Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)

Baada ya kukukosa kwenye huku MCT, bandiko lako limekosa maana, unajiita MD, MMED, PhD wakati hautambuliki, maana we ni Dr wa mchongo.
Screenshot_20220519-080731.jpg
 
Mfamasia ana idea pia kuhusu dawa za mifugo , maana dawa nyingi zinafanana tofauti ni pharmacokinetics parameters ndio zinakuwa tofauti kidogo , sijajua kwenye mitaala ya kitanzania kwa wenzetu huwa wanasoma pia veterinary pharmacology semester 1 au 2.
Basi tuongee na Mzee Bashe ili wamiliki wa maduka ya dawa za mifugo na mimea wasome ADDO. Maana huku mtaani tunakula sana sumu zinazotokana na utumiaji mbaya wa pesticides katika mazao na dawa za mifugo hivyo kupelekea watu kuugua.
 
Mie nashauri ...kila mtu afanye kazi yake ....daktari aandike hizo prescription...
Mfamasia agawe dawa ....kwa kufuata prescription.... na kutengeneza dawa (hii kwa tanzania bado sana)

Prescription only medicines zisitolewe bila cheti cha daktari (hii haifuatwi sana nchini kwetu ) ...Controlled drugs tu ndio wapo makini nazo
 
Mteremko wa Addo umefutwaa mnaanza kulia liaa...!! No shortcut vinajaa rudini darasanii kama ambavyo mnasema hatuyajui magonjwa bhasi na nyie Dawa hamzijui vile vileee...
Lol, taifa linaweza ishi bila wafamasia, Ila haliwezi ishi bila madaktari. Shika adb
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kijana nchi hii haiwezi kuishi bila wanasiasaa sisi tuendelee kupoteza mudaa tuu hukuuu...!! Daktari huko vijijini hawajawahi hata kumwona ila wana Mbunge..diwani...mwenyekitii...
 
Madaktari wa bongo faka sana na wanatakiwa wawe regulated to the maximum, sitasahau kuna Dr mmoja tena Prof alinipa diagnosis fake ya kipumbavu na nusu inimalize kwa ajiri ya madawa niliyopewa kutibu ugonjwa ambao ulikuwa fake, sitasahau hilo
Pharmacy wakijaga lazima waulize tenaa Hivi hizi Dawa za Ugonjwa gani??[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] maana madoctor wa mchongoo sanaaa..
 
Unachotakiwa kufahamu Mtoa mada kila Taaluma ina eneo lake la kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria.

Suala la kutoa dawa ni eneo la Kisheria kwa Kada ya Famasi Ulimwengu mzima. Mafunzo ya ADDO yaliletwa na Mpango maalumu wa kusaidia upatikanaji wa dawa za msingi katika maeneo mengi ya nchi. Kisheria hakuna anayeruhusiwa kutoa dawa unless anatambuliwa na Baraza la Famasi. Baraza la Famasi lina Mamlaka ya kuamua nani awe nani asiwe mtoa dawa.

Kuhusu kwamba Wafamasia hawawezi kutoa dawa on their own hii inaonesha upeo duni ambao mtoa mada unao. Nchi mbalimbali zina mifumo ya kuruhusu Wafamasia na kada zingine mbali ya madaktari kufanya prescribing. Wanaruhusiwa ku prescribe kwa sababu Elimu wanayopata Vyuoni inawapa uwezo kubaini magonjwa na kwa kuwa Wana ufahamu mkubwa wa dawa basi wanaweza kutoa dawa hizo.Ushahidi kwa nchi ya Uingereza ni huu hapa.

evidence.nihr.ac.uk

Nurses and pharmacists can prescribe as effectively as doctors - NIHR Evidence

Did you know that when it comes to prescribing medication, nurses and pharmacists can do it just as effectively as doctors can?
evidence.nihr.ac.uk
evidence.nihr.ac.uk
Hapa Tanzania hatujawa na guidelines za kuruhusu Wafamasia au Wauguzi kuanza kuandika vyeti vya dawa kwa Wagonjwa. Hata hivyo zipo Kanuni za Makundi ya Dawa ( Scheduling of Medicines) ambazo zimegawanya dawa katika makundi 10. Kanuni hizo za mwaka 2015 zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2018 zimegawa dawa katika makundi 5 ya dawa za binadamu na makundi 5 ya dawa za mifugo.

