Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Sasa bruh kuliko kuponda mtu ungejibu hoja yake kwa hoja kama kuna mahali hapako sawa paweke vizur paeleweke maaana hapa ina mwatack bila hoja,hoja hujibiwa kwa hojaaa na wewe weka kazi ya mfamasia daktar na nesi tujue yupi ni yupi
 
Walimu wenyewe ndiyo hawa wabovu hakuna jipya
 
Sasa bruh kuliko kuponda mtu ungejibu hoja yake kwa hoja kama kuna mahali hapako sawa paweke vizur paeleweke maaana hapa ina mwatack bila hoja,hoja hujibiwa kwa hojaaa na wewe weka kazi ya mfamasia daktar na nesi tujue yupi ni yupi
Fact
 
Mungu amlaze mahala pema
 
MIMI NI MDAU WA ADDO TANGU MWAKA 1995 NA NAOMBA NICHANGIE KAMA IFUATAVYO:

HISTORIA:
Private/illegal outlet kwa dawa za binadamu imekuwepo kwa miaka mingi lakini ilishamiri zaidi mwaka 1978/79 wakati wa mlipuko wa kipindupindu ambapo Tetracycline ilionekana kama dawa ya maajabu makubwa. Dawa hizi zilitoka katika mikono rasmi na kuanza kuuzwa katika maduka ya kawaida (dukawala).Baadae tukaingia katika mdororo wa kiuchumi na kwa wale wanaokumbuka upungufu mkubwa dawa ulionekana kila mahali na watu walihamia mpaka kwenye muarobaini.

Maduka ya dawa muhimu: Uanzishwaji wa maduka muhimu ulikuwa na lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi kwa dawa za kawaida na jambo hili lilifanikiwa sana.Utararibu uliwekwa kwa kuwapa mafunzo wamiliki,watoa na dawa na baadhi ya sehemu vilianzishwa vyama vya webey maduka haya katika jitihada za kujisimimamia na kupeana taarifa mhumi.

Mafanikio:Mafanikio ni makubwa sana na mojawapo lilikuwa ni kuruhusu upimaji wa malaria katika maduka haya kwa kutumia rapid diagnostic test nah ii ilianza kuwapa imani wananchi na wengi wameanza kuacha kutumia kiholela dawa za malaria.Kuna sehemu ambazo wamefundishwa KUIBUA wagonjwa wanaohisiwa kuwa na TB.

Changamoto:Kama ilivyo kwa mambo yote yanayotengenezwa na binadamu changamoto hazikosekani na mimi nazigawa katika makundi mawili,

  • Changamoto kutoka kwa mamlaka:Haijulikani wazi nini kilitokea lakini ADDO ilitolewa TFDA na kupelekwa Baraza la Famasia.Barasa la Famasia ADDO imekuwa ni mradi wa kuingizia pesa.Mafunzo ya ADDO yameanza kugubikwa na ukiritimba mkubwa na usimamizi wa ADDO umekuwa si wa kuboresha.Mamlaka washirika wa Baraza la wafamasia katika ngazi za chini wameshindwa kusimamia hata umbali kati ya duka na duka na wametoa vibali visivyo rasmi kiasi ambacho kila mtu anafungua atakavyo.Jambo la pili ni kuwa ukipitia orodha inayoruhusiwa dawa kuuzwa katika haya maduka unaona wazi ya kuwa inashawishi watu kuuza visivyohusika.Orodha iliyopo haiendani na ada za Baraza,liseni na hata makadirio ya kodi.NI WAZI wanaelewa ya kuwa maduka yanauza visivyostahili ndio maana wana uwezo wa kulipa ada hizo.
  • Changamoto toka kwa wamiliki:Wamiliki karibu wote wameingia katika kuuza dawa ambazo haziruhusiwi.Maduka haya yanaendeshwa pia na watu ambao hata mafunzo ya awali hawana.
SULUHISHO:Haya maduka ni muhimu sana kwa sehemu za vijijini ikiwa yataendeshwa na kusimamiwa ipasavyo.Kupunguza idadi ya dawa zinazoruhusiwa wakati dawa hizo hazipatikani katika hospitali/zahanati za serikali kutawaumiza wananchi na pia kutafungua magendo ambayo yatakuwa hatari zaidi.Wadau wakae na kujadili umiliki na uendeshaji na kipengele cha kuzuia watu wenye fani kuuza dawa hizo mpka wakasome ADDO si sahihi.Wanaweza kuweka mtihani wa kulipia na anayetaka afanye mtihani huo na apewe cheti kuliko hiki kinachofanyika leo.

Serikali inaweza kuua biashara hii ya kuanzisha BIMA kwa kila Mwanachi na kuhakikisha ya kuwa vituo hasa vya serikali vinakuwa na dawa zote muhimu (Mengi yatajifia tu).

