Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
Nime mwelewa vizuri sana Waziri lichukue hili. Lifanyie kazi.
 
Hapana, siyo kitu kimoja ni vitu viwili tofauti.
Drug administration ni kumpa mgonjwa dawa au mgonjwa mwenyewe kutumia dawa kwa maelekezo aliyopewa. Si lazima nesi ampe dawa (administer) dawa kwa kila mgonjwa.

Nesi atampa mgonjwa dawa ya sindano kwa mfano, kama mgonjwa yupo hospitalini. Lakini dawa nyingi huwa self-administered na mgonjwa mwenyewe.

Daktari ha'dispense wala ha'adaminister' dawa.

Dispensing ni kutoa dawa kwa mgonjwa kunakofanywa na mfanyakazi wa afya, iwe hospitalini au madukani
Daktari ana prescribe dawa
 
Hakuna mfamasia anayesema kuwa wanaweza kutoa kila aina ya dawa kwa kila aina ya ugonjwa bila prescription ya daktari. Ila ukweli ni kwamba anayejua madhara ya dawa zaidi ni mfamasia wala si daktari. Tatizo lililopo ni daktari kutaka kufanya kazi kwenye pharmarcy kwa kujitawala bila uangalizi wa mfamasia!! Daktari baki hospitalini, mfamasia baki kwenye pharmacy!! Daktari una hila za kula ugali wa kidaktari na ule ugali wa kifamasia, HAPANA!! Daktari analalamika mfamasia kugawa dawa kwenye duka la madawa, hivi ni nani anaweza kusema kuwa mfamasia hawezi kusoma prescription ya daktari? Kwani huko hospitalini si kuna pharmacy pia? Ni nani huwa anasimamia na kutoa dawa kwenye chumba cha kutolea dawa cha hospitalini??
Kwakweli mpaka ulipofikia huu mjadala sijauelewa vizuri kutokana na kukosa background ya mfumo wetu wa utoaji dawa hospitalini, kwenye pharmacies na nini hasa kinachogombewa humu.

Hoja nyingi zinazobishaniwa humu kijijini kwetu mfumo wake ni tofauti inaonekana.

Ni hivi kwa mfumo wa kijijini kwetu dawa anaandika Dokta kupitia ushahidi wa vipimo kila kitu huku ni evidence based; so hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuandika dawa nje ya hospitali ata kama ni dokta.

Dawa zozote ambazo zinahitaji mixing kama antibiotics fluids and other drips hiyo kazi inafanywa na nurse, kitu kingine nurse kwa kuwa yupo na mgonjwa muda mrefu kupitia uzoefu wake anauwezo wa kuchua clinical decision bila ya Dr hali ya mgonjwa inapobadilika na kunahitajika intervention za dharura.

Nurse pia anafahamu pathophysiology za magonjwa ya ward anayofanya kazi akiona dawa aliyopendekeza Dr ailingani na hali ya mgonjwa anaweza shauri tofauti there is always a senior nurse to consult kila ward ndio in charge ambae ataamua.

Kama kuna dawa za kupewa kutumia nyumbani ndio mgonjwa unaenda kuchukua pharamacy kwa prescription ya Dokta.

Otherwise kazi za pharmacy zinasimamiwa na pharmacists not anyone else; na kwenye medicine kwa taratibu zake kama kuna mtu ameajiriwa kuuza dawa au kutoa huduma yoyote ata ya kumwangalia mgonjwa (care assistant) kama ajasomea maswala afya lazima apewe basic training ya kazi kulingana na majukumu yake vinginevyo aruhusiwi you are not allowed to delegate duties to anyone who is not trained to perform them in a health system nadhani ndio msingi wa ADDO huko pharmarcy.

Sasa kwenye huu mjadala I am lost sijui hata wanabishania nini tena if anything nilichojifunza mfumo wa wetu wa everyday operation za hospitali unatatizo unahitaji wataalamu kuangalia upya; kila mtu mjuaji.

Sidhani ata kama hospitali zetu zina utaratibu wa ku record medical errors na sababu zake kama ni uzembe (negligence) mtu anachukuliwa hatua za kisheria au hata kama wana record any other critical incidents na kuzichunguza ili baadae watu wachukiwe hatua if it’s deemed negligence. Sio kila mara hayo makosa yanapotokea lazima mtu aadhibiwe mengine ni innocent mistakes.

