Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

"Professor" naona hauna mtaala wa kozi ya Ufamasia katika makarabrasha yako!! Ufamasia ni zaidi ya ulivyoelezea hapo.

General Pathology
Anatomy
Physiology
Biochemistry
Microbiology
Basic Pharmacology

Hizo course hapo juu vyuo vingi kwa semester 2 au 3 za mwanzo huwa zinatolewa kwa wanafunzi wote wanaosoma udaktari na Ufamasia na zote zina maudhui ya kumpa mtu msingi wa maarifa kuhusiana na mwili wa binadamu na magonjwa.

Ni ajabu kusema kuwa Mfamasia hajui dalili zozote za magonjwa ya binadamu na wala hawezi kujua chochote kuhusu uhusiano wa dawa na ugonjwa husika.

"Professor" katika kada ya afya kuna majukumu na miiko na kila Mwana taaluma wa afya anatakiwa kuheshimu. Daktari, mfamasia, nesi, mtu wa maabara, wataalamu wa mionzi na hata watu wa physiotherapy wote hao wanapaswa kushirikiana na kila mtu atimize majukumu yake ili kuweza kutoa huduma bora.

Zama za kulazimisha majukumu ya kada fulani yabaki kwa kada isiyo husika zimepita. Nchi yetu kwa sasa kuna wataalamu wa afya wengi wanazalishwa kila uchao na Waziri ametoa Takwimu bungeni kwa kada ya Famasi ambayo ndio ina wajibu wa Kusimamia mambo yote yanayohusu Dawa na vifaa tiba.
Naomba nikuulize kitu, katika hayo yote sijaona umeandika Pathophysiology. Kama hukusoma Pathophysiology, utasemaje unaweza kugundua dalili za magonjwa?


Kazi Diagnosis ya Mgonjwa ni ya daktari usitake kupoteza muda kwa ubishi hapa ndugu. Kazi ya Mfamasia kutoa dawa from the store or dispensing room kwa maelekezo ya daktari. Kama Doctor's prescription unatoaje dawa?
 
Umejikita kumkosoa prof bila kupiga hoja zake

Mi sio mtu wa afya ila nilitaman kupata ukweli kuhusu machache ambayo prof ameaninisha
1. Mfamasia hasomei kuhusu magonjwa chanzo na dalili zake je ni kweli? Na kama kweli

Basi mfamasia hawezi kuwa mtu sahihi hapo

Maana ni ukweli nurse anasomea hayo na dr wake

Hoja hii binafs nahitaji majibu yake
Asante mtaalamu

Usipojua ugonjwa utatoaje dawa? Ugonjwa utaujua kulingana na dalili kwa kuthibitisha na vipimo.

Kwa mantiki hiyo Mfamasia hajasoma magonjwa na dalili zake?

Kwako Prof Koboko
 
Ooooh!
Huyu ni dokta na Profesa, kweli?

Nchi yetu hii imepoptea kweli kweli.
Hajui Famasia kazi yake ni nini, na wala hajui kwamba kuna sheria kabisa inayotambua kazi ya Famasia duniani kote?

Andiko lote toka mwanzo halionyeshi kuwa huyu ni mtaalam kama inavyoonyesha katika utambulisho wake, MD, Ph.D. n.k.
Ni kama andiko la mtu ambaye kamaliza kidato cha nne? Leo hii anatafuta kujitambulisha kwa waziri naye awe mshauri wa waziri?

Dr Koboko, kama wewe kweli ni daktari, udaktari wako ni wa shaka sana, na huo uProfesa unaojitangaza nao sijui umeupata wapi kama hata hujui kazi za mtaalam ambaye unapaswa kushirikiana naye wakati wa kumhudumia mgonjwa. Kama umesomea Muhimbili, kuna chuo cha maFamaciia hapo hapo na wote mpo chuoni hapo, utashindwa hata kudadisi na kujua famaciia anasoma nini?

Unasema "administration of drugs" hiyo ni kazi ya daktari? Na huko kumpa mgonjwa dawa, ina maana wagonjwa wote wapo hospitalini wamelazwa wakisubiri kupewa dawa wakiwa mahtuti?

