini ya miaka mitano kupitia utaratibu wa misamaha.

====View attachment 2750967
Sasa watoto wanasajiliwa vipi katika hiyo bima na kwa gharama gani?
 
Watoto under 5 wanatibiwa bure kwenye hospitali zote za serikali
 
Ili ku fast track kuondoa maradhi kwa watoto utaratibu wa toto bima ungebaki kama zamani, kwa sasa utaratibu haueleweki vizuri kwa kupitia shule zipi? na kwa vipi? kuna mkanganyiko mno
 
Watoto under 5 wanatibiwa bure kwenye hospitali zote za serikali
Embu jiongeze na ufikirie wewe.
Kama watoto under five ni kweli bure, sasa serikali inapoteza nini ikiwa watu watataka kuwakatia bima watoto wa under five?

Kwanini serikali ilikuja na bima ya toto afya wakati mpango wa matibabu bure kwa watoto under five ulikuwepo siku zote kabla hata NHIF haijaanzishwa

Logic ni kwamba, kama kweli watoto under five wanapata matibabu bure na bora, automatically Toto afya ingekosa watumiaji na wala serikali isingepoteza muda na nguvu kuifuta.
 
Mbwa Tanzania ndio pumzi imekata kila mtu anakula pesa uchaguzi 2025 ni kiama Kwa watanzania
 
Nakosa neno sahihii ya kuwashauri ila ki ukweli viongozi wetu wanaonekana kama wapumbavu flani hivi.
Sio tu wanaonekana bali ni wapumbavu haswa.

Kama wanashindwa kujali afya za watu wanaowaongoza watajali nini sasa?
 
Kwa sasa NHIF endeleeni kutoa elimu kwa watanzania kujua umuhimu wa BIMA tusiwe watu wa kulalamika kila wakati ,pili endeleeni kuhamasisha watu wengi zaidi kujiunga na Bima ya Afya na ndio namna ya kulinda mfuko wetu
 
Ili ku fast track kuondoa maradhi kwa watoto utaratibu wa toto bima ungebaki kama zamani, kwa sasa utaratibu haueleweki vizuri kwa kupitia shule zipi? na kwa vipi? kuna mkanganyiko mno
Watoto wanajiunga kuanzia chekechea ,primary ,shule za sekondari tena mpaka vyuoni ni 50400 na hata makundi maalum kama yatima nao wanaungwa kupitia vituo vyao rasmi kwa bei ileile ,lengo la NHIF kama mfuko wowote ule duniani ni kuboresha na kuimarisha mfuko
 
Tofauti ya usajili wa shuleni na huu wa sasa uliofutwa ni upi? Ndio hasara itapungua?

Hao ambao hawajaanza shule hawana haki ya matibabu?

Bla bla za waziri.
Swali zuri sana.
 
Ili ku fast track kuondoa maradhi kwa watoto utaratibu wa toto bima ungebaki kama zamani, kwa sasa utaratibu haueleweki vizuri kwa kupitia shule zipi? na kwa vipi? kuna mkanganyiko mno
Sema nn mkuu, ule utaratibu wa zamani ilikuwa no way mfuko ungetoboa, watu walikuwa wanasajili watoto wagonjwa tu,

Sio kwa ubaya ila ndo ukweli, hili ilibidi lije tu, kingine Waziri ajitahidi kupunguza upigaji wa hospital hasa za Pvt toka kwenye mfuko na serikali,
Mara nyingi mtu unaenda unatibiwa huduma moja ila kwenye bima wanaandika huduma 5
 
Tofauti ya usajili wa shuleni na huu wa sasa uliofutwa ni upi? Ndio hasara itapungua?

Hao ambao hawajaanza shule hawana haki ya matibabu?

Bla bla za waziri.
Kwa mujibu wa ummy ambao awajaanza shule means wapo 5 years ama chini ya hapo watakuwa kwenye msamaha wa huduma za afya. Japo uo msamaha ni kichekesho, mtoto anaweza asipate vipimo au akapata ila dawa ukaambiwa ununue. Kuishi Tanzania ni mateso makali sana 😭😭😭
 
Waziiri wa Afya mh Ummy Mwalimu amesema Toto Afya Kadi haijafutwa ila Utaratibu ndio umebadilika sasa Watoto Watasaniliwa Shuleni kwa gharama ile ile ya tsh 50,400.
---
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Toto Afya Kadi haijafutwa ila kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili ambapo utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh. 50,400 ili waingie wengi, wasio Wagonjwa na hivyo kuweza kuchangiana wachache watakaogua.

Akijibu hoja za Wadau mbalimbali kupitia mtandao wa X leo, Ummy amesema “Bima ni Sayansi, wakate wengi wachangiane wachache watakaougua, Toto Afya Kadi haijafutwa, kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili, utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh. 50,400 ili waingie wengi, wasio Wagonjwa na hivyo kuweza kuchangiana wachache watakaogua”

“Kwa sasa Toto Afya Kadi wamesajiliwa Watoto laki 2 tu, tuhimizane Wazazi/Walezi kuwakatia Bima ya Afya Watoto wetu, naamini wakisajiliwa Watoto japo asilimia 10 tu (Milioni 3) kwa utaratibu huu basi tunaweza kuhakikisha ustahamilivu na uendelevu wa fao hili”

“Mwisho, Sera ya Watoto wa umri chini ya miaka mitano au Watu wasio na uwezo kupata msamaha bado haijafutwa, Hospitali zote za umma zinaendelea kuhudumia Watoto wa umri chini ya miaka mitano kupitia utaratibu wa misamaha”

“Nimeshaelekeza NHIF kutoa elimu zaidi kuhusu Watoto wanaokatiwa Bima ya Afya kwa hiari kuwa utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe kupitia Shuleni kwa gharama ile ile ya Tsh. 50,400 au kwa utaratibu wa kifurushi cha Familia, NHIF washirikiane na Kamati za Shule kutoa elimu hiii, nasi tuendelee kuhimizana na kuhamasishana kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa kila Mtu, tusisubiri hadi tuwe Wagonjwa ndio tukate bima”

Source: Millard Ayo
Je, ni kweli kwamba watoto wote Tanzania wanasoma? Nafikiria watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri kabla ya kwenda shule. Lakini pia kuna watoto ambao hawaendi shule kwa sababu mbalimbali na wengine wameacha shule kwa sababu mbalimbali. Je, hawa wanasajiliwa shule zipi?
 
Kwa mujibu wa ummy ambao awajaanza shule means wapo 5 years ama chini ya hapo watakuwa kwenye msamaha wa huduma za afya. Japo uo msamaha ni kichekesho, mtoto anaweza asipate vipimo au akapata ila dawa ukaambiwa ununue. Kuishi Tanzania ni mateso makali sana 😭😭😭
Ummy ni msanii sn
 
Back
Top Bottom