Sasa huu mjadala umejaa majigambo ambayo hayana tija kwa watumiaji wa huduma ya afya ni professional rivalry inayohatarisha quality ya utoaji wa huduma na usalama wa wateja na inaonyesha there is so much medical error iwapo hakuna ushirikiano na kila mtu mjuaji.
 
Halafu mbona maduka ya dawa za mifugo na mimea hawaihaji cheti cha ADDO!? Au dawa zao hazisomewi na wafamasia!?
 
1. Sehemu ya kupewa dawa inaitwa PHARMACY. Pharmacist ndiyo amequalify kufanya kazi hapo. Clue ipo kwenye jina

2. Mambo mengi anayosoma Daktari mfamasia pia anasoma.
Physiology(jinsi mwili unafanya kazi)

Microbiology(bakteri na virusi)

Parasitology(Minyoo na parasites
wengine),

Biochemistry(chemistry ya viumbe hai)

Epidemiology(Kusambaa kwa magonjwa)
Biostastatistic(Takwimu za afya)

Anatomy(muundo wa mwili) na Pathology(magonjwa yanavyokuwa) anasoma haya kwa kiasi.

Mambo haya yanamuwezesha kufahamu magonjwa na mwili wa binadamu unavyofanya kazi.

Pharmacology(jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini). Hili anosoma kuliko daktari

3. Anasoma pia. Chemistry ya madawa, madawa ya mitishamba, jinsi ya kutengeneza dawa, jinsi ya kutunza dawa, jinsi ya kutoa dawa, na clinical pharmacology(jinsi dawa zinavyotumika hospitalini, magonjwa yanavyokuwa na matibabu yake).

So kabla ya kubishana tunapaswa kwanza kufahamu huyu mfamasia ana maarifa ya namna gani. Sijaona madaktari wengi kwenye huu uzi, wanajua jinsi ambavyo huyo Prof yupo wrong.
 
Madaktari wa bongo faka sana na wanatakiwa wawe regulated to the maximum, sitasahau kuna Dr mmoja tena Prof alinipa diagnosis fake ya kipumbavu na nusu inimalize kwa ajiri ya madawa niliyopewa kutibu ugonjwa ambao ulikuwa fake, sitasahau hilo
 
Sijui wanazungumzia mfamasia wa level gani mbona kwenye maduka ya madawa wanaogawa dawa na kuelekeza namna ya kuzitumia utakuta ni watu wa kawaida kabisa tena wengine walifaulu kwa kiwango cha chini Elimu ya kidato cha nne?

Kama daktari ndo anapendekeza dawa gani mgonjwa atumie Ili kutibu tatizo na mfamacia kazi yake ni kutoa dawa zilizopendekezwa na daktari sasa hapo Nani ni Nani?

Wafamasia mnataka kujifanya mko juu kuliko daktari huo ni uongo! Daktari anaweza kufanya kazi bila mfamasia ila mfamasia hawezi kufanya kazi kama daktari hayupo
 
Sijui wanazungumzia mfamasia wa level gani mbona kwenye maduka ya madawa wanaogawa dawa na kuelekeza namna ya kuzitumia utakuta ni watu wa kawaida kabisa tena wengine walifaulu kwa kiwango cha chini Elimu ya kidato cha nne?...
Wewe na we akili yako imedumaa..hoja hapa kila mtu asimamie taaluma yake..madaktari wa bongo wengi ni njaa tupu..wamekalia kupoka kila fursa ndani ya kada ya afya..hasa zile zenye harakati ya pesa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wewe na we akili yako imedumaa..hoja hapa kila mtu asimamie taaluma yake..madaktari wa bongo wengi ni njaa tupu..wamekalia kupoka kila fursa ndani ya kada ya afya..hasa zile zenye harakati ya pesa.

#MaendeleoHayanaChama
Kama mtu ameaomea pre nursing au nursing tena ya mwaka mmoja halafu anaweza kugawa dawa na kumuelekeza mtumiaji je kwa MD itakuwa ajabu? Kwani hata Hawa wafamasia wa kibongo wana Nini kama si kugawa dawa tu? Wamegundua au kutengeneza dawa gani? Kujifanya wakubwa wakati hata panado hawawezi kutengeneza !!! Wafamasia wa kibongo ni wagawa dawa tu hakuna jingine wanalijua
 
Sijui wanazungumzia mfamasia wa level gani mbona kwenye maduka ya madawa wanaogawa dawa na kuelekeza namna ya kuzitumia utakuta ni watu wa kawaida kabisa tena wengine walifaulu kwa kiwango cha chini Elimu ya kidato cha nne? Kama daktari ndo anapendekeza dawa gani mgonjwa atumie Ili kutibu tatizo na mfamacia kazi yake ni kutoa dawa zilizopendekezwa na daktari sasa hapo Nani ni Nani? Wafamasia mnataka kujifanya mko juu kuliko daktari huo ni uongo! Daktari anaweza kufanya kazi bila mfamasia ila mfamasia hawezi kufanya kazi kama daktari hayupo
Wewe unaweka uongo kwa sababu hujui kama ulivyojieleza hapa mwenyewe.