Hujui sehemu nyingine nyingi ambako dawa nyingi zaidi hutolewa bila uwepo wa nesi wala daktari?

Hata historia ya hizi taaluma huijui ilikotokea?
Usitafute sifa! Huyu mwandishi yuko sahihi kabisa! Siyo kazi ya mfamasia kugawa dawa kwenye maduka na vidirisha. Hiyo ni fact na iko wazi. Mfamasia hawezi kuwa na kazi ya kutoa dawa kwa wagonjwa mitaani, halafu hospitalini hahusiki. Mfamasia hawezi kutoa dawa za vidonge tu, sindano iwe ni kazi ya nesi. Hiyo ni kujichanganya na kutafuta pesa mitaani ikiwa ni hatari kwa wagonjwa.

Wafamasia fanyeni kazi za kuchanganya madawa na kutafuta dawa mpya za magonjwa na kuzitengeneza. Kama hamuwezi kutengeneza dawa, ninyi ni bure kabisa!!!! Wafamasia kutoa dawa ni kudandia kazi isiyowahusu.
 
Leave the drug to the pharmacist...!! Sasa mtu anataka Dr akakae pharmacy kisa tu amesoma pharmacology semister 2...[emoji28][emoji28] sisi tunasoma mpaka Infusion rate...incase kuna toxicity what to do kucalculate dose sahihi incase lower dose inahitajika than available dose.. Leo mtoto ana haeart failure anaandikiwa digoxin 0.0625mg lakini kuna kidonge cha 0.5mg hapo Dr kacalculate tu ila sasa unapataje hiyo dawa digoxin 0.0625mg??? Hapo ndo tunarudi kwenye suala la why mfamasia ni muhimu... Mahospitalini siku hizi Polypharmacy imejaa mtu anamanage PUD na Malaria mgonjwa anaandikiwa dawa karibu 7 hukoo mfamasi ukiwa kilazaa utataoa tu dawa hapo tunasema mfamasia kazi yake sio kutoa Dawaaa tu mfamasia ana majukumu mengi yahusuyo dawa mabapo hakuna namna Dr anaweza yatekelezaa... Management ya magonjwa mengi ni changamoto na wagonjwa hawaponi japo wanatumia pesa nyingi kununua madawa sababu Dr anajiona anajua kila kitu. Mgonjwa anaweza kuja famasi na prescription ina list ya dawa karibu 7 au unakuta ni Mtoto ila Dr dawa alizomuandikia unabaki kushangaaa.. Haya yote hayawezi kukoma kama dr anadhani anajua dawa vizuri kuliko mfamasia
Kwa hiki ulichoeleza hapa upo sahihi, kwa knowledge ya pharamacology ya daktari hawezi kujigamba kwamba anajua complexities zote zinazohusu dawa ikiwemo kiwango na namna inavyopaswa kutolewa na any variations zinazoweza kujitokeza.

na pia kama ulivyoeleza kuna swala la drug interactions ambapo dakatari anaweza kuandika mchanganyiko wa dawa ambao wewe pharmacist kwa uelewa mpana ulio nao ukaona amefanya kituko.

Kwa hiyo naunga mkono hoja kwamba kila mmoja atambue na kufanya majukumu yake kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi badala ya kushadidia vitu ambavyo una uelewa wa juu juu tu au ule wa kawaida.
 
WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
Huyu pimbi hana adabu kaandika utumbo mtupu mbona anawivu sana na wafamasia huyu kibwengo, asilete uchawi ana akili za kikuda kidwanzi mtopolo.

MD wanachuki, dharau na wivu kwa wafamasia. Ummy wakazie hawa vibwetere uchwara songa mbele wape nafasi wafamasia watumike ipasavyo
 
Bora wameifuta hiyo ADDO maana haingii akilini eti MD haruhusiw kuuza dawa mpaka awe na cheti cha ADDO wakat pharmacology yote ipo kichwan,tena mbaya Zaid unakuta Baadhi ya watu wanaopewa hiyo ADDO wengine ni form 4 failures.
Wizara ya Afya imekaa kishenzi tu! Nasema hivyo kwa sababu ya majivuno ya kitaaluma waliyonayo ambayo yanasababisha wote ndani ya taaluma ya afya kudharauliana. Ni tangu hospitalini hadi wizarani wana maisha ya kishenzi, na ndo maana hatufiki mbali ktk huduma za Afya.

