Kwako Mh. Waziri wa Afya wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Ndugu Ummy Mwalimu.
Kwanza pole kwa kazi nzito unayoifanya yakusimamia wizara nyeti na ngumu yenye wataalam wengi wenye weledi, kadhia, hamu na kamu katika kuleta maendeleo chanya hususan katika sector ya Afya.
Mh. Waziri mimi ninayeandika makala hii ni mtaaluma wa fani zote mbili ambazo huleta mvutano usio na tija katika taifa letu, nina Diploma in Pharmaceutical science na Bachelor of medicine and surgery zote kutoka Oslo School of medicine nchini Norway.
Nasikitika kusema kwamba hali ya utendaji kazi katika sector ya afya inaharibiwa na watu wenye academical fallacy and abuse, watu hawa hujiona kuwa vyeti wanavyomiliki vinawapa dhima yakubeba dunia nzima katika mifuko yao wanayoweka shilingi, hali hii huleta utengano na hali ya kudharauliana katika taaluma walizopo, hii haipo tu katika kada ya afya bali katika fani zote zinazohisika na utendaji kazi kwa kutumia taaluma.
Nimesikitishwa na mtu anayejiita professor huku akijitwika vyeo kama mmed and PhD, akisahau kuwa anaaibisha wataaluma nguli katika sekta ya afya wenye wadhifa kama huu mathalani Prof. Sarungi ambaye amefanya mambo mengi mazuri katika wizara ya Afya.
Nilipojaribu kuingia katika mtandao wetu wa medical council of Tanganyika kumtafuta mwanataaluma huyu sikuweza kupata taharifa zake katika database ya baraza letu, ndipo nilipojua kuwa huyu ni kijana wa hovyo ambaye atakuja kuingia kwenye kundi la wataaluma wenye academical fallacy and ignorance kwa spidi ya 4g, kwa uelewa wake mdogo wakuchanganua mambo nimeona kabisa huyu ni mwanafunzi tena wa mwaka wa kwanza semester ya Kwanza Aliyegusa gusa human anatomy and physiology na kuanza kuona ameshamaliza taaluma nzima ya afya, ambaye hajui hata umuhimu wa team work katika kumuhudumia mgonjwa hospitalini.
Akishindwa hata kujua kuna kitu kinaitwa University prospectus ambacho kingemsaidi kujua anachokisoma mtaaluma mwingine kina mwingiliano gani na yeye, anashindwa hata kutambua kuwa hata wafanyakazi wa hospital wasio na utaalam wa tiba hupewa mafunzo juu ya magonjwa, dalili zake na namna ya kujikinga awapo katika mazingira yake ya kazi, leo hii anatoka kijana mmoja wa hovyo nakuandika kuwa mwanataaluma aliyefunzwa kwa miaka 5 hajui magonjwa na dalili zake? Hii ni hatari sana na academical fallacy ni ugonjwa unaotafuna wengi.
Katika pitapita zangu nikakutana na andiko la ndugu Yoshua nguyahambi aliyejishusha kuwa darasa la saba B ilihali kwa aliyoeleza inahakisi yeye ni mtaaluma anayejua anachokifanya napenda kuchangisha andiko lake na uzi wangu ili kuweza kusediment ujumbe wangu kama ifuatayo;
Yoshua Nguyahambi, Darasa la Saba B
Ndugu zangu nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nimeisoma kwa makini Makala ndefu ya mtu anayejiita Prof. Patrick Koboko, nashawishika kukiri wazi kwamba Profesa (Kama anavyojiita) amefanya upotoshaji wa makusudi kwa mhe. Waziri wa Afya na Umma wa watanzania kuhusu Addo na taaluma ya ufamasia.
Kwanza, katika makala yake amedai kazi ya mfamasia ni Kutunza na kuifadhi dawa, kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa, ameenda mbele zaidi na kusema kazi ya mfamasia siyo drug administration eti hii ni kazi ya watu wengine, ameendelea kudai kwamba mfamasia hajasomea magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi na hajasomea dalili za magonjwa, huu ni upotoshaji wa kijinga na makusudi kabisa uliofanywa na mtu wa ngazi ya uprofesa, angekuwa kwenye nchi za wenzetu angeshaitwa na kunyang'anywa uprofesa mara moja!
Hivi katika akili ya kawaida tu ya la saba B, kama yangu, mtu anaweza kukutengezea dawa kiwandani kama alivyodai anayejiita profesa, bila kujua issue za drug administration, epidemology, Anatomy, Physiology, Parasitology, Pathology, Medical semiology, medical toxicology, microbiology, biochemistry, Parasitology? Yaani mtu akutengenezee Paracetamol na asijue namna ya kuitoa kwa mgonjwa? Anasahau kabisa wao (wafamasia) watengenezaji wa dawa ndio wanawaandalia leflet zinazoonyesha namna dawa inavyopaswa kutumika, athari zake, n.k. Profesa wakati unaandaa makala hii ulikuwa wapi? Au ulikuwa na hangover ya K-vant?. Wakati mwingine tunapoamua kuandika makala sensitive na zinazogusa moja kwa moja Umma wa watanzania tusisukumwe na jicho la wivu, husda na kijino pembe kwa taaluma za wengine.