Jambo la tatu ni kuwa mfumo wetu wa kiutawala unakwenda hadi ngazi ya mtaa/kitongoji.Mfumo utumike kwa ufanisi katika kuanzisha na kuyasimamia haya maduka.Ni ajabu kuna serikali ya mtaa/kitongoji lakini inaanzishwa biashara isiyokuwa na vigezo!!
 
"Professor" naona hauna mtaala wa kozi ya Ufamasia katika makarabrasha yako!! Ufamasia ni zaidi ya ulivyoelezea hapo.

General Pathology
Anatomy
Physiology
Biochemistry
Microbiology
Basic Pharmacology

Hizo course hapo juu vyuo vingi kwa semester 2 au 3 za mwanzo huwa zinatolewa kwa wanafunzi wote wanaosoma udaktari na Ufamasia na zote zina maudhui ya kumpa mtu msingi wa maarifa kuhusiana na mwili wa binadamu na magonjwa.

Ni ajabu kusema kuwa Mfamasia hajui dalili zozote za magonjwa ya binadamu na wala hawezi kujua chochote kuhusu uhusiano wa dawa na ugonjwa husika.

"Professor" katika kada ya afya kuna majukumu na miiko na kila Mwana taaluma wa afya anatakiwa kuheshimu. Daktari, mfamasia, nesi, mtu wa maabara, wataalamu wa mionzi na hata watu wa physiotherapy wote hao wanapaswa kushirikiana na kila mtu atimize majukumu yake ili kuweza kutoa huduma bora.

Zama za kulazimisha majukumu ya kada fulani yabaki kwa kada isiyo husika zimepita. Nchi yetu kwa sasa kuna wataalamu wa afya wengi wanazalishwa kila uchao na Waziri ametoa Takwimu bungeni kwa kada ya Famasi ambayo ndio ina wajibu wa Kusimamia mambo yote yanayohusu Dawa na vifaa tiba.
 
CCM NI MAFII
 
Umemaliza mkuu, mh waziri pitia hapa
 
Nimesoma andiko ,liko vizuri tu, sema tu matusi ndo yamejaa watu, alafu hoja hujibiwa KWa hoja sio matusi,ana laana uyo achana nae mkuu
 
Huna uwezo Wa kusoma pharmaceutics, Industrial pharmacy,medicinal chemistry,pharmacognosy, vingi Tu husomi.....


Na hizi ndio core subjects Kwa pharmacy
 
Acha kudanganya watu wewe, huwezi kusoma Mpharm yoyote bila Bpharm. Phamacy sio pharmacology tu, kuna kozi nyingi zinahusiana na dawa ambazo wewe huzijui. Hata ukiulizwa kwanini dawa X ni 8 hourly na sio 12hourly au 24hourly huwezi kujibu halafu unataka uwe sawa na pharmacist.

Kazi inatakiwa zifanywe kwa ushirikiano na sio kada moja kutaka kufanya kazi za kada nyingine. Hivi inaingia akilini kweli wewe kitu usome semester 2 tena juujuu tu halafu uwe sawa na mtu aliyesoma 4 good years?.

Kabla hujajitetea nakukumbusha masters ya pharmacology ni Msc na sio Mpharm kama medicinal chemistry, pharmaceutics, pharmacognosy, n.k.

Wenzetu wameadvance mpaka kuanzisha Doctor of pharmacy ili kuongeza wigo wa pharmacist kuongeza wigo wa mfamasia kutoa huduma za kitaalamu. Huku madongo kuinama Md's wanataka waruhusiwe kufanya kazi za mfamasia, PATHETIC
 
Huyu professor hajui haya carriculum ya pharmacist ipoje.....

Anatia Aibu tuu
 
Nimesoma andiko ,liko vizuri tu, sema tu matusi ndo yamejaa watu, alafu hoja hujibiwa KWa hoja sio matusi,ana laana uyo achana nae mkuu
Tatizo mleta hoja pamoja na elimu yake kubwa lakini hajui majukumu ya msingi ya pharmacist na hata mtaala wa pharmacy haujui.
 
Tatizo mleta hoja pamoja na elimu yake kubwa lakini hajui majukumu ya msingi ya pharmacist na hata mtaala wa pharmacy haujui.

Kwa kuwa ametaja majina yake kamili, natamani mmoja athibitishe uwepo wa profesa huyu na eneo lake la kazi…. binafsi nachelea kusema ni mtu fulani tu kajivisha hizo shahada.
 
Huyu professor hajui haya carriculum ya pharmacist ipoje.....

Anatia Aibu tuu

Ni mpuuzi mmoja huyu wa kupuuzwa tu, huenda alikuwa na hoja nzuri ila imenajisiwa na uwasilishaji wake.

Unajiita profesa na hujui kuwa tunaweza kujua kama una-exist na hata kwa publications zako kwenye google domain?

Heshimu taaluma za watu, toa maoni yako kama raia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…