"Wafamasia mnataka kujifanya mko juu kuliko daktari...," Huu ni uongo. Umeona wapi famasia akitaka kuwa juu kuliko daktari? Daktari anayo kazi yake inayofahamika kisheria kabisa, na Famasia anayo kazi yake inayofahamika kisheria kabisa. Wote wamehitimu katika maeneo yao yanayowahusu. Mfamasia hawezi kwenda kudai kazi anazofanya daktari, sasa wewe kwa kutojua kwako, daktari anapotafuta kufanya kazi zinazomhusu Famasia, kwa vile hujui uwezo wa hawa wawili katika nyanja zao, hapo unachanganyikiwa na kuanza kuropoka kama ulivyofanya hapa.

Hao unaowaona wakigawa dawa kwenye maduka ya dawa, wote wanafanya kazi chini ya uangalizi wa Famasia. Ni lazima wawe chini ya uangalizi huo, ndivyo sheria inavyosema, na ndivyo taaluma ya Famasia inavyoelekeza.

Sasa basi, kama unataka daktari naye akagawe dawa, kama unadhani anaweza kufanya hivyo kama hao unaowaona watu wa kawaida kabisa ndani ya Pharmacy, basi tukubaliane, daktari wako afanye kazi hiyo chini ya usimamizi wa Famasia, maana ndivyo sheria inavyoelekeza duniani kote inapohusiana na madawa. Daktari kazi yake haihusu shughuli za madawa. Shughuli za madawa ni za Famasia. Hiyo ni taaluma nyingine, tofauti kabisa na taaluma ya udaktari, pamoja na kwamba wote wanahudumia mgonjwa, kila mmoja kwa ujuzi wake, mambo aliyoyasomea.

Sasa sijui kama utanielewa, lakini naomba usome kwa akili inayotaka kujifunza na kujua. Usisome kwa akili ambayo tayari umeielekeza katika ujuaji, kama ulivyofanya hapo juu.
 
"80% ya wapharmacia huko S.Africa alipo Professor kazi yao kubwa ni kugundua na kutengeneza dawa viwandani na hao 20% hufanya kazi hospitali (kuwasaidia ma nesi na ma MD kutunza na kusambaza dawa)" kwa madai ya Prof Koboko

"Mpharmacia hasomi kuhusu magonjwa na wadudu" kwa madai ya Professor

Hivi huko viwandani wanatengeneza vipi dawa kwaajili ya kutibu magonjwa ikiwa hawajasoma hayo magonjwa ?
;Utajuaje MECHANISM ya dawa bila kujua kisababishi/wadudu unakidhibiti vipi (?

:
 
Upo ushahidi wa wazi kabisa wa baadhi ya maduka haya ya dawa muhimu ambayo wanataaluma wenzetu (wasio wafamasia) wameyageuza kuwa Zahanati bubu kinyume kabisa kanuni zinazoruhusu uanzishaji wa maduka ya dawa muhimu unavyotaka, na ndicho anachojaribu kushauri Profesa (kama anavyojiita) kuwa maduka haya yageuzwe kuwa zahanati bubu kwa kupewa matabibu na Manesi bila kufundishwa chochote
Umefanya vizuri kutoa ufafanuzi kuhusu maduka haya ya "Dawa Muhimu."

Na kwa bahati mbaya sana, Koboko yeye katumia fursa ya udhaifu wa maduka haya kulaumu/kushutumu fani ya Famasia, jambo ambalo sasa naona halina uhusiano kabisa na maduka haya.

Lakini katika maelezo yako, inaonekana dhahiri kwamba pamekuwepo na udhaifu katika usimamizi na uendeshaji wa maduka haya. Kama yanageuzwa kufanya kazi nyingine ambazo hazikupangiwa kufanyika humo, inakuwaje chombo kinachosimamia haya maduka kisiwe na uwezo wa kuyafuta/ kuyasimamisha kufanya kazi kwa makosa yaliyofanyika? Pharmacy ikifanya ujinga huu, itaachwa iendelee kufanya kazi?