Profesa Patrick Koboko MD, MMED,PhD(kama anavyojiita) amenifanya mimi darasa la saba B nirudi kuangalia tena Prospectus ya vyuo vinavyotoa course za ufamasia, kuangalia je madai yake aliyoyatoa kuhusu wa wafamasia yana ukweli? Ni halali? Mathalan ukisoma prospectus ya chuo kikuu cha Muhimbili ya 2019/2020 – 2020/2021 ukurasa wa 75, kuna maneno yasomeka hivi, nanukuu "Pharmacy education embraces the search, development, formulation, analysis, storage and distribution of products for maintenance and restoration of good health as well as provision of information and guidance on proper use of medicines."
Sio kazi yangu darasa la saba B kumtafsiria maneno hayo, lakini ni wazi kuwa wafamasia ndio wanataaluma pekee wanaondaliwa sio tu kwajili ya yale aliyosema, wafamasia wanapaswa kuyafanya lakini pia kwajili ya kulea na kutoa taarifa sahihi za matumizi sahihi ya dawa, Prof. Koboko (kama anavyojiita) alipaswa alijue hili mapema hata kabla hajafikiria kuandika makala yake.
Kwahiyo kama darasa la saba B nampa home work profesa Koboko (kama anavyojiita) aende aipitie tena Prospectus ya Muhimbili na vyuo vingine vinavyo offer digrii ya ufamasia, aangalie vizuri kwa kulinganisha na hizo taaluma nyingine ni wapi kwenye Prospectus hizo mfamasia haandaliwi kutoa dawa kwa mgonjwa?
Litakuwa kosa kubwa la karne kama usimamizi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vitaondolewa kwenye mikono ya wafamasia kwa maana ya Baraza la famasi, kwasababu ya ushauri wa ki husda na kijino pembe ulitolewa na huyo anayeitwa Profesa, kwa sababu kwa mfumo wa elimu ya Tanzania ni wafamasia pekee ndio wameandaliwa kwa jukumu hilo. Profesa kama anavyojiita alipaswa kulifahamu hili.
KUHUSU ADDO.
Arudi aangalie vizuri kwanini wizara ya afya iliamua kuanzisha mafunzo hayo, ingawa ni kweli kuna mapungufu lkn haiondoi nia njema ya Serikali kupitia wizara ya Afya iliyoamua kuanzisha mafunzo hayo, ambapo awali yalikuwa chini ya TFDA sasa hivi TMDA, na baadae uratibu wake ukahamishiwa baraza la famasi kwasababu wao ndio wadau & walezi sahihi wa mambo yote yanahusiana na dawa, vifaa tiba na vitendanishi
Upo ushahidi wa wazi kabisa wa baadhi ya maduka haya ya dawa muhimu ambayo wanataaluma wenzetu (wasio wafamasia) wameyageuza kuwa Zahanati bubu kinyume kabisa kanuni zinazoruhusu uanzishaji wa maduka ya dawa muhimu unavyotaka, na ndicho anachojaribu kushauri Profesa (kama anavyojiita) kuwa maduka haya yageuzwe kuwa zahanati bubu kwa kupewa matabibu na Manesi bila kufundishwa chochote kuhusu malengo ya uanzishwaji ya maduka haya, kama nilivyosema awali litakuwa kosa kubwa la karne kuupokea ushauri huo bila kuzingatia ukweli niliouanisha kwenye makala yangu" mwisho wa andiko la Yoshua.
Ni rahi yangu kwa madaktari wote nchini kutambua, kuheshimu na kuthamini uwepo wa kila mmoja wetu katika sekta ya Afya, sisi hatuna authority yeyote yakushusha, kutweza na kubagaza taaluma zingine, nichelee kusema kwamba kwa sasa kipindi ambacho niko masomoni (Resident 2) wafamasia wamekuwa msaada mkubwa kwangu especially katika kufahamu dawa za aina mbalimbali hata zile ambazo haziko katika scope ya masomo yangu, ndugu hawa wako honest sana na wengi hupenda kurejea katika maandiko "books or publication" incase akihisi kitu hana uhakika nacho hali ambayo ni tofauti kwetu sisi madaktari ambapo uhusi kufanya hivyo ni kujishusha thamani na kuonekana HUJUI, nimepractice nchini Sweden na nakiri kusema hali ni tofauti Sana ukilinganisha na nchini kwangu, sikuwahi kusikia mvutano wakitaaluma katika nchi yoyote huku ulaya wala marekani na wao ndio chachu ya mifumo hii ya afya, sembuse sisi tuliopokea kama mapokeo..ni Aibu lakini ndio uhalisia.
Mwisho kabisa nachukua fursa hii kuwataka radhi wafamasia wote waliokerwa na andiko lile, niwatie moyo kufanya kazi kwa weledi kutokana na maadili ya kazi yenu, mchango wenu ni wamuhimu katika sekta ya afya, mnatusahihisha na mengi sana especially drug interactions and drug overdose kwa hili siwezi ficha mnatusaidia sana.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki taaluma ya Afya nchi Tanzania.
Doctor junior
Resident in internal medicine.