Ukiwa hospitali, daktari, nesi, mfamasia wote ni maringo ya kujiona ni bora kuliko mwingine. Sooo stupid characters. Mbona upuuzi huu hatuuoni ktk nchi zilizoendelea? Wizarani pia ni hayo hayo! Hata wakipelekewa waziri asiye daktari wanaona kama imekosewa. Miaka mingi walipewa madaktari wakaishia kuiba pesa na kuleta chanjo feki!
 
Hiii ligi ya Pharmacy Vs MD +Nursing huwa haiishi ....!! Wafamasia huwa hawataki kukubali kuwa MD yupo juu ya yote, mtu mwenye Bachelor ya Medicine doctor kwenye masters anaweza chepukia course karbia zote za Pharmacy, Ila mtu mwenye Bachelor of Pharmacy yupo limited Sana kuchepukia course za MD
Hiyo hoja hakuna inayomfanya superior! Kila taaluma ni muhimu na hizo taaluma zinategemeana! Hakuna anayeweza kusimama bila mwingine.
 
Leave the drug to the pharmacist...!! Sasa mtu anataka Dr akakae pharmacy kisa tu amesoma pharmacology semister 2...[emoji28][emoji28] sisi tunasoma mpaka Infusion rate...incase kuna toxicity what to do kucalculate dose sahihi incase lower dose inahitajika than available dose.. Leo mtoto ana haeart failure anaandikiwa digoxin 0.0625mg lakini kuna kidonge cha 0.5mg hapo Dr kacalculate tu ila sasa unapataje hiyo dawa digoxin 0.0625mg??? Hapo ndo tunarudi kwenye suala la why mfamasia ni muhimu... Mahospitalini siku hizi Polypharmacy imejaa mtu anamanage PUD na Malaria mgonjwa anaandikiwa dawa karibu 7 hukoo mfamasi ukiwa kilazaa utataoa tu dawa hapo tunasema mfamasia kazi yake sio kutoa Dawaaa tu mfamasia ana majukumu mengi yahusuyo dawa mabapo hakuna namna Dr anaweza yatekelezaa... Management ya magonjwa mengi ni changamoto na wagonjwa hawaponi japo wanatumia pesa nyingi kununua madawa sababu Dr anajiona anajua kila kitu. Mgonjwa anaweza kuja famasi na prescription ina list ya dawa karibu 7 au unakuta ni Mtoto ila Dr dawa alizomuandikia unabaki kushangaaa.. Haya yote hayawezi kukoma kama dr anadhani anajua dawa vizuri kuliko mfamasia
Stereotype na wivu wa MDs ni upumbavu wanawivu sana na sasa hivi ndio wanatumika kuua watanzania kwa kuwandikia madawa ya kuwaua ili tu stock za dawa ziishe, nina hasira na hawa MD wanaandikia watu dawa ili ziwaue nenda private hospitals huko wanaua sana watu na hii NHIF ndio hatari wanakomoa ili wapate pesa nyingi wanatoa dawa za kuua na kuwapa ukilema watu, katika watu hawana huruma na vifo ni hawa MD. Waziri Ummy komesha huu uchuro wa MDs ni wachawi wa afya zetu.
 
Wizara ya Afya imekaa kishenzi tu! Nasema hivyo kwa sababu ya majivuno ya kitaaluma waliyonayo ambayo yanasababisha wote ndani ya taaluma ya afya kudharauliana. Ni tangu hospitalini hadi wizarani wana maisha ya kishenzi, na ndo maana hatufiki mbali ktk huduma za Afya.

Ukiwa hospitali, daktari, nesi, mfamasia wote ni maringo ya kujiona ni bora kuliko mwingine. Sooo stupid characters. Mbona upuuzi huu hatuuoni ktk nchi zilizoendelea? Wizarani pia ni hayo hayo! Hata wakipoelekewa waziri asiye daktari wanaona kama imekosewa. Miaka mingiu walipewa madaktari wakaishia kuiba pesa na kuleta chanjo feki!
Kuna uzi humu umeongelea mfumo madaktari katika sekta ya afya unaua sekta ya afya..na hichi ndicho kanichoonekana.