Kwa hiyo basi, inaonekana matatizo yanaanzia kwa chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia shughuli za maduka haya; kuhakikisha kwamba hayakiuki taratibu yaliyopewa na shughuli yaliyopangiwa kuzitekeleza.

Baraza la Famasia wamejikokea wenyewe moto utakaowaunguza.
 
"80% ya wapharmacia huko S.Africa alipo Professor kazi yao kubwa ni kugundua na kutengeneza dawa viwandani na hao 20% hufanya kazi hospitali (kuwasaidia ma nesi na ma MD kutunza na kusambaza dawa)" kwa madai ya Prof Koboko...
Anyanganywe huu uprofesa wake wa mchongo...andiko hili limemuacha uchi sana.
 
Kwako Mh. Waziri wa Afya wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Ndugu Ummy Mwalimu.

Kwanza pole kwa kazi nzito unayoifanya yakusimamia wizara nyeti na ngumu yenye wataalam wengi wenye weledi, kadhia, hamu na kamu katika kuleta maendeleo chanya hususan katika sector ya Afya.

Mh. Waziri mimi ninayeandika makala hii ni mtaaluma wa fani zote mbili ambazo huleta mvutano usio na tija katika taifa letu, nina Diploma in Pharmaceutical science na Bachelor of medicine and surgery zote kutoka Oslo School of medicine nchini Norway.

Nasikitika kusema kwamba hali ya utendaji kazi katika sector ya afya inaharibiwa na watu wenye academical fallacy and abuse, watu hawa hujiona kuwa vyeti wanavyomiliki vinawapa dhima yakubeba dunia nzima katika mifuko yao wanayoweka shilingi, hali hii huleta utengano na hali ya kudharauliana katika taaluma walizopo, hii haipo tu katika kada ya afya bali katika fani zote zinazohisika na utendaji kazi kwa kutumia taaluma.

Nimesikitishwa na mtu anayejiita professor huku akijitwika vyeo kama mmed and PhD, akisahau kuwa anaaibisha wataaluma nguli katika sekta ya afya wenye wadhifa kama huu mathalani Prof. Sarungi ambaye amefanya mambo mengi mazuri katika wizara ya Afya.

Nilipojaribu kuingia katika mtandao wetu wa medical council of Tanganyika kumtafuta mwanataaluma huyu sikuweza kupata taharifa zake katika database ya baraza letu, ndipo nilipojua kuwa huyu ni kijana wa hovyo ambaye atakuja kuingia kwenye kundi la wataaluma wenye academical fallacy and ignorance kwa spidi ya 4g, kwa uelewa wake mdogo wakuchanganua mambo nimeona kabisa huyu ni mwanafunzi tena wa mwaka wa kwanza semester ya Kwanza Aliyegusa gusa human anatomy and physiology na kuanza kuona ameshamaliza taaluma nzima ya afya, ambaye hajui hata umuhimu wa team work katika kumuhudumia mgonjwa hospitalini.

Akishindwa hata kujua kuna kitu kinaitwa University prospectus ambacho kingemsaidi kujua anachokisoma mtaaluma mwingine kina mwingiliano gani na yeye, anashindwa hata kutambua kuwa hata wafanyakazi wa hospital wasio na utaalam wa tiba hupewa mafunzo juu ya magonjwa, dalili zake na namna ya kujikinga awapo katika mazingira yake ya kazi, leo hii anatoka kijana mmoja wa hovyo nakuandika kuwa mwanataaluma aliyefunzwa kwa miaka 5 hajui magonjwa na dalili zake? Hii ni hatari sana na academical fallacy ni ugonjwa unaotafuna wengi.

Katika pitapita zangu nikakutana na andiko la ndugu Yoshua nguyahambi aliyejishusha kuwa darasa la saba B ilihali kwa aliyoeleza inahakisi yeye ni mtaaluma anayejua anachokifanya napenda kuchangisha andiko lake na uzi wangu ili kuweza kusediment ujumbe wangu kama ifuatayo;

Yoshua Nguyahambi, Darasa la Saba B

Ndugu zangu nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nimeisoma kwa makini Makala ndefu ya mtu anayejiita Prof. Patrick Koboko, nashawishika kukiri wazi kwamba Profesa (Kama anavyojiita) amefanya upotoshaji wa makusudi kwa mhe. Waziri wa Afya na Umma wa watanzania kuhusu Addo na taaluma ya ufamasia.