Kwa dawa za binadamu makundi hayo ni
Schedule 1: Controlled na Psychotropic medicines
Schedule 2: Prescription Only Medicines
Schedule 3: Pharmacy Only Medicines
Schedule 4: General Sale Medicines
Schedule 5: Human ADDO Prescription Only medicines

Sasa ukienda Schedule 3 ya makundi ya dawa, imegawanyika katika makundi mawili, Behind the counter medicines , hizi ni aina ya dawa ambazo hazihitaji cheti cha Daktari ola lazima zitolewe na Mfamasia na pia kuna Over the Counter medicines ambazo hazihitaji cheti za Daktari wala kuhitaji Mfamasia azitoe. Sasa kwa mujibu wa Schedule 3 ya Kanuni za makundi ya Dawa za Tanzania , Mfamasia anazo dawa nyingi sana anazoweza kuzitoa kutokana na umahiri wake katika dawa bila ya kuhitaji cheti cha Daktari
 
Kudiagnose mfamasia pia anaweza ingawa anazidiwa na Daktari ambaye yupo, wale wa mchongo anazidiwa pia na mfamasia ambaye yupo deep. Diagnosis ndio jukumu kubwa na Daktari, Mfamasia hajawahi kulalamika hapa maana sio jukumu lake ingawa anaweza.

Kuprescribe ni jukumu la Dk kulingana na sheria zetu, ingawa Mfamasia anaweza pia hasa Clinical Pharmacist(huyu ana Master ya Clinical Pharmacy). Huko kwa wenzetu Wafamasia wanaruhusiwa kuprescribe kulingana na sheria zao
Hamna Mfamasia aliyelalamika kuwa Dk asiprescribe isipokuwa yeye anajukumu la kuhakiki dawa iliyoandikwa ni sahihi kulingana na tatizo la mgonjwa, kama haiko sahihi atatoa ushauri wake.
Hao wanafuata sheria zao walizojipangia ndio maana unaona ni tofauti na huku ambapo dawa zinatolewa hata kama zinahitaji cheti cha daktari

Sawa hata dr alie deep kazi za mfamasia anazifanya bila tabu japo at
Azidiwa kdgo na mfamasia
 
Anyanganywe huu uprofesa wake wa mchongo...andiko hili limemuacha uchi sana.
Anavyosema manesi wanazijua "wengi hawajui hata isotonicity " mbaka waphamacia tuwafanyie compounding.

Nesi mwingine namkuta anamazoea ya kuchoma watu penadour IV namwelewesha analeta ujuaji siku moja bado kidogo mgonjwa aukate ndo akaelwa namaanisha nini.
 
Wewe hapo ni 'valium', lakini naona huelewi hata hiyo 'pharmacology' ya diazepam' ipoje.

Ni Famasia yupi ambaye anadai kuwa kujua 'pharmacology' ndiko kutibu"? Ni Famasia yupi ambaye analilia majukumu ambayo siyo yake katika kumhudumia mgonjwa?
Hata hujui kwamba katika kutibu si jukumu la taaluma moja tu, hili nalo hulijui mpaka uelezwe?

"Description ya kazi" ya daktari ni kutoa dawa (dispense) kwa mgonjwa, toka lini na kwa sheria gani? Description ya kazi ya daktari ni kutunza dawa katika mazingira yanayotakiwa? Toka lini na wapi?

Hapa hakuna hoja ya kusoma 'pharmacology' au nini, ni swala la majukumu yaliyo wazi kwa kila mmoja wa watu wanaomhudumia mgonjwa. Mgonjwa siyo mali ya daktari, hawezi kuhodhiwa na daktari kama mali yake na kutaka afanye kila kitu yeye pekee kwa mgonjwa huyo.
Kaa dirishani subiri prescription ufunge dawa umpe mgonjwa, huna basics za kutibu ugonjwa.
 
Kama mtu ameaomea pre nursing au nursing tena ya mwaka mmoja halafu anaweza kugawa dawa na kumuelekeza mtumiaji je kwa MD itakuwa ajabu? Kwani hata Hawa wafamasia wa kibongo wana Nini kama si kugawa dawa tu? Wamegundua au kutengeneza dawa gani? Kujifanya wakubwa wakati hata panado hawawezi kutengeneza !!! Wafamasia wa kibongo ni wagawa dawa tu hakuna jingine wanalijua
Ahahahah wafamasia ujuaji mwingi sana.
Kama tu uwezo hata wa kutake history ukatoa diagnosis na DDx zake sasa utaprescribe nini?

Wao wakae dirishani watoe dawa kulingana na prescription pia wasisahau kuwasha friji ili dawa zitunzwe vizuri na MSD wakileta dawa wasisahau kuvaa shati nyeusi wakashushe mabox ya dawa.
 
WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)

WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
Mtoa mada hajui chochote kuhusu taaluma ya ufamasia. Si kweli kwamba wamafamasia kazi Yao ni kutengeneza tu viwandani, kwanza kwa Tanzania hata hivyo industrial pharmacy bado sana. Pili wafamasia kwenye mitaala Yao Wana course ya pharmacology inayo deal na drug administer, pamoja na magonjwa mbalimbali na viwango vya dozi ya huo ugonjwa. Na pia still wanasoma basics za pathology so wanajua dalili za magonjwa.
 
Kaa dirishani subiri prescription ufunge dawa umpe mgonjwa, huna basics za kutibu ugonjwa.
Wewe mbona unaililia hiyo kazi ya kukaa dirishani. Unataka nini huko?
"Kutibu mgonjwa" bila dawa utaweza?
 
Back
Top Bottom