Hao jamaa wamechangia sana kuua sekta ya afya nchini..wengi sasa wamebakiza kuhodhi madaraka na ila hawa output yoyote ya maana.

Mfumo wa afya ubadilishwe..tofauti na hapa kila siku ni business as usual tu...kutoka kwa hawa incompetent MDs

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujamuelewa Pro. Koboko.
Yeye yupo Sahihi,

Tabibu ikiwa yeye ndiye anafanya Diagnosis Kwa magonjwa, kisha baada ya majibu kutoka maabara anamuandikia Dawa, iweje azuiewe kuuza Duka la dawa au kuwa na Famasi?

Tabibu amesoma kozi ya Pharmacology iweje mpaka apewe kozi nyingine ya ADDO Ndipo aruhusiwe kuuza kwenye Duka la Dawa au Famasi?

Unajua MD Kwa sehemu kubwa anaweza kufanya kazi ya Mfamasia lakini mfamasia hawezi kufanya kazi za MD?
Unajua Kazi za pharmacist wewe???....

Kitu kidogo kama compounding hajui hayo Mambo mengine atajua
 
Sasa mkuu, pharmacist anachotakiwa ni kuhifadhi dawa au kubainisha aina ya dawa na kuitoa kwa mgonjwa? maana haya mambo sasa yanaanza kuleta msigano.
MDs ni washenzi na wivu wao wa kichawi hawana lolote.
 
Wewe bwana mimi ni Mtanzania ninayeishi South Africa, nimesajiliwa huku ingawa nafundisha madaktari and soon nitaanza kufundisha huko na pia Tanzania namiliki hospitali. Wanaonijua wapo humu humu hawaongei.

Shut up!!
Kwenye hicho chuo unachofundisha hamna kozi ya Famasi?

Kama ipo fanya utafiti wa mtaala wake ili ujue Wafamasia waajifunza nini, halafu uje uweke kipengele hicho kwenye bandiko lako.

Hospital yako inaitwaje? nipe kazi basi hapo
 
Kwanza kabisa pamoja kubeza elimu yangu na kunitukana sana, nikiri kusema tu kwamba Wafamasia nchini Tanzania ni MZIGO KWA TAIFA.
Sijajua wanaobisha humu ni wafamasia kweli au wengine ni Mafundi sanifu wa dawa na Dispensers ambao kimsingi mjadala huu is beyond their capacities.

NISIKIKIZENI KWA UFUPI PENFINGINE HAMSOMI ANDIKO LANGU LOTE.
Nimesema hivi.......

1.Pamoja na kwamba wafamasia wanasoma anatomy,microbiology, Physiology nk, hivi ni basic knowledge pale wanapotakiwa kusoma therapeutics, mechanisms of actins za dawa kwa wadudu mwilini. Hii siyo knowledge ya kumfanya Mfamasia ajue mgonjwa anaumwa nini, yeye siyo daktari anayeweza kufanya Diagnosis.

2.Nimesema kwa nchi za Wenzetu hata hapa SA 80% of pharmacists wako viwandani kutengeneza dawa na wengine kwenye Godowns za kuhifadhia dawa and rest of them 20% wako mahospitali kusaidiana na madaktari kwenye kufadhi na kutoa dawa. Kwakua Tanzania hatuna viwanda vya vya kutosha vya kutengeneza, Wafamasia wengi hawana kazi wapo kwa ajili ya kuuza vyeti vyao kwa wale wanaotaka kufungua madawa, hata hizi ADDO ni kwa sababu wengi hawana kazi za kufanya wanatafuta kupiga tu pesa. Wanapoona nesi au daktari ana kufika cha dawa basi wanachanganyikiwa na kupanic wanaona kama wanaporwa ulaji wao.