Kwanza, katika makala yake amedai kazi ya mfamasia ni Kutunza na kuifadhi dawa, kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa, ameenda mbele zaidi na kusema kazi ya mfamasia siyo drug administration eti hii ni kazi ya watu wengine, ameendelea kudai kwamba mfamasia hajasomea magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi na hajasomea dalili za magonjwa, huu ni upotoshaji wa kijinga na makusudi kabisa uliofanywa na mtu wa ngazi ya uprofesa, angekuwa kwenye nchi za wenzetu angeshaitwa na kunyang'anywa uprofesa mara moja!

Hivi katika akili ya kawaida tu ya la saba B, kama yangu, mtu anaweza kukutengezea dawa kiwandani kama alivyodai anayejiita profesa, bila kujua issue za drug administration, epidemology, Anatomy, Physiology, Parasitology, Pathology, Medical semiology, medical toxicology, microbiology, biochemistry, Parasitology? Yaani mtu akutengenezee Paracetamol na asijue namna ya kuitoa kwa mgonjwa? Anasahau kabisa wao (wafamasia) watengenezaji wa dawa ndio wanawaandalia leflet zinazoonyesha namna dawa inavyopaswa kutumika, athari zake, n.k. Profesa wakati unaandaa makala hii ulikuwa wapi? Au ulikuwa na hangover ya K-vant?. Wakati mwingine tunapoamua kuandika makala sensitive na zinazogusa moja kwa moja Umma wa watanzania tusisukumwe na jicho la wivu, husda na kijino pembe kwa taaluma za wengine.

Profesa Patrick Koboko MD, MMED,PhD(kama anavyojiita) amenifanya mimi darasa la saba B nirudi kuangalia tena Prospectus ya vyuo vinavyotoa course za ufamasia, kuangalia je madai yake aliyoyatoa kuhusu wa wafamasia yana ukweli? Ni halali? Mathalan ukisoma prospectus ya chuo kikuu cha Muhimbili ya 2019/2020 – 2020/2021 ukurasa wa 75, kuna maneno yasomeka hivi, nanukuu "Pharmacy education embraces the search, development, formulation, analysis, storage and distribution of products for maintenance and restoration of good health as well as provision of information and guidance on proper use of medicines."

Sio kazi yangu darasa la saba B kumtafsiria maneno hayo, lakini ni wazi kuwa wafamasia ndio wanataaluma pekee wanaondaliwa sio tu kwajili ya yale aliyosema, wafamasia wanapaswa kuyafanya lakini pia kwajili ya kulea na kutoa taarifa sahihi za matumizi sahihi ya dawa, Prof. Koboko (kama anavyojiita) alipaswa alijue hili mapema hata kabla hajafikiria kuandika makala yake.

Kwahiyo kama darasa la saba B nampa home work profesa Koboko (kama anavyojiita) aende aipitie tena Prospectus ya Muhimbili na vyuo vingine vinavyo offer digrii ya ufamasia, aangalie vizuri kwa kulinganisha na hizo taaluma nyingine ni wapi kwenye Prospectus hizo mfamasia haandaliwi kutoa dawa kwa mgonjwa?

Litakuwa kosa kubwa la karne kama usimamizi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vitaondolewa kwenye mikono ya wafamasia kwa maana ya Baraza la famasi, kwasababu ya ushauri wa ki husda na kijino pembe ulitolewa na huyo anayeitwa Profesa, kwa sababu kwa mfumo wa elimu ya Tanzania ni wafamasia pekee ndio wameandaliwa kwa jukumu hilo. Profesa kama anavyojiita alipaswa kulifahamu hili.

KUHUSU ADDO.

Arudi aangalie vizuri kwanini wizara ya afya iliamua kuanzisha mafunzo hayo, ingawa ni kweli kuna mapungufu lkn haiondoi nia njema ya Serikali kupitia wizara ya Afya iliyoamua kuanzisha mafunzo hayo, ambapo awali yalikuwa chini ya TFDA sasa hivi TMDA, na baadae uratibu wake ukahamishiwa baraza la famasi kwasababu wao ndio wadau & walezi sahihi wa mambo yote yanahusiana na dawa, vifaa tiba na vitendanishi

Upo ushahidi wa wazi kabisa wa baadhi ya maduka haya ya dawa muhimu ambayo wanataaluma wenzetu (wasio wafamasia) wameyageuza kuwa Zahanati bubu kinyume kabisa kanuni zinazoruhusu uanzishaji wa maduka ya dawa muhimu unavyotaka, na ndicho anachojaribu kushauri Profesa (kama anavyojiita) kuwa maduka haya yageuzwe kuwa zahanati bubu kwa kupewa matabibu na Manesi bila kufundishwa chochote kuhusu malengo ya uanzishwaji ya maduka haya, kama nilivyosema awali litakuwa kosa kubwa la karne kuupokea ushauri huo bila kuzingatia ukweli niliouanisha kwenye makala yangu" mwisho wa andiko la Yoshua.