3.Nimesema kua kazi ya Daktari ni kusoma magonjwa na kuyabaini, anasoma Pathophysiology jinsi ugonjwa unavyoingia na kuenea mwilini kwa dalili pamoja na kutibu either kwa dawa au Upasuaji. Sawa unaposema Mfamasia atoe dawa kwa mgonjwa moja kwa moja bila cheti cha daktari l, amesomea wapi magonjwa na dalili zake? Anatomy and physiology ndio zinawafanya waweze kutibu?
-Mfamasia anaweza hata kuchoma sindano?
-Mfamasia anaweza kupasua hata jipu na anajua baada ya upasuaji ni dawa gani itolewe?
-Nesi yupo zaidi kwenye kutoa dawa na uangalizi wa mgonjwa anayetibiwa.
 
Kuna uzi humu umeongelea mfumo madaktari katika sekta ya afya unaua sekta ya afya..na hichi ndicho kanichoonekana.

Hao jamaa wamechangia sana kuua sekta ya afya nchini..wengi sasa wamebakiza kuhodhi madaraka na ila hawa output yoyote ya maana.

Mfumo wa afya ubadilishwe..tofauti na hapa kila siku ni business as usual tu...kutoka kwa hawa incompetent MDs

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
MDs ni incompetent wengi sana yanasoma theory tu hayana kitu yamejaa wivu tu, Hio cannibalism waikubali haikwepeki MDs kaeni huko mahospitalini
 
Kwenye hicho chuo unachofundisha hamna kozi ya Famasi?

Kama ipo fanya utafiti wa mtaala wake ili ujue Wafamasia waajifunza nini, halafu uje uweke kipengele hicho kwenye bandiko lako.

Hospital yako inaitwaje? nipe kazi basi hapo
Nimekuambia wanayojifunza ni basics tu kwa ajili ya therapeutics na sito kubaini magonjwa. Kozi 99% imejikita kwenye utengenezaji na uhifadhi wa dawa. Kujipa kazi ya biashara ya dawa ni Tanzania tuu kutafuta ulaji ila kwa wenzetu haya hayapo.
 
Kwa hiki ulichoeleza hapa upo sahihi, kwa knowledge ya pharamacology ya daktari hawezi kujigamba kwamba anajua complexities zote zinazohusu dawa ikiwemo kiwango na namna inavyopaswa kutolewa na any variations zinazoweza kujitokeza.........na pia kama ulivyoeleza kuna swala la drug interactions ambapo dakatari anaweza kuandika mchanganyiko wa dawa ambao wewe pharmacist kwa uelewa mpana ulio nao ukaona amefanya kituko. Kwa hiyo naunga mkono hoja kwamba kila mmoja atambue na kufanya majukumu yake kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi badala ya kushadidia vitu ambavyo una uelewa wa juu juu tu au ule wa kawaida.
Wewe naye ni fake tu, daktari asijue namna dawa inayotolewa wakati ndiye anayejua ugonjwa na wadudu wake na kutoa Orders kwa Mfamasia atoe dawa leo unasemaje hajui?
 
Wewe bwana mimi ni Mtanzania ninayeishi South Africa, nimesajiliwa huku ingawa nafundisha madaktari and soon nitaanza kufundisha huko na pia Tanzania namiliki hospitali. Wanaonijua wapo humu humu hawaongei.

Shut up!!
Umeongea uchuro tu huna tofauti na mende MDs wapumbavu fulani tu tokeni acheni uchawi acheni uchawi, Endeleeni kutoa mimba za wanawake na watoto wa shule.
 
Naomba nikuulize kitu, katika hayo yote sijaona umeandika Pathophysiology. Kama hukusoma Pathophysiology, utasemaje unaweza kugundua dalili za magonjwa?


Kazi Diagnosis ya Mgonjwa ni ya daktari usitake kupoteza muda kwa ubishi hapa ndugu. Kazi ya Mfamasia kutoa dawa from the store or dispensing room kwa maelekezo ya daktari. Kama Doctor's prescription unatoaje dawa?
Huyu kaandika Kwa kifupi tuu...ila kapitie carriculum ya pharmacist ipoje

Alafu usiende direct kwenye conclusion,Nenda kaangalie

Responsibilities of Pharmacist in Hospital setting......ukijua HUTAKAA UONGEE UJINGA HUU
 
Back
Top Bottom