Ni rahi yangu kwa madaktari wote nchini kutambua, kuheshimu na kuthamini uwepo wa kila mmoja wetu katika sekta ya Afya, sisi hatuna authority yeyote yakushusha, kutweza na kubagaza taaluma zingine, nichelee kusema kwamba kwa sasa kipindi ambacho niko masomoni (Resident 2) wafamasia wamekuwa msaada mkubwa kwangu especially katika kufahamu dawa za aina mbalimbali hata zile ambazo haziko katika scope ya masomo yangu, ndugu hawa wako honest sana na wengi hupenda kurejea katika maandiko "books or publication" incase akihisi kitu hana uhakika nacho hali ambayo ni tofauti kwetu sisi madaktari ambapo uhusi kufanya hivyo ni kujishusha thamani na kuonekana HUJUI, nimepractice nchini Sweden na nakiri kusema hali ni tofauti Sana ukilinganisha na nchini kwangu, sikuwahi kusikia mvutano wakitaaluma katika nchi yoyote huku ulaya wala marekani na wao ndio chachu ya mifumo hii ya afya, sembuse sisi tuliopokea kama mapokeo..ni Aibu lakini ndio uhalisia.

Mwisho kabisa nachukua fursa hii kuwataka radhi wafamasia wote waliokerwa na andiko lile, niwatie moyo kufanya kazi kwa weledi kutokana na maadili ya kazi yenu, mchango wenu ni wamuhimu katika sekta ya afya, mnatusahihisha na mengi sana especially drug interactions and drug overdose kwa hili siwezi ficha mnatusaidia sana.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki taaluma ya Afya nchi Tanzania.

Doctor junior
Resident in internal medicine.
 
Dawa zao hazisomewi na wafamasia.
Mfamasia ana idea pia kuhusu dawa za mifugo , maana dawa nyingi zinafanana tofauti ni pharmacokinetics parameters ndio zinakuwa tofauti kidogo , sijajua kwenye mitaala ya kitanzania kwa wenzetu huwa wanasoma pia veterinary pharmacology semester 1 au 2.
 
Sijui wanazungumzia mfamasia wa level gani mbona kwenye maduka ya madawa wanaogawa dawa na kuelekeza namna ya kuzitumia utakuta ni watu wa kawaida kabisa tena wengine walifaulu kwa kiwango cha chini Elimu ya kidato cha nne? Kama daktari ndo anapendekeza dawa gani mgonjwa atumie Ili kutibu tatizo na mfamacia kazi yake ni kutoa dawa zilizopendekezwa na daktari sasa hapo Nani ni Nani? Wafamasia mnataka kujifanya mko juu kuliko daktari huo ni uongo! Daktari anaweza kufanya kazi bila mfamasia ila mfamasia hawezi kufanya kazi kama daktari hayupo
Pharmacist (mfamasia) ni Degree holder

Pharmaceutical Technician (Fundi dawa sanifu) Huyu Ni Diploma

Pharmaceutical Assistant (Fundi dawa sanifu msaidizi) Huyu ni Certificate

Dispenser (Huyu Ni mtoa dawa ila yupo chini ya Fundi dawa sanifu msaidizi)

Hao unaowaona wanakupa dawa kwenye pharmacy si phao labda ubahatike kukutana nae, pharmacist Kazi yake ni kusimamia shughuli zote za uendeshaji pharmacy na kuangalia competent ya hao wanaotoa huduma kwenye pharmacy Kwa wagonjwa....

Pharmacist ndio msimamizi mkuu wa pharmacy yeyote ndo maana Cheti chake hutumika kusajili pharmacy

Note: Wabongo tumezoea kila anaetoa dawa tunamuita mfamasia, au ukienda hospitalini kila alievaa Koti Muna Muita Dokta ila sivyo hivyo....

Nawasilisha hoja
 
Da
WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!
Daktari upo wapi?
Kunywa chochote nitalipa.
Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom